Rais Kikwete anaweza asikubali kukabidhi nchi CCM ikishindwa

Wadau nimefuatilia matamshi kadhaa wa kadhaa ya mkuu wetu inaonekana dhahiri shairi kutokuwa tayari kukabidhi madaraka kiungwana kwa Rais ajaye kama CCM ikishindwa.

Rai yangu kwa Watanzania wote wapenda haki na amani tuombe sana na kwa mzigo juu ya taifa letu.

Ajenda za kuombea 1) Mungu aingilie kati Tume ya Uchaguzi itende haki.

(2) Mungu aingilie kati mamlaka iliyopo ya nchi iweze kukabidhi madaraka bila misuguano wala vurugu.

Wapinzani nao wameonyesha kila dalili ya kutokubali kushindwa tuombe nao wakishindwa wakubali
 
Nchi hii si ya wapiga dili, pia anayewambia kuwa ccm inashindwa ni nani? watu wenyewe mnatapatapa mara mnashitaki ICC hii ni akili ndogo ya gege la wapiga dili, kwa akili ndogo wanaona kuwa wanamtisha JK- JK ni mtoto wa mjini kuliko hilo genge mara 100- upande Mr.0 upande ED, kweli inadhihirisha chadema haina viongozi makini.
CCM wote wana akili mbofu mbofu kama yako. January Makamba alipoulizwa iwapo CCM itakuwa tayari kukubali matokeo kama ikitokea ikashindwa uchaguzi alijibu, nanukuu. "CCM haijajiandaa kisaikolojia kushindwa, hatujawahi kufikiria kushindwa, na hatupo tayari kushindwa". Lowassa alipoulizwa iwapo atakubali matokeo alijibu, kama kutakuwa kuna proof beyond doubt kwamba uchaguzi ni huru na haki nitakubali matokeo.
Sasa kila mwenye akili hapa anajua ni nani aliyejiandaa kwa vita. CCM msidhani ninyi ni mhimu zaidi kuliko mamilioni ya watanzania waliochoshwa na ubabaishaji wenu.
 
Tusimwombe Amani bila kuwajibika tukapige kura then tuone kama ushindi upo halafu kikwete asikabidhi nchi
 
Mbona wa Nigeria alikabidhi nchi kwa mpinzani vizuri tuu. Ndo ukomavu wa demokrasia. Asie kubali kushindwa sio mshindani, yaani kwa pande zote. Ila uwe ushindi halali na ashindwe halali, pasipo na figisu figisu za matokeo.

We unataka nani ashinde ili ionekane kashinda kihalali weka wazi uwe huru
 
Wadau nimefuatilia matamshi kadhaa wa kadhaa ya mkuu wetu inaonekana dhahiri shairi kutokuwa tayari kukabidhi madaraka kiungwana kwa Rais ajaye kama CCM ikishindwa.

Rai yangu kwa Watanzania wote wapenda haki na amani tuombe sana na kwa mzigo juu ya taifa letu.

Ajenda za kuombea 1) Mungu aingilie kati Tume ya Uchaguzi itende haki.

(2) Mungu aingilie kati mamlaka iliyopo ya nchi iweze kukabidhi madaraka bila misuguano wala vurugu.

"unguja" Unachokipanda kichwani mwako ni vumbi inayotibuka kutaka kuwasadikisha watu vumbi lako. Kalale umeishiwa nyimbo wewe bana huna jipya zaidi ya kiweweseka tu.

Taifa lenye watu makini na amani yao hawawezi kudiriki kufanya au kufuata vumbi yako. Kama umetumwa kuharibu amani yetu kamwambie aliyekutuma "HAO WATANZANIA BWANA NI WATU WENYE BUSARA NA HEKIMA MAANA MATAIFA YA AFRIKA WANAOMBA KUJIFUNZA NAMNA TZ ILIVYOSIMAMA IMARA KWENYE SUALA LA MARAIS KUACHINA MADARAKA KWA AMANI NA UPENDO MKUBWA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom