Rais Kikwete amuumbua John Tendwa

Rais Kikwete amuumbua John Tendwa

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete amewataka wajumbe wapya wa NEC wa CCM kutokulala bali kuzunguka kila kona ya nchi kufanya mikutano ya hadhara,kuingiza wanachama wapya na kueneza sera za chama hicho.

Rais Kikwete amesema kazi hiyo ikamilike kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 kisha iendelee mpaka uchaguzi mkuu wa 2015.Rais Kikwete amesema hiyo ndiyo njia pekee itakayokipa ushindi mkubwa chama hicho kwenye chaguzi zijazo.Rais amesema kamwe chama kisichozunguka kwa wananchi kuhutubia na kueneza sera lazima kitaangamia.

Itakumbukwa ni hivi karibuni Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa alitishia kupiga marufuku chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kuendelea na operesheni yake ya M4C kwa kile alichodai amesitisha operesheni zote mpaka nyakati za uchaguzi.Alisema akiwa kama msajili wa vyama kamwe hatakubaliana na operesheni za CDM za kujijenga.

Naye Mhadhiri wa chuo kikuu cha DSM Dr Benson Banna alimuunga mkono Tendwa kwa kusema Operesheni ya CDM ya M4C haikubaliki kwani ni kuwasumbua wananchi na kuwanyima muda wa kufanya kazi na kuwataka CDM wasubiri kipindi cha uchaguzi.

Kama vile ni mpango mahususi ulikuwa umepangwa nayo Kamati ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi maarufu kama kamati ya Nchimbi iliungana na Tendwa katika moja ya mapendekezo yake kuitaka serikali kupitisha sheria ya kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa mpaka nyakati za uchaguzi.Pendekezo hilo lilisema shughuli zote za siasa baada ya chaguzi zihamie bungeni.

Kauli ya Rais Kikwete ya leo imeonekana waziwazi ni kupingana na kauli ya msajili wa vyama vya siasa John Tendwa na Msajili huyo ameonekana wazi hafai kuendelea kushikilia wadhifa huo.

Source: ITV/Chanel Ten.
 
Wote vigeugeu tu...Kwa ufupi CCM ilikuwa haijajipanga, sasa wanahisi wanaweza kuchechemea hususan baada ya moles walioko CDM kuwasilisha ripoti maalum...
 
Binafsi nimemsikia Rais akiongea.Nina uhakika Tendwa hatathubutu kufungua mdomo wake tena.Ninaweza kusema ameaibishwa vibaya.
Tendwa alipiga marufuku M4C kwa kudhani anaifurahisha sana CCM.
 
Habari za kibongobongo, unasoma mwanzo mpaka mwisho hamna direct quote hata moja. Kwa mtu anayejali usahihi wa habari ni lazima kujiuliza kama habari ni sahihi au ni maluweluwe ya muandishi.

Muandishi angeipa habari yake nguvu zaidi kama angeweka nukuu ya maneno halisi aliyotumia Tendwa na maneno halisi aliyotumia Kikwete ili tuweze kujua kama anachodai ni kweli au katia chumvi.

Bila hilo habari inakosa uhakika na context.
 
Dah ! John Tendwa tena ! Huyo mbona tushamgomea hatutashirikiana naye tena .
 
tatizo ni viongozi wa ccm kufanya kazi kwa kuwaiga chadema.wanashindwa kupanga mikakati ya kuwafikia wananchi na kuishia kuilaumu chadema.shame on you ccm.
 
Habari za kibongobongo, unasoma mwanzo mpaka mwisho hamna direct quote hata moja. Kwa mtu anayejali usahihi wa habari ni lazima kujiuliza kama habari ni sahihi au ni maluweluwe ya muandishi.

Muandishi angeipa habari yake nguvu zaidi kama angeweka nukuu ya maneno halisi aliyotumia Tendwa na maneno halisi aliyotumia Kikwete ili tuweze kujua kama anachodai ni kweli au katia chumvi.

Bila hilo habari inakosa uhakika na context.

Mtoto una Kiranga wewe!!!! Amekwambia source ITV na Channel Ten, hebu acha uvivu basi kesho fuatilia you tube ya ITV wana tabia ya kutupia habari za kitaifa.
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti kawagiza wajumbe wa nec hahahaha hapo mama salma atakuwa busy na wilaya yake lindi then mzee mwenyewe anaendlea kupiga pole pole watoto wa lundega tena juzi tu ndo wametoka kwenye kambi..
 
Hata hivyo viongozi wa CDM wana uzalendo mkubwa sana katika programe zao tofauti na CCM ambao itwagharimu fedha nyingi kutokana na wanachama wake kutokuwa wazalendo na kuamini chama ni sehemu ya kuchuma.

Ili wafanikiwe labda watangaze kuchukua rushwa ruksa.
 
Mkuu Molemo

Umeeleza vizuri sana.Ni kweli JK amewataka viongozi wapya wazunguke kila kona ya nchi kuhutubia mikutano ya hadhara.Na kwa kweli hii ni sahihi kabisa.

Lakini pia ikumbukwe CDM ikianza operesheni zake inazuiwa na vyombo vya dola hata kuua watu kama ilivyotokea kule Morogoro na Iringa.Isitoshe Msajili bila aibu badala ya kutetea mikutano ya CDM yeye anaungana na polisi kulaani CDM na kusema CDM isubiri nyakati za uchaguzi ndiyo ifanye mikutano.

Sasa hapa wajanja tunajiuliza vipi tena CCM wanatakiwa kuzunguka nchi nzima ilihali msajili.wa vyama alishasema mikutano isubiri nyakati za uchaguzi?

Hakika Tendwa amepwaya sana kwenye nafasi yake!
 
Mtoto una Kiranga wewe!!!! Amekwambia source ITV na Channel Ten, hebu acha uvivu basi kesho fuatilia you tube ya ITV wana tabia ya kutupia habari za kitaifa.

Kati yangu mie ninayetahini kuondoa uhaini na muandishi anayeleta habari nusunusu nani mvivu?

Tutajuaje kwamba kauli ya Tendwa haikuwa na qualification ambayo haijatajwa hapo kwenye habari?

Huu mwaka 2012, uchaguzi ni 2015, unataka tuamini kwamba Tendwa kapiga marufuku mikutano yote ya siasa mpaka uchaguzi ujao? No qualification, no explanation?
 
Habari za kibongobongo, unasoma mwanzo mpaka mwisho hamna direct quote hata moja. Kwa mtu anayejali usahihi wa habari ni lazima kujiuliza kama habari ni sahihi au ni maluweluwe ya muandishi.

Muandishi angeipa habari yake nguvu zaidi kama angeweka nukuu ya maneno halisi aliyotumia Tendwa na maneno halisi aliyotumia Kikwete ili tuweze kujua kama anachodai ni kweli au katia chumvi.

Bila hilo habari inakosa uhakika na context.

Kiranga mkuu wangu

Wewe ndiye unayetaka kuliongopea jukwaa.Nimesikiliza taarifa ya habari ni kweli Kikwete ametoa agizo hilo.Pili ni kweli Tendwa alishakaririwa kuzuia operesheni za CDM za M4C mpaka bila aibu yoyote akatishia kufuta CDM wakiendelea na operesheni zake.

Sasa mkuu wangu kwanini usichutame tu mtu mzima kama Molemo kakugusa kwa hoja yake? Kwanini utake kusimama huku ukiwa uchi?
 
Tendwa na Benson Bana wote wana akili za matope, wako kujipendekeza kwa Mkwele kama malaya waliokosa wateja. Sasa Mkwele kaamua kuwaumbua live ili waache kuropokaropoka ovyo.

*Halafu huyu Kikwete yeye anasakizia makada wenzie waende mitaani kwenda kupayuka wakati yeye wenyewe anasafiri kama popo nje ya nchi.

*Ombi langu kwa wanaCCM tusiende huko mitaani mpaka Kikwete aanze yeye, kama aibu tuvune wote. Kikwete anadhani mziki wa M4C ni wa kitoto, aje uwanjani aone moto ukoje?

*Halafu huyu Kikwete hana hata shukrani kabisa, kwani CCM nao si walikuwa na mikutano sambasamba na ile ya Chadema?
CHADEMA walipozindua operation zao za M4C na CCM nao walizindua Operation vua gwanda!! na wakafanya mikutano mikubwa Dar, Tabora, Rukwa, Kigoma, Mwanza na kupita vijijini tena ikiongozwa na Nape, Mwigulu, Mwanry, Sitta, Magufuri, Mwakyembe, Tibaijuka nk
Vipi tena? Haikuwa na mafanikio? Ilikuwa imedoda?
 
Habari za kibongobongo, unasoma mwanzo mpaka mwisho hamna direct quote hata moja. Kwa mtu anayejali usahihi wa habari ni lazima kujiuliza kama habari ni sahihi au ni maluweluwe ya muandishi.

Muandishi angeipa habari yake nguvu zaidi kama angeweka nukuu ya maneno halisi aliyotumia Tendwa na maneno halisi aliyotumia Kikwete ili tuweze kujua kama anachodai ni kweli au katia chumvi.

Bila hilo habari inakosa uhakika na context.

Umeona mkuu na wewe
Yaaani premises na conclusion mbalimbali....................mtu kakurupuka tu na mihemko yake basi anapost!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kati yangu mie ninayetahini kuondoa uhaini na muandishi anayeleta habari nusunusu nani mbishi?

Tutajuaje kwamba kauli ya Tendwa haikuwa na qualification ambayo haijatajwa hapo kwenye habari?

Huu mwaka 2012, uchaguzi ni 2015, unataka tuamini kwamba Tendwa kapiga marufuku mikutano yote ya siasa mpaka uchaguzi ujao? No qualification, no explanation?

Kiranga

Kushangaa kwako kama Tendwa alisema hivyo,ndipo na sisi tunaposhangaa Tendwa kwanini aachwe kukaa ofisini mpaka leo huku akiwa anaropoka hovyohovyo maneno ambayo mpaka leo hii wakina Kiranga wanashangaa kusikia Tendwa alisema hivyo.
 
Habari za kibongobongo, unasoma mwanzo mpaka mwisho hamna direct quote hata moja. Kwa mtu anayejali usahihi wa habari ni lazima kujiuliza kama habari ni sahihi au ni maluweluwe ya muandishi.

Muandishi angeipa habari yake nguvu zaidi kama angeweka nukuu ya maneno halisi aliyotumia Tendwa na maneno halisi aliyotumia Kikwete ili tuweze kujua kama anachodai ni kweli au katia chumvi.

Bila hilo habari inakosa uhakika na context.

Ni habari ya kweli.
 
Umeona mkuu na wewe
Yaaani premises na conclusion mbalimbali....................mtu kakurupuka tu na mihemko yake basi anapost!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu Olesaidimu

Wakati mwingine nyie wana CCM muwe munakubali ukweli.Mlimuunga mkono sana Tendwa hapa jamvini alipotoa ile kauli ya kihuni kuzuia CDM.Leo JK kaeleza ukweli kuhusu kazi ya chama cha siasa kinapaswa kufanya nini.

Sasa unalalamika nini mkuu wangu?
 
Chadema mmechanganyikiwa na safu ya mashambulizi. Nyie mlikuwa mnahamasisha furugu na kujidai eti mnafungua matawi na hata kutaka kuvuruga zoezi la sensa. Hapa hamtwambii kitu tendwa siyo mtoto anajua mbivu na mbichi. Mkuhubiri vurugu mtaipate kama yule jamaa yenu yule yule na niiiii hahaha
 
Ni habari ya kweli.

Ukweli ni upi?

Sisemi kwamba habari ni ya uongo, natahini details. Natafuta kauli halisi aliyosema Tendwa. Sisemi kwamba Tendwa hawezi kusema uozo, nasema pia kwamba kwa sababu za kisiasa watu hawako beyond kusema "Tendwa kapiga marufuku CHADEMA kufanya mikutano" hata kama kasema "Jirekebisheni na dhibitini vurugu la sivyo mikutano yenu itapigwa marufuku mpaka kipindi cha uchaguzi".

Ndiyo maana natafuta maneno halisi aliyosema Tendwa na aliyosema Kikwete.

Hizi habari za redio mbao, tunaambiwa katika information theory kila habari inapopitia kigingi kimoja inabadilishwa kidogo, kiasi kwamba kitu kilichoanza kwa kusemwa "Masikini akipata, m.atako hulia mbwata" kinaishia kutafsirika kama "Maskini akipata m.atako, hulia mbwata".

Hapo utaona ni maandishi, na sijabadilisha chochote zaidi ya sehemu ilipo comma tu, na maana nzima ya sentensi imebadilika, kama unajua kusoma.

Sembuse hii habari ya kuhadithiwa na mtu aliyehadithiwa?

Weka direct quotes hapa tutaelewana. Vinginevyo kila kitu suspect.
 
Hii tabia ya kuandika habari kwa maneno jumlajumla bila direct quote tunayo sana. Natafuta direct quote/ video ya Tendwa, to no avail.
 
Back
Top Bottom