Rais Kikwete atamani muda wake uishe akachunge ng'ombe!

Rais Kikwete atamani muda wake uishe akachunge ng'ombe!

Kwa hiyo una maana kuwa Rais JK hakuwafanyia wananchi chochote? Na hizo degree alizopata zimetokana na nini?

Degree kapewa tu kama alivyopewa suit 5. Uongozi ni mgumu hasa pale unapokosa vision kama kiongozi. Visionary leaders wanatamani waongezewe muda ili kukamilisha vision zao.
 
kwa ufupi ni kuwa kinachomuweka ikulu kwa sasa ni katiba tu lakini alishakimbia urais mapema tu... urais sio URAHISI jamani..
 
Jk alishatabiri kuwa kazi hii huwezi....wewe ukang'ang'ania....kisa eti na ww ni JK.....akililia wembe mpe umkate.
 
Ndio sababu alikuwa akikimbia nchi kila baada ya siku chache, alidhani Urais ni lelemama!? Matokeo yake ataiacha nchi katika hali mbaya sana kwenye kila sekta elimu, usafiri, maji, umeme, matibabu n.k.
 
Hakika kaongea kiprofesa zaidi. Ni maprofesa tu wanaweza kutoa kauli kama hizo

Wahenga walisema 'mtoto akililia wembe.........., sasa huyu mwana wembe wenyewe hakusubiri kupewa, aliupoka, umemkataje! Hautaki tena
 
“Hivi tunahitaji wazungu kuja
kutufundisha kuwa ni jambo baya kuua
raia wako? Unahitaji mzungu aje
kukwambia kuwa ni jambo baya
kuwafanyia ukatili na unyama wananchi
wako?”
HAPO JUU Namkumbuka Mwangosi.
 
Wachunga ng'ombe ni wasukuma na wamasai, ya wakwere wapi na wapi, labda kuuza korosho

ila hajasema anaenda kuchungia wapi, so anaweza akaenda hata usukumani. Si unamwona hata Benja yupo zake huko tanga?
 
unafiki tu, akachunge ng'ombe?? dhamira inamsuta alivyo ifanyia katiba ya wananchi. hata leo atoke tu mzururaji mkubwa!

mazuri yapo, tusione tu kasoro
 
Sasa kama raisi mwenyewe hajui kwanini nchi ni maskini unategemeanini
 
JK, he is worse., Sifa kuu ya kiongozi wa nchi yeyote ile duniani ni kujiamini, JK hakuwahi kujiamini hata siku 1 kama rais wa nchi amekuwa akipigwa danadana tu na wahafidhina tahamaki mda wake umekwisha nchi ina mpasuko mkubwa kikatiba, kisiasa, kiuchumi, ajira, maendeleo ya mtu mmoja mmoja, pato la mtanzania mmoja mmoja kwa siku sidhan kama inafikia shs 500., Fedha kushuka maradufu naskia sasa kuna coin ya shs mia 5, sijuwi ajaye atatoa coin ya shilingi ngapi. Tz bado muna kazi kubwa mbele mutahitahi miaka elf 1 zaid labda kufikia angalau nusu ya maisha ya hapa nilipo.
 
Hakika kaongea kiprofesa zaidi. Ni maprofesa tu wanaweza kutoa kauli kama hizo

Ukweli kabisa, ngoja "profesa dhaifu" apumzike safari, maanake hata popo huwa wanapumzika mchana lakini huyu dhaifu mchana na usiku yuko safarini, kwa kweli amechoka ngoja tu atamani kupumzika.
 
Rais mwingine lazima atakuwa bora kwani vigezo vya Kikwete alivyoweka si mchezo, amewapita Marais wote wa tatu kwa aliyoyafanyia Tanzania kwenye kila nyanja, kwa hiyo anaekuja inabidi ampite Kikwete, chini ya hapo tutamuona ni bogus tu.

Hapo sasa.
 
Back
Top Bottom