Rais Kikwete amtimua Mwenyekiti wa Bodi Bandari

Una uhuru wa kusema lolote maana JF imetupa uhuru huo lakini nimeshasema na narudia tena, SIFANYI KAZI TPA, sina ndugu TPA wala rafiki. Bora TICTS nina washkaji huko nilikuwa nao wakati nikifanya research 2007.

By the way, mnachanganya sana kila kitu kuitupia lawama TPA. Hivi hamjui kuwa TICTS wanafanya pia kazi kama za TPA tena kwa kiwango kikubwa kuliko TPA? Hamjui kama TICTS wanapakua mizigo na kupakia?? Hamjui kama wizi pia waweza kutokea TICTS wakati wa kupakua? Hamjui kuwa mizigo inayopitia TICTS haikusiani hata chembe na TPA?

Mnahitaji kupewa elimu sana ili muelewe maana inawezekana mnafuata mkumbo tu bila kujua.

We unaonekana ni kiraza wa ajabu,na hata hiyo desertion yako ilipitishwa kwa hongo.haya mambo c tunayajua vizur kuliko wewe uliyekua unapita tu na Kipara wambea wa TICTS unaowaita washkaji.hivi mawazir wakiboronga anaelaumiwa si ni rais!

Tics ikiboronga inalaumiwa mamlaka inayoisimamia(TPA).Tics haiko pale independently.jipange kaka NA master yako ya kichina
 
Do whatever they can kama hawatapunguza mudsa wa meli kusubili hili zipakuliwa tutazidi kupiteza wateja. Meli inatoka Salala mpaka Dar kwa siku kumi inasubili kupakuliwa kwa week tatu. Ni mfanya biashara gani atakubali upuuzi huo?
 
JK kama askari wa Kihindi vile, jamaa washatawanyika wao ndo wanaingia. Hahaaaaahahaaa hongera lakini Baba Ritz kwa kazi nzuri!!!!

Mkuu jiheshimu unajua kama unafanya makosa Name Calling?
 
Last edited by a moderator:
Wana JF,

Rais Kikwete amemtimua mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari TPA Raphael Mollel kuanzia tarehe 16 Januari na badala yake Amemteua Profesa Msambichaka kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo.

Updates:

Taarifa kamili ya IKULU Leo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Mamlamka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) .

Katika uteuzi huo Rais Kikwete amemteua Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa TPA na kutengua uteuzi wa Bwana Raphael Mollel, ambaye alikua anashikilia wadhifa huo. Prof. Msambichaka ni Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Mbeya.

Rais Vilevile amemteua Bwana Severine M.A Kaombwe, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRL. Bwana Kaombwe ni Mtaalam wa Usafirishaji (East Africa Corridor Diagnostic Study for Northern and Central Corridors).

Kulingana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peniel Lyimo, uteuzi huu unaanza tarehe 16 Januari, 2013.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishiwa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam
18 Januari, 2013

KWENYE RED: Tafadhali msiniulize ndivyo mwandishi wa Rais alivyoandika katika taarifa yake. Lakini sijawahi kukisikia chuo hicho.

Tunampongeza kwa hilo ila nataka kusema kwamba tatizo si kuondoa huyu na kumuweka yule bila kuondoa management yote na kuweka mpya bado haisaidii kwani naweza kuifananisha na mitambo mikukuu unaiwekea betri mpya jambo ambalo utaifanya hata nguvu ya betri mpya yake inyonywe kabisa.
 
We unaonekana ni kiraza wa ajabu,na hata hiyo desertion yako ilipitishwa kwa hongo.haya mambo c tunayajua vizur kuliko wewe uliyekua unapita tu na Kipara wambea wa TICTS unaowaita washkaji.hivi mawazir wakiboronga anaelaumiwa si ni rais!

Tics ikiboronga inalaumiwa mamlaka inayoisimamia(TPA).Tics haiko pale independently.jipange kaka NA master yako ya kichina

Asante mkuu we mjuaji sana naomba nikuache maana ukimwamsha aliyelala utalala wewe. Na pia ni uendawazimu kumuelewesha mwendawazimu maana hatakuelewa kutokana na wendawazimu wake.
Kila la kheri
 
(off topic): hivi pinda yupo nchini.
Mi naona ka kaususa u PM.
Any way, liwalo na liwe.
 
Pole mkuu wala usihangaishe kichwa na kupata tabu. Research yangu ya Masters niliifanya mwaka 2007 ilinifikisha TICTS na nilikaa nao nikifanya OBSERVATION kwa miezi mitatu na ndipo nilipojua mambo mengi ya Bandari. Lakini Bahati mbaya nafanya kazi kwenye sekta nyingineeeeeee isiyohusiana hata chembe na Bandari. Kama mdadisi fuatilia TICTS mtu aliyefanya research kipindi hicho kwao.
Mkuu,
Hiyo research yako kwa sasa ina miaka zaidi ya mitano toka ifanyike. Things have become even worse.
Hiyo sekta naomba tukubaliane, ilikuwa imejengeka kwenye msingi kama wa organised crime. Wanafanyakazi wanafahamiana, wanashirikiana na wanalindana katika kulihujumu taifa. Hilo haina ubishi.

Kawaida ya crime cartel, hairuhusu mtu wa nje kuingia kwenye ring yao na ndiyo hii inayotokea kw Mh. Mwekyembe kupigwa majungu na kuwa undermined ili kionekane kile anachokifanya ni autocratic.

Hiyo idara kwa kiwango ilichofikia (crime cartel) ni lazima Mh. Mwakyembe afanye kazi juu ya sheria na taratibu kidogo ili kuruka viunzi walivyojiwekea ili kuiweka katika hali inayotegemewa na taifa.

Soma kauli mbiu ya JF: WHERE WE DARE TO TALK OPENLY. Hiyo ndio ninayoitumia kusema hapa na pia kuwapa darasa wasiojua. Ungejua Mwakyembe hata Juzi nilikuwa naye tukinywa kahawa pamoja.

Kunya chai, kahawa au lunch na Mh. Mwakyembe halihusiani na mada hii zaidi ya kutaka kujikweza huku ukimpiga vijembe vya chini chini. Is that double standard?..
 
Una uhuru wa kusema lolote maana JF imetupa uhuru huo lakini nimeshasema na narudia tena, SIFANYI KAZI TPA, sina ndugu TPA wala rafiki. Bora TICTS nina washkaji huko nilikuwa nao wakati nikifanya research 2007.

By the way, mnachanganya sana kila kitu kuitupia lawama TPA. Hivi hamjui kuwa TICTS wanafanya pia kazi kama za TPA tena kwa kiwango kikubwa kuliko TPA? Hamjui kama TICTS wanapakua mizigo na kupakia?? Hamjui kama wizi pia waweza kutokea TICTS wakati wa kupakua? Hamjui kuwa mizigo inayopitia TICTS haikusiani hata chembe na TPA?

Mnahitaji kupewa elimu sana ili muelewe maana inawezekana mnafuata mkumbo tu bila kujua.

Watanzania hatuwezi kuacha ubinafsi. We have read between the line dude.

Kelele zingine kama za huju jamaa lazima tu ziwe na malipo.

Mkuu, ujumbe wako umefika, unarusiwa kuendelea kupata kinywaji kutoka kwa hao washikazi zako lakini wakumbushe wachukue mapema kwa sababu fagio liko njiani linakuja.

Ni ushauri tu.
 
Safi sana,sasa bandari italutea mapato yale yaliyotakiwa tuyapate tangu muda mrefu,ondoa wote kuanza upya sio ujinga.
Hongera sana

mawazo yako ni mazuri sana na nia yako ni nzuri mno. Lakini kwa upande wangu siamini kabisa kama huyo aliyeteuliwa atafikia malengo na matarajio yanayokusudiwa. Isije akaathiriwa na mfumo wa Wanamtandao na watafuna hela za nchi, nae akajikuta analegea kama wengine wale wale wa siku zote.
 
Tusiandikie mate wakati wino upo, tusubiri baada ya mwaka tuone mapato ya bandari kabla ya Mwakyembe na baada ya wizara kuchukuliwa na Mwakyembe.
So far i am learning towards Mwakyembe side kwa kutatua matatizo sugu matatu.

1. Usafiri wa ndege kwenda Mby toka nchi hii ipate Uhuru.
2. Usafiri wa Treni jijini Dar toka nchi hii ipate uhuru.
3. Kung'oa reli ya Kati na kuweka mpya sehemu korofi toka nchi ipate uhuru.

Hayo mambo 3 bado hayajakufungua tu kichwa chako?
 
