Rais Kikwete anastahili sifa

Rais Kikwete anastahili sifa

Sifa kweli anazo nyingi!
1)Rais asiyejua nchi yake kwanini Masikini!!!-Na bado anaongoza
2)Rais pekee duniani ambaye hajui kazi ya Makamu wa Rais !
3)Rais aliyevunja Rekodi za kusafiri za Marais etc
 
2015,bado sana!ni mapema kumsifia kihivyo wakati bado tuna miaka 2 1/2 mbele.Mapema sana,sijui kama atatoboa?
 
hapana nasema hapana TO THE WEAKNESS AS THE POINT OF VIEW.HASTAHILI ATA KIDOGO YUKO WAPI ALIEMUUA MWANGOSI,WATESAJI WA ULIMBOKA NA KIBANDA NA VIPI MAUAJI YA ARUSHA JE MFUMUKO WA BEI UONI.

"THE DIFFERENCE BETWEEN THE STUPIDITY AND GENIUS IS THAT GENIUS HAS ITS LIMITS" ALBERT EINSTEIN.
 
Alituomba kazi ya Uraisi na tukampa, sasa kama anafanya kazi yake kuna sababu gani ya kumsifia?. Kumbuka kwamba tunamlipa mshahara mkubwa na malupulupu kibao.
 
Kuna waliosema mheshimiwa rais hatoboi 2015 yaani angekuwa amengatuka mapema,baada ya kumtuhumu kuwa mambo mengi ameyafumbia macho.
Atawezaje wakati zimempungua kwenye hicho kitu alichokitwisha juu ya shingo analiita kichwa.
Kwake na kwa kila mtu wa aina yake kama wewe kila kitu sawa tu.
By the way unajua hadithi za mfalme Juha?
 
Imebakia miaka 2 tu akamilishe safari ngumu na nzito,basi mimi nimeona nimtakie kazi njema na yenye mafanikio,kiukweli anastahili sifa.
Na unaona mahali ambapo Yeye kikwete na wewe na wengine wa aina yenu wanapo-capitalize?
"Imebakia miaka 2 tu...."
Urais kwake na kwenu ni kuhesabu miaka?
Minane imepita bado miwili....?
  1. Content?
  2. Quality
  3. Quantity
Nakupa tu hints ili uje tena uweke mada yako vizuri.
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete anastahili sifa,mimi kama Mtanzania nampa pongezi rais Kikwete kwa kuongoza nchi katika hali ya amani na utulivu.

Kuna waliosema mheshimiwa rais hatoboi 2015 yaani angekuwa amengatuka mapema,baada ya kumtuhumu kuwa mambo mengi ameyafumbia macho.

Unajua nchi haiongozwi kwa jinsi tunavyotaka sisi.Kiukweli nchi ilifika mahali iliyumba ila mwanaume wa shoka rais kikwete alituliza akili zake akafumua uongozi mambo yakaenda shwari.

Wapo waliomuombea mabaya ila rais hakuwajali sana alijitahidi mpaka hapa tulipofika.

Imebakia miaka 2 tu akamilishe safari ngumu na nzito,basi mimi nimeona nimtakie kazi njema na yenye mafanikio,kiukweli anastahili sifa.
Unapotoa credit kwa kitu fulani ni lazima unafanya ulinganishi(comparison) ya hiyo kitu na kitu kingine chenye uhusiano au ufanano.

Unapompa sifa Rais kikwete kuwa ameongoza vizuri, ila tu kwa sababu moja tu, amani na utulivu inakubidi ulinganishe na awamu zilizopita, binafsi natilia shaka hizi sifa kama ni sifa za dhati toka moyoni au ziko corrupted.

Je, rais ametimiza ahadi alizoahidi kwa kiwango gani?, Je, wewe unadhani aliingia madarakani kwa ajili ya kuleta utulivu na amani tu?

Tangu nchi yetu ipate uhuru, ni kipindi cha JK pekee ambacho tumeshuhudia ukosefu wa amani na utulivu kama vile mauaji ya albino, kutekwa na kuumizwa kwa watu maarufu, mapigano ya kidini yaliyosababisha mauaji sanjari na kupigwa risasi na kuuawa kwa viongozi wa dini. Haya mambo yametokea katika kipindi hiki cha JK na katika tawala zilizotangulia hatukuwahi kuyashuhudia.

