Hapa siyo suala la serikali tatu, mbili au moja bali cha muhimu ni matakwa ya wananchi. Ukikataa kuwa wananchi waliotaka serikali tatu walikuwa wengi wengi itabidi utoe ushahidi wa kuthibitisha kuwa waliotaka seriakali mbili walikuwa wengi.
Laiti ndani ya CCM kungekuwa na wenye akili, wangeweza kugomea serikali tatu lakini wangeamua suala la serikali 3, 2 au moja lipigiwe kura ya maoni au kuundwi kamati ndogo nyingine ya kukusanya maoni juu ya jambo hili la aina ya mwungano. Lakini kwa CCM kuamua kwa nguvu kubadilisha maoni ya wananchi na kuamua kuweka ya kwao, wajue kuwa wamejitengenezea kaburi wenyewe.
Azimio la Jukwaa la Wakristo litasomwa katika makanisa yote, na muda si mrefu mtasikia azimio la misikiti, majukwaa ya wanaharakati, n.k. Na huko ndiko waliko Watanzania.
Kwa ujinga wa ajabu CCM wanagomea hata Rais kupunguziwa madaraka, Rais kushtakiwa, n.k. Je, kweli hawa ni watu wenye nia njema na Watanzania. Utawala unapokufa dalili ya kwanza ni kuwa kiziwi, ya pili ni kuwa kipofu. CCM tayari ni viziwi, na wameanza kuwa vipofu ili kuhitimisha kanuni ya utawala unaokufa.