Mh.mwakiembe iangalie na airpot, pale tukisafiri tunaambiwa kila mtu anakatwa dola 30 kwenye tiket, na naamini kwa siku wanaweza kusafir mpaka watu 2500. lakini ukipanga foleni ya kukaguliwa paspot kila mtu anakua na kihanjifu cha kufutia jasho hii ni albu airpot hata aircondition hamna hizi kodi zetu zinafanya nini!? Mbona nchi zawatu wanatueleza kodi zao zinavotumika.
 
Sidhani kama mwenyekiti ana influence kubwa sana kwenye shirika la umma. Maana hiyo nafasi ni ya kisiasa zaidi na sio kiutendaji; Labda kutakuwa na tofauti za sera kati ya Mwenyekiti na Waziri.

Na inauma wakati mwingine kwasababu Raisi inabidi achague upande kati ya watu wawili aliowachagua.
 
[QUOTE Prof. Msambichaka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mbeya.

KWENYE RED: Tafadhali msiniulize ndivyo mwandishi wa Rais alivyoandika katika taarifa yake. Lakini sijawahi kukisikia chuo hicho.
[/QUOTE]

Mbeya Institute of Sc & Tech. (MIST) has been changed to Mbeya University of Sc & Tech (MUST) =Chuo Kikuu cha Mbeya
 
Naomba niwape pole sababu hamjui historia yangu JF.

Mie naongea ukweli daima bila kujali kama mtapokea kwa namna gani. Mbaya zaidi mie sifanyi kazi TPA wala hakuna ndugu ama rafiki yangu YOYOTE aliyeko Bandari. Nafanyakazi katika eneo ambalo nina access ya information za ndani na nje ya serikali tena za usahihi asilimia 100%. Fuatilieni posts ama threads zangu mtajua.

Hamna sababu ya kukariri kuwa kila anayesema ukweli kuhusu Mwakyembe basi nduguye amefukuzwa ama yeye amekatiwa mirija ya kuiba. Lakini sio makosa yenu, watawala wetu tangu enzi ya Nyerere wametujengea akili ya kuwa rahisi kudanganywa na kukubali kudanganywa huku tukiwawaona wadanganyifu kama watu maarufu na kuwa-praise. Ndio sababu asilimia 80 kati yenu mlimpigia kura JK mwaka 2005 huku mkimuita ni chaguo la Mungu na Rais Kijana. Leo hamtaki hata kumsikia. Mlikubali kudanganywa kirahisi sana.

Nakubali Mwakyembe kuna mambo alikuwa akifanya vizuri sana, nanhuenda huko mbele atakuja kufanya mazuri. Lakini sasa amejikuta anaingizwa mkenge bila kujua na matokeo yake mtakuja kuyaona baadae.

Tunadanganywa na Treni ya Ubungo -Posta ambayo inaingiza hasara ya Sh 1.5 Million daily na Mwakyembe kakiri hivyo! Hatuoni kama uchumi wetu utakomaa zaidi kwa kuboresha reli ya mizigo ya Dar -Kigoma -Mwanza na kujenga reli ya Isaka-Burundi-Rwanda. Lakini amini msiamini Mwakyembe kaingia mkenge wa wamiliki wa magari ya mizigo (akina Riz1) kwa kujua ama kutokujua ili kuhakikisha reli ya mizigo haifanyi kazi ili biashara yao ikomae.

Anyway niishie hapa, lakini we have a long way to go kwa jinsi tunavyodanganywa kirahisi na watawala wetu!

Kwaiyo unataka kutuambia pale bandarini kulikua hakuna wizi wowote uliokua unafanyika wa kodi zetu na mali zetu? Kweli watz sisi ni wajinga sana lakini tufike pahali tukubali matokeo, tumechoka tumechoka tumechoka bora tufie huko mbele hatujui itakuaje, hii ni aibu kwako na kwa Watz wote, nchi hii imeoza kila mahali kila idara, tunahitaji watu kama mwakiembe wafikie angalau 10 je tuone hapatokua na mabadiliko? Sasa tunataka tupate na waziri wa mambo ya ndani as mwakiymbe. Tunawaogopa watu wanaotulinda, ukikutana nae bora ukutane na jambazi.
 
