Rais Kikwete aagiza flyovers zijengwe Dar haraka sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete aagiza flyovers zijengwe Dar haraka sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Feb 6, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 42,478
  Likes Received: 26,041
  Trophy Points: 280
  Date::6/2/2010
  Mwandishi Maalumu
  RAIS Jakaya Kikwete, ameagiza hatua za haraka zichukuliwe, kujenga barabara zinazopita juu katika Jiji la Dar es Salaam, ili kupunguza misongamano mikubwa ya magari.

  Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM alitoa agizo hilo juzi, baada ya kupewa taarifa ya utendaji ya CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam.

  Mwenyekiti huyo alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu ya kukagua shughuli za CCM mkoani humo.

  "Hili la flyovers lipewa kipaumbele ili tupunguze msongamano wa magari katika Dar es salaam. Tusipofanya hili jiji hili litakuwa halipitiki katika muda wa miaka mitano, ama hata katika miaka miwili ama mitatu ijayo," Rais Kikwete.

  Rais Kikwetepia aliwaagiza wataalam wa mipango miji katika Jiji la Dar es Salaam, kuanza kupunguza maeneo yasiyopimwa kwa kuzingatia kuwa kwa sasa ni asilimia 30 ya jiji ndiyo iliyopimwa.

  Alisema Jiji la Dar es Salaam, haliwezi kuendelea kupanuka bila mpangilio na kwamba wakati sasa umefika wa kuhakikisha kuwa linajengwa kwa kuzingatia mipango miji.

  "Hatuwezi kuendelea namna hii na mji unaopanuka namna hii. Hili ni jambo zito, kubwa linalohitaji umakini wa haraka kutatuliwa. Ndio maana kipindupindu hakiishi katika mji huu." alisema Rais Kikwete baada ya kupata taarifa kutoka kwa watalaam wa huduma za maji, ardhi na barabara.

  Katika mkutano huo, Rais Kikwete pia alipewa taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ukosefu wa maji ya katika jiji hilo.

  Rais Kikwete pia aliusifu utendaji wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam akiwataka viongozi wa chama hicho kutafuta njia za haraka za kutatua matatizo ya wananchi.

  "Angalieni na chunguzeni sana matatizo ya wananchi. Haya ndiyo muhimu kwetu kuyashughulikia, tena kwa haraka. Hii ndiyo nguvu ya chama chetu," amesema Mwenyekiti huyo wa CCM

  Source: MWANANCHI

  My take:
  swala la mpangilio wa mji wa DAR linatia hadi hasira, sijui walikuwa wapi mda wote huo. Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa?

  Unaweza kukuta wengine hata wamepanga manzese,na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? Isije ikawa kama ile ya maisha bora.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,541
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mzee anafikiriaga kweli maagizo anayoyatoa au anapauka tu?madawati kununua yanawashinda anawaza flyovers?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,232
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hivi ni baada ya miaka mitatu ndo zitakuwa hazipitiki, au ni tangu miaka zaidi ya mitatu ya nyuma?

  Au kwa vile yeye anapita kwenye njia iliyosafishwa kila atokapo!
  Wataahidi sana hawa safari hii, yetu macho.
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Uchaguzi unakuja....miaka minne yote alikua wapi kuzijenga hizo barabara za juu...wanatafuta ahadi mpya.
  wakati wauchaguzi mkuu mwaka 2005 walikua na ahadi kuwa kufikia 2009 kutakua na usafiri wa mabasi yaendayo kasi DSM, SASA WAMESHINDWA WANAKUJA NA KELELE MPYA, tunataka vitendo, Kikwete tumechoka na maneno maneno yako.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,541
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  yaani JK kwa sasa namfananisha na goalkeeper ambaye beki zake hazikabi sasa anahangaika tu mipira inavogonga besela....hahaaaaaa
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 42,478
  Likes Received: 26,041
  Trophy Points: 280
  kweli wazee mabasi yaendayo kasi yameyeyuka .ahadi gani inachukua karne?,then anajaribu kutoka na single nyingine tena sa ivi.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 145
  Wameshindwa kujenga shule za matofauli watoto wanasomea shule zilizo ezekwa kwa nyasi sasa wanaota flyovers bado tunasafari ndefu na hiki chama za zidume fikra za mwenyekiti wa chama.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  napata sana shida kumuelewa Kikwete, naonaga uvivu kumsikiliza, na waliomsikiliza makiniambia aliyoyasema nafadhaika sana......anaanza kuleta ngonjera hizo, yeye ni mtendaji mkuu awaachie wanataarabu kina Tabwe hiza watuburudishe na nyimbo za kipropaganda....yeye awe mtendaji....Kikwete na watu wako ya wapi mabasi yaendayo kasi Dar es salaam kabla hamjakuja na mradi hewa mwingine.
   
