Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Huko Tz, kuna kitu ka hicho wakenya wamepata? Na bado utakuta wabongo wengine wakilalamika!
 
Shida watu hamjui historia ya Kenya na Tanzania. Kutokuelewana wakenya na watanzania hasa kiserikali hakujaanza leo. Wakati wa Nyerere kulikuwa na hiyo vita ya maneno. Hadi kuitana majina. Nyang'au n.k.
Kenya siku zote wanaitamani ardhi ya Tanzania. Na uchumi wa Kenya adilimia 8 huko mikononi mwa matajiri wwachache hasa wazungu.
Hivyo Kenya wanataka kutumia hyo oen market ili waweze kufaidi maliasili za Tanzania. Na product zao wataandika made in Kenya, wakati viwanda vitakuwa Tanzania.
Nimeishi Kenya toka utoto. Ni watu wsnao jivunia nchi yao. Si kama sisi watanzania. Kenya awawasemi na kuwatukana ovyo viongozi wao. Watatofautiana lkn bado wataipenda nchi yao na kuisifia. Ni tofauti na watanzania. Wanao jidharau na kusifia nchi nyingine.
Subirini wskenya waje. Muanze kulalamika tena.
Bora tutalalamike lakini tutajifunza kitu mkuu
 
ni kweli mkuu..
lengo lake ni tanzania iseme the same, ili pia waje wafanye biashr upande wa pili bila permit..

na sisi tukifuata hilo, wakenya watakuwa wame win
Hapo umemaanisha nini? So nyie wa Tz kutolewa vikwazo hivyo na rais Uhuru, nikufeli mmefeli au wasemaje?
 
Huu uwoga na tumeaminishwa na wana siasa kuwaogopa wa Kenya na unyonge ndio shida kubwa, tunawaogopa nini hasa mbona tumejaza wahindi makampuni yote na kila siku wanaingia tu. Ajira ni ushindani na ufanisi ndio inabidi tujiongeze tuwe waadilifu ili sisi ndio tuwe na thamani kwao siku waombe wa Tanzania katika makampuni yao. Tabia ya kuaminishwa kuwaogopa wa Kenya hata sijui nani aliyeileta, Mimi simuogopi mkenya kwa lipi zaidi? tuache unyonge
Na ujinga.yaani tuna ujinga mwingi hadi inasikitisha.
 
Hata wakiruhusiwa kuja kufanya biashara kwetu huoni kuwa ni faida kwetu tutajifunza mengi? huoni wanaweza kuja kuzalisha ajira pia na kuongeza pato la kodi?
mtego ninaouona mimi kwa mazingira yetu ya kodi kandamizi na taasisi zisizo kichwa wala miguu ni kuwa watanzania wanaweza wakaona bora wakafanye biashara Kenya,
Na hii kitu ya kodi inafaa kuzungumziwa. Wafanya biashara wa Sector mbalimbali KE wamelalamika ju ya kutozwa kodi ya juu sana wakileta bidhaa Tz au wakitaka kuanzisha biashara flani huko, wakati huku KE hakuna udhalilishaji ka huo kwa wafanyabiashara wa Tz.
 
Shida yetu iko hapo..tunamuogopa kila mtu..hv why lakini?sijui niNyerere au nani alitujaza ujinga wa kuogopa ogopa kila kitu! Tujaribu tukiona wanatuzid akili mamlaka zipo!khaa
Sisi ni makondoo.hatuko aggressive kwenye mambo ya msingi.Tunataka tu kupiga porojo za mdomoni,majungu na umbea.
 
Hivi kenya kuna ajira gani kwa watanzania,hili chaka la working permit tusijaribu kuliingia kwenye biashara hapo sawa,kwenye ajira watuache kwanza kidogo
Kama huna sifa unataka uajiriwe vip.Dunia ya sasa ni mapambano na kama huwezi kupambana kaa tulia wenye uwezo watapambana.Hakuna nchi ambayo haina fursa mambo mengine yatategemea uwezo wako wa akili na kutenda.
 
sema hawa jamaa sjawahi kua na imani nao, uwekezaji ni muhimu sawa ila sheria ziwekwe nzuri haya mambo ya kubrand mlima kilimanjaro kenya iwe mwisho
Huo mlima Kilimanjaro haujabrandiwa kuwa wa Tz, hata kwenye issue za guide books wanaonesha kabisa mlima uko Tz ila ukiwa Amboseli Game Park unaweza pata view yake pia. Ukiwa msafiri nafkiri utaelewa nacho zungumzia hapa!
Na hapo kumbuka faida kwenyu pia, watalii wakitaka kuuona full, si tunawaleta Tz au wao wenyewe wanaweza kuja next trip huko?
 
Wakenya wajanja, hata kama huna work permit, wala business visa, kazi hupati Kenya.. Mtanzania hawezi pewa nafasi na wakenya kufanya kazi.. Sisi tusiruhusu hilo, eti wakenya waje free huku, hilo litakuwa kosa kubwa sana kutokea
Kasome kwanza upate shahada, na uwe na washkaji huku, alafu njoo KE. Hakuna mteremko kwenye maisha ya hustling, labda uwe mtoto wa Sheikh Khalifa! 🤣
 
Sisi ni makondoo.hatuko aggressive kwenye mambo ya msingi.Tunataka tu kupiga porojo za mdomoni,majungu na umbea.
Hivi kwanini tuko hivyo sasa? Kuna mdada nilikutana naye 3yrs ago anatoka kenya anakusanya🌻🌻🌻🌻🌻 mikoa yenye alizeti ana kampuni so anaprocess mafuta ya alizeti sana anaenda uza huko!
Yule bidada hana maongezi kama ya kitz...yaan hata ukimpgia simu inabidi umchallenge vitu vya msingi..sasa sisi si wanawake si wanaume tunapenda petty issues balaa..hivi ni LAANA au kuna kiongoz huko nyuma alishaharibu kuturithisha?
Haiwezekani ukamuogopa binadamu mwenzako eti kisa anaakili kukuzidi wewe...kwanini usiombe huo weledi ukawa nao wewe! Mie bongo jamani sina hata la kusema! Nasema sina
 
Mtego huo. By so saying, he envisages 'reciprocity'

In terms of capacity (qualification) watz wengi hawana uwezo wa kuexcel kwenye white-collar jobs in Kenya.

Pia, wakenya wana roho mbaya, na ni watu ambao ni very aggressive when it comes to opportunities. Mkenya hana ile sense of 'undugu & ujamaa'. So mtz ndezi ndezi hawezi survive kwenye business atmosphere ya nchini Kenya.

Labor force ya Kenya ni very skilled! Wakenya wakimwagika hapa nchini, watz tumekwisha!

Rais Samia asiingie kwenye huo mtego wa kitoto.

-Kaveli-
Unataka tuendelee kua makondoo mpaka lini.Unaposhindwa kua na uwezo wakupambana maana yake wewe ni dhaifu sasa namna yakuondoa huo udhaifu sio kujifungia ndani bali kutoka nakujifunza kwa yule aliyekuzidi.Tukumbuke miaka inaenda tusiporekebisha mapungufu yetu sasa iko miaka kitakuja kizazi kitakachokua hakiwezi chochote wakati huo wenzetu watakua wameshafika mbali kwenye kila nyanja.Na athari za huu ukondoo zinagusa jamii nzima kuanzia uchumi,elimu,burudani na mengine yakijamii.Kwahiyo tutafute ufumbuzi wa matatizo yetu badala ya kujificha.
 
Mkuu unachekelea na yeye mama atafanya the some....uone ajira zote zitachukuliwa na wakenya Hadi uwalimu.....kwasababu wako smart na agressive....time will tell utakujaa kulala Mika hapa tenaa
Kinachotushinda sisi kua kama wao au zaidi yao ni nini,au sisi ni matahira?,au vilema,hebu tujiulize maswali ya msingi ili tutafute ufumbuzi wakudumu.tuache kulia lia.
 
Mtego huo. By so saying, he envisages 'reciprocity'

In terms of capacity (qualification) watz wengi hawana uwezo wa kuexcel kwenye white-collar jobs in Kenya.

Pia, wakenya wana roho mbaya, na ni watu ambao ni very aggressive when it comes to opportunities. Mkenya hana ile sense of 'undugu & ujamaa'. So mtz ndezi ndezi hawezi survive kwenye business atmosphere ya nchini Kenya.

Labor force ya Kenya ni very skilled! Wakenya wakimwagika hapa nchini, watz tumekwisha!

Rais Samia asiingie kwenye huo mtego wa kitoto.

-Kaveli-
Oya una undugu na hii id ya makaveli10
 
tuanze kuwaandaa watu wetu kuwa washindani kwanza ndio tuingie kwenye contract za namna hii otherwise tutakuwa tumejipiga kitanzi...

tukitegemea wao waje ndio watu wetu wacatch up, tumeliwa jamaa yangu, kifupi watu wetu watakuwa utumwani kwa miaka mingi na kujinasua itakuwa ni machafuko labda...the more you advance the more they will advance..
Muda wakufanya hayo ulishapita.tuko nyuma ya muda kwahiyo ni vyema tukaamsha vichwa tukiwa ndani ya mpambano.Kama tu kwa huu utulivu tulionao tumeshindwa kuboresha elimu yetu iwe na viwango vyakueleweka unadhani itatuchukua karne ngapi kubadilisha jamii nzima mentallity ya kinyonge tuliyonayo.
 
tutaenzi kufundisha watu wetu kufanya kazi kwa bidii, tuanze kufundisha skills kwa watu wetu, tuanze kuwapa watu wetu elimu bora halafu ndio tuingie kwenye mashindano ya namna hii otherwise watu wetu watakauwa wanafanya kazi za chini sana....
Haya mawazo ilitakiwa yafanyike miaka ya uhuru sio sasa.Ata uko kwenye soka si unaona baada yakugundua viwango vya wachezaji wetu viko chini na ili wapate exposure dawa ni kuwachanganya na wachezaji kadhaa wa kigeni.Kwa kufanya hivyo naamini yako mabadiliko mengi kwa wachezaji wetu hasa kwa wale wenye nia ya kujifunza.Tukiendelea hivyo tutatengeneza wachezaji wengi wenye moyo wakujituma na kua serious na kazi kuliko tungesema wafundishwe kwanza nadharia yakujiamini na kujituma alafu badae ndo waingie kwenye ushindani.
 
wao tayari wana backup ya serikali yao..
yaani wafanya biashra wakikenya, serikali ipo nyuma yao kuwasapot kwa kila jambo tofauti na sisi, serikali hututelekeza kama yatima..

ukiwa tanzania, km chache kabla hujafika mpakani mwa tanzania na kenya, tayr unapokea text upo kenya, wakt vice versa haipo hivyo.

tuna bank gani kwao? wao wanazo huku kwetu wakishindana na hizi zetu. Uhur au mzalendo lipo kenya kama citizen la kwao huku?

sikatai ushindani kwamba waje, ila na sisi intellijensi yetu ijipange kuwasapot wafanya biashar watanzania kwanza, kabla ya kufungua hizo permit
Hapo matatizo ni yetu sio wao.Tatizo letu tumeridhika sana na maisha ndo maana tunajua vizuri matatizo yetu lakini hatutaki kuyapatia ufumbuzi zaidi yakupiga tu porojo za maneno.
 
Haya mawazo ilitakiwa yafanyike miaka ya uhuru sio sasa.Ata uko kwenye soka si unaona baada yakugundua viwango vya wachezaji wetu viko chini na ili wapate exposure dawa ni kuwachanganya na wachezaji kadhaa wa kigeni.Kwa kufanya hivyo naamini yako mabadiliko mengi kwa wachezaji wetu hasa kwa wale wenye nia ya kujifunza.Tukiendelea hivyo tutatengeneza wachezaji wengi wenye moyo wakujituma na kua serious na kazi kuliko tungesema wafundishwe kwanza nadharia yakujiamini na kujituma alafu badae ndo waingie kwenye ushindani.
Naungana nawe kwa kila kitu kwwnye uzi huu...tuache hofu zisizo na maana jamani
 
Wakati wa mgomo wa madoctor wa Kenya waliomba madoctor wa huku ilikuaje waliambiwa Kama hawajitaki waende Nini kilifuatiaa?
 
Back
Top Bottom