Mkuu,
Hiyo research yako kwa sasa ina miaka zaidi ya mitano toka ifanyike. Things have become even worse.
Hiyo sekta naomba tukubaliane, ilikuwa imejengeka kwenye msingi kama wa organised crime. Wanafanyakazi wanafahamiana, wanashirikiana na wanalindana katika kulihujumu taifa. Hilo haina ubishi.

Kawaida ya crime cartel, hairuhusu mtu wa nje kuingia kwenye ring yao na ndiyo hii inayotokea kw Mh. Mwekyembe kupigwa majungu na kuwa undermined ili kionekane kile anachokifanya ni autocratic.

Hiyo idara kwa kiwango ilichofikia (crime cartel) ni lazima Mh. Mwakyembe afanye kazi juu ya sheria na taratibu kidogo ili kuruka viunzi walivyojiwekea ili kuiweka katika hali inayotegemewa na taifa.

Kunya chai, kahawa au lunch na Mh. Mwakyembe halihusiani na mada hii zaidi ya kutaka kujikweza huku ukimpiga vijembe vya chini chini. Is that double standard?..

Thanx kaka ng'wamapalala.hawa watu ndo wapotoshaji wa ukweli ktk jamii. Kujifanya wako karibu sana na mamlaka ili tuamini wakisemacho.

Kwa fikra kama zao hatuisaidii nchi yetu kusonga mbele.
 
Wana JF,

Rais Kikwete amemtimua mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari TPA Raphael Mollel kuanzia tarehe 16 Januari na badala yake Amemteua Profesa Msambichaka kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo.

Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa TPA na kutengua uteuzi wa Bwana Raphael Mollel, ambaye alikua anashikilia wadhifa huo. Prof. Msambichaka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mbeya.

KWENYE RED: Tafadhali msiniulize ndivyo mwandishi wa Rais alivyoandika katika taarifa yake. Lakini sijawahi kukisikia chuo hicho.

Hicho chuo kipo. Tembelea hapa: Bofya link hii Mbeya Yetu: WANANCHI WA VIJIJI VITATU MKOANI MBEYA WAIDAI SERIKALI FIDIA KWA ZAIDI YA MIWAKA MMOJA
katikati kwenye picha ni mtajwa.
DSCN0013.JPG
 
Leo nilipokwenda kwenye kikao cha Mwakyembe pale Bandari nilisikia ZENGWE la kusikitisha kutoka kwa staff wa TPA kama ifuatavyo:Katika ile Kamati iliyoundwa na Mwakyembe kulikuwa na mtu anaitwa Richard Kasesera.Huyu alitokea kujuana na Phares Magesa(ambaye ni TPA Staff,aliyekuwa level ya Principal kwenye idara ya IT).Hawa wawili walijuana kwenye Kikapu.Wakati Kamati ikiwahoji wafanyakazi,huyu PM alipeleka fitna na majungu mengi mno kwa RK,bila kujiuliza RK akawapa wanakamati hayo majungu.Ikumbukwe pia,PM alishaombaga nafasi ya Manager huko nyuma ila hakuitwa hata kwenye interview.Kwa hasira,akamfuata na kumweleza Mwenyekiti wa Board (Mollel) kuwa ameonewa.Mwenyekiti akamweleza DG,ila DG akamwambia huyu ni kijana mwenye uchu wa madaraka tu.PM akabaki na Principal Web Development.Sasa baada ya kupata mwanya wa kuwachongea ya KWELI&UWONGO waliokuwa juu yake kwenye idara ya IT,aliitumia ipasavyo.Then alipokuja Madeni Kipande,kila Kamati ilichokuwa inashauri alikifanya.Na ndio hapa RK akamshauri Madeni amweke PM kukaimu Ukurugenzi wa IT.PM kukaimu ilipingwa na HR kwa sababu: i)Taratibu zinasema Senior wake ambaye ni level ya Manager ndiye alitakiwa kukaimu Ukurugenzi na si yeye PM wa level ya Principal.ii)PM hanaga muda na kazi coz ni member wa NEC-CCM,ni Makamu wa Rais wa Chama cha Kikapu nchini,ni Mwenyekiti wa Tanz. Professional Net(TPN) na bado anajipanga kugombea tena Ubunge wa Kigamboni.Madeni alilazimisha na hadi leo PM ni Kaimu Mkurugenzi wa IT.Sina kinyongo na yeye kupewa ila naona hapa kuna tatizo ndani ya idara na ushirikiano ndani ya shirika.Mwakyembe amka Baba!.
 
Back
Top Bottom