 9. O

  Omumura JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mmmh, mwaka huu tutasikia mengi na mengine yasiyo na kichwa wala miguu, mwenyekiti wa taifa yake wanachama nao hoi kwa umaskini unawaambia habari ya flyovers, makamba nae ni zaidi ya hoi!!!Hizo flyovers wamwambie chenge na Lowassa ambao ni wajumbe wa kamati kuu wazijenge wenyewe kwa vijisenti vyao!
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 42,478
  Likes Received: 26,041
  Trophy Points: 280
  kwanza baadhi ya barabara ambazo huo mradi ungetakiwa upite zishaanza kuharibika aka kilwa road.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  sasa nilikoma kulinga nilipoambiwa wanataka eti kupanua barabara za posta mpya na mnazi mmoja ili kuruhusu magari hayo kupita...nilihisi ni ulongo usio kifani, sasa kama unavyosema, tukajengewa KILWA RD. kwakiwango cha chini kuliko , waziri wa miundo mbinu sijui Kawambwa sijui nani ni kama hayupo, aaah Kikwete bana, unaniboaga basi tu.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 42,478
  Likes Received: 26,041
  Trophy Points: 280
  OK. WAKUU TUSHAANZA KUSIKIA NGONJERA,NA TUKIENDELEA KUBLAME HUMU HAKUNA FAIDA YOYOTE.SASA INABIDI TUJE NA SOLUTION: JF NI KUBWA NA PANA HATA IKULU WATAKUWA WANAISOMA HIO NI KWELI KABISA.SASA BASI WE COME WITH SOLUTION INSTEAD OF BLAMMING.piriodi.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 42,478
  Likes Received: 26,041
  Trophy Points: 280
  kote huko ni watu wanataka kula tu. Utakuta hata kwenye kugawa ile tenda kulikuwa na utata.
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  utata utakosekana vipi, kama wajanja walitaka kukomba hadi mradi wa vitambulisho vya Taifa....nnchi bana, uongo mwingi, wizi mwingi, umbea umbea mwingi...na Mtawala nae anaingia kwenye mkumbo huo, mimi kwakweli simfagilii.....
   
 15. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,500
  Likes Received: 7,802
  Trophy Points: 280
  Kamuagiza nani!?

  Hivi anaelewa hata 'feasibility study' ya hii kazi inachukua muda gani?

  Majuzi hapa wamesema wapo njiani kuleta train ziendazo kasi ya ajabu (kupitia kwenye reli ile ile ya mjerumani!!?)

  Hivi uchaguzi mkuu ni mwezi wa ngapi vile!!?

  Nadhani imefika muda sasa tusiwe na president mwanasiasa
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,732
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kwani flyover ndiyo jawabu pekee la matatizo ya usafiri?

  Amandla.....
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 36,095
  Likes Received: 7,673
  Trophy Points: 280
  Hivi April 1 ishafika tayari? Are you guys on some type of Klingon calendar?

  Huyu Kikwete anasema hivyo kwa ushauri wa wataalam au yeye kashakuwa Engineer in Chief siku hizi?
   
 18. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,816
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 180
  hamna kitu kaka...mbio za oktoba 2010 zimeshaanza..
   
 19. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,755
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi mwenyewe nimestuka sana nilivosikia hivo lakini sikushangaa kwani huyu kiongozi wetu ni mtu wa kutamka mambo sana bila kuyafikiria. Manake vitu vingine hauhitaji kuambiwa kuwa ni bla blaa, juzi juzi tu wamezungumzia train ziendazo kasi leo hii fly-overs tena mh? Hiri rinchi sasa!!
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 42,478
  Likes Received: 26,041
  Trophy Points: 280
  Nani atakubali kumpika? uchaguzi ndio huo na mkulu hadi sasa anaongoza tatu bila winga na mfungaji akiwa mnajimu wetu. makamba beki la kupanda na kushuka.mrema D:D:D:???
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...