Leo wewe unasimama hadharani tena mchana kweupe na kusifu kuwa ameongoza kwa amani na utulivu, huoni aibu?
 
Ukiona mtu anaposti thread kama hii kwa hali ilivyo hivi sasa hapa nchini ni lazi ujuulizwe maswali mengi juu ya uwezo wa kufikiri wa huyu mtu kwa mfano: Ivi ni kweli huyu mtu hawaoni wagonjwa wanafariki kila siku kwa magonjwa yanayotibika kisa kakosa dawa? Ivi ni kweli huyu mtu hafahamu kuwa uwanja wandege ukiweka shilingi mfukoni unajulikana lakini twiga walipita bila kujulikana? Ivi ni kweli hafahamu sababu za kuuwawa daudi mwangosi? Ivi ni kweli mtu huyu hafahamu tatizo la udini linaloendelea hivi sasa linasababishwa na nn? Hivi ni kweli huyu mtu hajui mgawanyiko uliopo ndani ya CCM umesababishwa na nn? Hivi huyu mtu hajui kabisa kwa nn wadogo zetu fm 4 walifeli kiasi kile? Kama hajui mambo hayo basi hakustahili hata kuisumbua keyboard yake kuposti upuuzi huu.
 
kikwete mwanaume wa shoka?

Alikuonyesha wapi uanamme wake wa shoka.?
 
mungu mkubwa wote waliokuja na silogani ya nchi haitatawalika. Sasa wanaona aibu kila kona wanayopita, sasa wamebaki kulalama na katiba mpya, katiba ambayo wenyewe waliichekelea pale ikukummheshimiwa alipowapa nafasi ya kuwasikiliza.

Eleza vizuri. Sifa nzuri au mbaya?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete anastahili sifa,mimi kama Mtanzania nampa pongezi rais Kikwete kwa kuongoza nchi katika hali ya amani na utulivu.

Kuna waliosema mheshimiwa rais hatoboi 2015 yaani angekuwa amengatuka mapema,baada ya kumtuhumu kuwa mambo mengi ameyafumbia macho.

Unajua nchi haiongozwi kwa jinsi tunavyotaka sisi.Kiukweli nchi ilifika mahali iliyumba ila mwanaume wa shoka rais kikwete alituliza akili zake akafumua uongozi mambo yakaenda shwari.

Wapo waliomuombea mabaya ila rais hakuwajali sana alijitahidi mpaka hapa tulipofika.

Imebakia miaka 2 tu akamilishe safari ngumu na nzito,basi mimi nimeona nimtakie kazi njema na yenye mafanikio,kiukweli anastahili sifa.

mwanaume wa shoka anakuwaga IMPOTENT? hii nchi ni semi-bikira jamaa kashindwa kuizalisha anashangaa eti hajui kwa nini haizai
 
Unapotoa credit kwa kitu fulani ni lazima unafanya ulinganishi(comparison) ya hiyo kitu na kitu kingine chenye uhusiano au ufanano.

Unapompa sifa Rais kikwete kuwa ameongoza vizuri, ila tu kwa sababu moja tu, amani na utulivu inakubidi ulinganishe na awamu zilizopita, binafsi natilia shaka hizi sifa kama ni sifa za dhati toka moyoni au ziko corrupted.

Je, rais ametimiza ahadi alizoahidi kwa kiwango gani?, Je, wewe unadhani aliingia madarakani kwa ajili ya kuleta utulivu na amani tu?

Tangu nchi yetu ipate uhuru, ni kipindi cha JK pekee ambacho tumeshuhudia ukosefu wa amani na utulivu kama vile mauaji ya albino, kutekwa na kuumizwa kwa watu maarufu, mapigano ya kidini yaliyosababisha mauaji sanjari na kupigwa risasi na kuuawa kwa viongozi wa dini. Haya mambo yametokea katika kipindi hiki cha JK na katika tawala zilizotangulia hatukuwahi kuyashuhudia.

Leo wewe unasimama hadharani tena mchana kweupe na kusifu kuwa ameongoza kwa amani na utulivu, huoni aibu?

Sasa ulitaka asemeje rafiki? Ila binafsi nakushukuru kwa kumtambua kwamba yeye ni Rais,kwani kufanya hivyo ni uthibitisho tosha sifa anazopewa anastahili na ndizo anazo.

Hivi usipomsifu kiongozi wako wa nchi yako, utamsifu kiongozi wa nchi gani?.Na kama utamsifia kiongozi wa nchi fulani,je ulikwisha wahi

kuishi huko? Na kama ulikwisha wahi ishi huko,ni kitu gani kilikuleta nchini Tanzania?

Ndugu yangu,jenga utamaduni wa kusifia cha nyumbani na kama kuna mapungufu ni bora ukatoa mapendekezo/maelekezo yenye tija

kuliko kuwakatisha tamaa wenzako,mbaya zaidi kuwaona wenzako ni majuha ila wewe ni bora mwenye upeo mkubwa wa kufikiri.

Mwisho,ni vema ukaelewa kuwa vyote hivyo unavyomtuhumu Mh.Rais eti vimetokea kwa sababu yake vingeweza kutokea kwa kiongozi

yoyote yule kwani masuala ya udini,usalama wa waandishi wa habari,mauaji ya ablino na utesaji yamejitokeza karibu nchi nyingi sana

duniani.Natumaini wewe ni mwelevu sana ebu fanya utafiti katika baadhi ya nchi zikiwemo nchi jirani utagundua kwamba hapa Tanzania

kuna uhuru mkubwa sana,sema tu kuna baadhi ya watu,makundi fulani yanatumika kuchafua uhuru wetu kwa maslahi yao na makundi

yao.
 
Sasa ulitaka asemeje rafiki? Ila binafsi nakushukuru kwa kumtambua kwamba yeye ni Rais,kwani kufanya hivyo ni uthibitisho tosha sifa anazopewa anastahili na ndizo anazo.

Hivi usipomsifu kiongozi wako wa nchi yako, utamsifu kiongozi wa nchi gani?.Na kama utamsifia kiongozi wa nchi fulani,je ulikwisha wahi kuishi huko? Na kama ulikwisha wahi ishi huko,ni kitu gani kilikuleta nchini Tanzania?

Ndugu yangu,jenga utamaduni wa kusifia cha nyumbani na kama kuna mapungufu ni bora ukatoa mapendekezo/maelekezo yenye tija kuliko kuwakatisha tamaa wenzako,mbaya zaidi kuwaona wenzako ni majuha ila wewe ni bora mwenye upeo mkubwa wa kufikiri.
Nimerudia tena kusoma post yangu, hakuna sehemu nimesema kuwa wenzangu ni majuha na mimi nina uwezo mkubwa wa kufikiri, ila tu nilikuwa namkumbusha mleta mada alinganyishe utawala ya JK na tawala zilitangulia halafu aseme ni wapi amani imepotea?.

Si kweli kwamba mtu akiwa Raisi basi anatakiwa kusifiwa tu hata kama anavurunda, eti kwa kuwa ni kiongozi wa nchi yangu, kusifia uongozi katika hatua tuliyonayo Tanzania ni kukosa uzalendo.

;Ufaulu umeshuka sana.
;Deni la taifa limekua sana.
;Mfumuko wa bei unatisha.
;Thamani ya sarafu yetu imeshuka mno.
;Umasikini unaongezeka.
;Ajira zilizoahidiwa kwa vijana hazionekani.
;Ujangili unamaliza tembo wetu pamoja na wanyama wengine.
;Udini unatishia mustakabali wa taifa n.k, n.k,

Wewe unayetaka tumsifie kiongozi wetu(Raisi) pamoja na ukweli huu badala ya kumkosoa ili arekebishe mambo,
Unalitakia mema taifa letu kweli au haujali hata likiangamia?
 
That rotten mind piece of shit doesn't deserve a thing,him and Kinana-the-Poacher belong behind bar.
 
Sifa kubwa si kusafirisha nyara za serikali nje ya nchi kupitia kwa KINANA family
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom