Rais Kikwete abanwa Bunge la Katiba

Rais Kikwete abanwa Bunge la Katiba

Nimelisikia pia kigangoni kwangu leo, Matarawe, Songea. Nadhani viongozi wa kikristo wanataka kuwajuza wakristo wote kuhusu maoni na misimamo yao kuhusu mchakato wa katiba mpya. Na ndio maana wanasoma huo waraka makanisani.
 
Ni tamko lilisomwa nchi nzima. Hapa mwanza taktibani makanisa yote limesomwa na porokia niliyosali mimi limesomwa pia. Kama uamini tanzania daima nenda JUKWAA LA katiba kuna tamko zima bila editing yoyote

Mie nimesali Nyakahoja Hapa Mwanza.Nimekuta ndio waraka unasomwa kwa wale waliosali misa ya Pili.Tulipoingia misa ya tatu ambayo ni ya kiingereza halikusomwa kwani hakukua na nakala ya kiingereza,na padri mwenyewe ni mzungu anayefundisha pale SAUT, hivyo kilichofanyika ,alipewa summary ya sehemu muhimu katika waraka huo na akazifafanua kwa lugha iliyokuja kwa meli.

Kimsingi Waraka huo umesomwa nchi nzima na madhehebu yote ya kikristo na kwenye kila ibada.Hii inaenda kuleta mwamko mpya wa Watanzania kwenye suala hili la katiba.

Leo nimefurahi sana kwani Sitta na Unafiki wake ndio anaenda kufikia mwisho wa siasa zake, na CCM inakwenda chali.
 
Ukawa wamekwama nia yao kuyumbisha chama tawala kishindwe tekeleza majukumu yake. Bila shaka bmk halitayumba na litaendelea kuandaa katiba.
Kwani CCM mmekatazwa kuendelea kutengeneza katiba ya kulinda genge la mafisadi wa chama chenu?Ila mkae mkijua kwamba ajenda ya katiba ya wananchi itarudi tena Kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani,Kazi ya UKAWA itakuwa rahisi sana wakati wa kampeni,nayo ni kuinadi rasimu ya katiba ya tume ya Warioba,basi!
 
Kweli wakijifanya hawasikii cdm itafanya rasimu ya wananchi kama ndio msingi wa kampeni na kwa hili watapata support ya kutosha!wakristo tu wamoja kuliko wanavyodhani!
Naomba pia viongozi wa kiislam wakutane watoke na tamko
 
RC is ma place

Mkuu unakosea sana kusema RC. sisi ni Catholic na sio Roman Catholic(RC) kama wengine wanavyosema.
 
Kwani CCM mmekatazwa kuendelea kutengeneza katiba ya kulinda genge la mafisadi wa chama chenu?Ila mkae mkijua kwamba ajenda ya katiba ya wananchi itarudi tena Kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani,Kazi ya UKAWA itakuwa rahisi sana wakati wa kampeni,nayo ni kuinadi rasimu ya katiba ya tume ya Warioba,basi!

Sidhani kama CCM wanasikia au kuona kama wewe unavyoona! wacha tuwasubirie, ....Bungeni watashinda lakini uraiani kamwe hawatashinda na wasubiri maumivu tu
 
Ingawa CCM wamelala usingizi wa pono lakini sema taratibu basi ama sivyo utawabumburusha, hiyo ndio fimbo pekeee iliyojificha mgongoni mwa UKAWA
 
Hawa nao wanatuchanganya sasa!Kama wakati huu wa mkwamo ndo wameipitia Rasimu ya pili, na kujielimisha kwayo nakugundua kuwa ndiyo yenye kufaa, yale matamko ya yao ya kipindi cha nyuma ndio kusema walikurupuka!
Wakati wanawataka UKAWA kurudi bungeni wakati ule, hawakufahamu haya?
Je UKAWA wangerudi kwa kufuata ushauri wao, utamu, uzuri na umuhimu wa rasimu ya pili wangejielimisha saa ngapi?

Ni busara sana kabla hujakurupuka kutoa matamko na shutuma na hata kujifanya mpatanishi ukijielimisha vya kutosha ili usije kuonekana ndumila kuwili na mchumia tumbo!

