Rais Kikwete anaweza asikubali kukabidhi nchi CCM ikishindwa


Wapinzani nao wameonyesha kila dalili ya kutokubali kushindwa tuombe nao wakishindwa wakubali
 
CCM wote wana akili mbofu mbofu kama yako. January Makamba alipoulizwa iwapo CCM itakuwa tayari kukubali matokeo kama ikitokea ikashindwa uchaguzi alijibu, nanukuu. "CCM haijajiandaa kisaikolojia kushindwa, hatujawahi kufikiria kushindwa, na hatupo tayari kushindwa". Lowassa alipoulizwa iwapo atakubali matokeo alijibu, kama kutakuwa kuna proof beyond doubt kwamba uchaguzi ni huru na haki nitakubali matokeo.
Sasa kila mwenye akili hapa anajua ni nani aliyejiandaa kwa vita. CCM msidhani ninyi ni mhimu zaidi kuliko mamilioni ya watanzania waliochoshwa na ubabaishaji wenu.
 
Tusimwombe Amani bila kuwajibika tukapige kura then tuone kama ushindi upo halafu kikwete asikabidhi nchi
 
Mbona wa Nigeria alikabidhi nchi kwa mpinzani vizuri tuu. Ndo ukomavu wa demokrasia. Asie kubali kushindwa sio mshindani, yaani kwa pande zote. Ila uwe ushindi halali na ashindwe halali, pasipo na figisu figisu za matokeo.

We unataka nani ashinde ili ionekane kashinda kihalali weka wazi uwe huru
 

"unguja" Unachokipanda kichwani mwako ni vumbi inayotibuka kutaka kuwasadikisha watu vumbi lako. Kalale umeishiwa nyimbo wewe bana huna jipya zaidi ya kiweweseka tu.

Taifa lenye watu makini na amani yao hawawezi kudiriki kufanya au kufuata vumbi yako. Kama umetumwa kuharibu amani yetu kamwambie aliyekutuma "HAO WATANZANIA BWANA NI WATU WENYE BUSARA NA HEKIMA MAANA MATAIFA YA AFRIKA WANAOMBA KUJIFUNZA NAMNA TZ ILIVYOSIMAMA IMARA KWENYE SUALA LA MARAIS KUACHINA MADARAKA KWA AMANI NA UPENDO MKUBWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…