Rais Kikwete afanya mabadiliko Tume ya Uchaguzi (NEC) Pia ateua Majaji

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Rais Kikwete amemuondoa mkurugenzi wa uchaguzi katika Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Julius Malaba na badala yake amemteua Bw. Kairuna Ramadhani Kombwey kushika wadhifa huo mpya.

Bwana Kombwey anaapishwa leo jioni kushika wadhifa huo mpya. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa utawala katika NEC.

Sababu za uteuzi huu wa ghafla na kuapishwa haraka mteule huyu hakujaelezwa bayana. Hata hivyo Rais amemteua Malaba kuwa Jaji wa mahakama kuu kuanzia leo. Malaba kateuliwa na wenzake 12.

Nitawawekeeni majina yao soon.

IMG-20150725-WA0010.jpg
Bw. Kairuna Ramadhani Kombwey akiapa mbele ya Rais Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kumteua Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Vile vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumamosi, Julai 25, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa teuzi hizo zote zimeanza leo hii.

Kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Sefue, Ndugu Kombwey ambaye anaapishwa baadaye leo jioni,anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu Julius Benedicto Mallaba.

Badala yake, Rais Kikwete amemteua Bwana Mallaba kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kombwey alikuwa Mkurugenzi wa Utawala, Tume ya Uchaguzi.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa Jaji Mziray ambaye anateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.

Majaji wa Mahakama Kuu ambao wameteuliwa na Rais Kikwete, kwa mujibu wa taarifa hiyo ni,

1.Ndugu Ignas Pius Kitusi ambaye ni Msajili Mkuu,Mahakama ya Tanzania,
2.Ndugu Wilfred Peter Dyansobera ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu;
3.Ndugu Lameck Michael Mlacha ambaye ni Naibu Msajili na Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi;
4. Ndugu Salima Mussa Chikoyo ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi;
5. Ndugu Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania na
6. Ndugu Julius Benedicto Mallaba.
7. Ndugu Adam Juma Mambi ambaye ni Katibu Msaidizi, Tume ya Kurekebisha Sheria; 8. Ndugu Sirilius Betran Matupa ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Rais, Sheria, Ofisi ya Rais, Ikulu;
9. Ndugu Issa Maige ambaye ni wakili wa kujitegemea,
10. Ndugu Licia Gamunya Kairo ambaye ni wakili wa kujitegemea;
11. Dkt. Masoud Shaaban Benhaji wakili wa kujitegemea na Mhadhiri Mwadamizi,Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam,
12. Ndugu Victoria Makani ambaye ni wakili wa kujitegemea na
13. Ndugu Rehema Joseph Kerefu ambaye ni mwanasheria wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo imesema kuwa wakati Ndugu Kombwey anaapishwa leo, majaji wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

itakuwa mkutano wa vyama vya siasa na NEC,ulivunjika,pia inawezekana ni maandalizi ya goli la mkono,hawa majaji wanaandaliwa kwa ajili ya kumlinda nani?
 
Maandalizi ya goli la mkono hayo wameanza kwa kubadilisha refarii. Huyu Kikwete upo uwezekano wa kuzeekea Den Hague maana machafuko yatakayosababishwa na wizi wa kura kuhalalalisha bao la mkono atayasababisha yeye. Halafu haya majamaa ya UKAWA yako kama makondoo yanapelekwa kuchinjwa, miaka mitano hayajadai tume huru ya uchaguzi na sasa wanabadilishiwa refarii yatakaa kimya. Pia ikumbukwe kuwa ile sheria inayozuia kumshitaki mshindi wa uraisi iko pale pale wakipigwa bao la mkono watabaki kususia hotuba ya raisi na kutishia kuwa nchi haitatawalika. Hakuna upinzani Tanzania zaidi ya usakatonge tu
 
Hiyo yote ni homa ya Lowassa kwenda Ukawa.... Malaba alishawahi kukiri tena nikiwa namsikia kwa masikio yangu kuwa Ukawa wana dalili ya kushinda na NEC watakuwa fair katika kutangaza matokeo
Mkuu Lowasa ameshakatw anatoka wapi tena huku au umepagawa mkuu.
 
Maandalizi ya goli la mkono hayo wameanza kwa kubadilisha refarii. Huyu Kikwete upo uwezekano wa kuzeekea Den Hague maana machafuko yatakayosababishwa na wizi wa kura kuhalalalisha bao la mkono atayasababisha yeye. Halafu haya majamaa ya UKAWA yako kama makondoo yanapelekwa kuchinjwa, miaka mitano hayajadai tume huru ya uchaguzi na sasa wanabadilishiwa refarii yatakaa kimya. Pia ikumbukwe kuwa ile sheria inayozuia kumshitaki mshindi wa uraisi iko pale pale wakipigwa bao la mkono watabaki kususia hotuba ya raisi na kutishia kuwa nchi haitatawalika. Hakuna upinzani Tanzania zaidi ya usakatonge tu

Yamekua hayo!!!!
 
Acha upuuzi wewe. Mpinzani ni nani? Kama wewe hujaridhika na hali hiyo chukua hatua sio unalalama na kulaumu kana kwamba kuna mtu anatakiwa kukuletea mabadiliko. CHANGE START WITH YOU
 
Back
Top Bottom