You're absolute right Mkuu! Nikikumbuka vituko vya akina Muadhama Policarp Kadinali Pengo na Ngalalekumtwa wa kule Iringa kwa kweli sina hamu na hawa watu! Sometimes, wanafanya mambo yenye utata sana; leo wanaongea hivi, kesho anaibuka mwingine miongoni mwao anatoa kauli tata zaidi baadaye "wanarekebisha" kwamba ilikuwa "kauli yake binafsi" alimradi michanganyo kwa waumini.

Katika hili la Katiba Mpya ni kiongozi mmoja tu wa kiroho ameweza kuwa consistent na kauli zake - Baba Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Makanisa ya FGBF - huyu peke yake. Wengine ni michosho tu.
 
Kwani CCM mmekatazwa kuendelea kutengeneza katiba ya kulinda genge la mafisadi wa chama chenu?Ila mkae mkijua kwamba ajenda ya katiba ya wananchi itarudi tena Kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani,Kazi ya UKAWA itakuwa rahisi sana wakati wa kampeni,nayo ni kuinadi rasimu ya katiba ya tume ya Warioba,basi!
Mtakwama kama agenda yenu kuu itakua serikali tatu. cdm hua mnajidanganya wenyewe. Takwimu za warioba wala hazionyeshi serikali tatu kama ni agenda ya wananchi. Njooni na agenda zingine ila hiyo ya katiba kinyume na matarajio yenu itaipandisha chati ccm.
 
Sidhani kama CCM wanasikia au kuona kama wewe unavyoona! wacha tuwasubirie, ....Bungeni watashinda lakini uraiani kamwe hawatashinda na wasubiri maumivu tu

Zanzibar peke yake wanatosha kufutilia mbali upuuzi unaoendelea Dodoma. Sioni ni kwa vipi kitakachopitishwa Dodoma kitapata 2/3 kwa wale wahafidhina wa Zanzibar hasa baada ya kukosekana MARIDHIANO kati ya CCM na UKAWA ambao wana nguvu za kutosha Zanzibar. Sijui ni kwa nini viongozi wetu wanakuwa vipofu kiasi hiki hata kushindwa kuuona ukweli ulio dhahiri.
 
maCCM wataweweseka sana lakini katiba mpya itapatikana mwaka 2016 baada serikali ya UKAWA kutinga magogoni.
 
Hapa siyo suala la serikali tatu, mbili au moja bali cha muhimu ni matakwa ya wananchi. Ukikataa kuwa wananchi waliotaka serikali tatu walikuwa wengi wengi itabidi utoe ushahidi wa kuthibitisha kuwa waliotaka seriakali mbili walikuwa wengi.

Laiti ndani ya CCM kungekuwa na wenye akili, wangeweza kugomea serikali tatu lakini wangeamua suala la serikali 3, 2 au moja lipigiwe kura ya maoni au kuundwi kamati ndogo nyingine ya kukusanya maoni juu ya jambo hili la aina ya mwungano. Lakini kwa CCM kuamua kwa nguvu kubadilisha maoni ya wananchi na kuamua kuweka ya kwao, wajue kuwa wamejitengenezea kaburi wenyewe.

Azimio la Jukwaa la Wakristo litasomwa katika makanisa yote, na muda si mrefu mtasikia azimio la misikiti, majukwaa ya wanaharakati, n.k. Na huko ndiko waliko Watanzania.

Kwa ujinga wa ajabu CCM wanagomea hata Rais kupunguziwa madaraka, Rais kushtakiwa, n.k. Je, kweli hawa ni watu wenye nia njema na Watanzania. Utawala unapokufa dalili ya kwanza ni kuwa kiziwi, ya pili ni kuwa kipofu. CCM tayari ni viziwi, na wameanza kuwa vipofu ili kuhitimisha kanuni ya utawala unaokufa.

Mtakwama kama agenda yenu kuu itakua serikali tatu. cdm hua mnajidanganya wenyewe. Takwimu za warioba wala hazionyeshi serikali tatu kama ni agenda ya wananchi. Njooni na agenda zingine ila hiyo ya katiba kinyume na matarajio yenu itaipandisha chati ccm.
 
Ninyi ndiyo inaonekana wala hamkusoma wala kuelewa tamko la maaskofu la mwanzo. Nina uhakika kuwa msimamo wa viongozi hawa haujawahi kubadilika. Tofauti niinayo ni kuwa tamko la sasa ni wazi zaidi na limetumia lugha kali zaidi.

Tamko la awali lilisema kuwa, 'wanawashauri UKAWA warudi bungeni' lakini maoni ya wananchi yaheshimiwe. Kwenye maneno haya ni dhahiri kuwa walichokuwa wakishauri ni UKAWA kurudi Bungeni kujadili maoni ya wananchi. Maana yake ni kwamba umuhimu wa kurudi Bungeni ni pale maoni ya wananchi yatakapojadiliwa na kuheshimiwa. UKAWA hawakurudi Bungeni kwa sababu maoni ya wananchi yamepuuzwa.

Tamko lile la mwanzo lilikuwa linahusu pande mbili, kwa CCM na UKAWA. Kwa CCM ujumbe ulikuwa dhahiri, waheshimu maoni ya wananchi. Kwa uKAWA warudi Bungeni kukiwa na uthibitisho wa kujadili maoni ya wananchi.

Polycarp Pengo alisema wazi kuwa yeye anapendelea serikali mbili, kwenye ufafanuzi alisema kuwa hayo ni maoni yake binafsi na wala hayawakilishi wakristo wa Jimbo kuu la Dar es Salaam. TEC ambalo ndiyo Baraza la Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki Tanzania, msimamo wake ambao ulielezwa na Mwenyekiti wa Baraza kwa niaba ya Maaskofu wote Tanzania ni serikali tatu kwa vile ndivyo wananchi wanavyotaka.

Wengi wasichokijua ni kuwa Pengo ni askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, na ana nafasi sawa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Mwanza, Kilimanjaro, n.k. Nafasi yake ya Ukadinali haimaanishi ni mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Ukadili ni nafasi ya ujumbe wa Vatikani ambao haumwongezei mamlaka yoyote kwa hapa nchini.

You're absolute right Mkuu! Nikikumbuka vituko vya akina Muadhama Policarp Kadinali Pengo na Ngalalekumtwa wa kule Iringa kwa kweli sina hamu na hawa watu! Sometimes, wanafanya mambo yenye utata sana; leo wanaongea hivi, kesho anaibuka mwingine miongoni mwao anatoa kauli tata zaidi baadaye "wanarekebisha" kwamba ilikuwa "kauli yake binafsi" alimradi michanganyo kwa waumini.

Katika hili la Katiba Mpya ni kiongozi mmoja tu wa kiroho ameweza kuwa consistent na kauli zake - Baba Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Makanisa ya FGBF - huyu peke yake. Wengine ni michosho tu.
 
RC is ma place

Mkuu unakosea sana kusema RC. sisi ni Catholic na sio Roman Catholic(RC) kama wengine wanavyosema.

kweli mkuu: wananiboa ni wale wanaosema mimi ni ROMA
 
Mimi ni mmojawapo waliohoji sana ukimya wa viongozi wa dini na chama cha wanasheria nchini kuhusu ukimya wao kwenye suala hili la katiba. Ni muda mrefu watawala wamejificha kwenye kichaka cha udini kwa support ya viongozi wa dini ils sasa naona wamegundua kosa lao wameamua kusimamia ukweli.
 
Hao ccm si ndio walitengeneza sheria mbovu ya kumuweka rais juu ya mchakato wa katiba mpya wakati wapinzani waligoma kabisa rais kuwa juu ya mchakato. Viongozi wa dini hili mlikaa kimya kwani mlikuwa mkitishwa na watawala na sasa kinachotekea ni matokeo ya sheria mbovu iliyoundwa na wabunge wengi wa ccm. Wote tunajua wabunge wengi wa ccm walishinda kwa rushwa, kutegemea dola nk. leo watakuwaje ndio watengeneza sheria mama ya nchi?
 
Back
Top Bottom