Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 11,626
- 22,004
Watanzania wenyewe hizo fursa azitutoshi,wabaki huko kwao,bado hatujafikia uchumi wa kugawana fursa 50-50 na mataifa mengineTanzania bado fursa zipo nyingi mno waje tu
Watanzania wenyewe hizo fursa azitutoshi,wabaki huko kwao,bado hatujafikia uchumi wa kugawana fursa 50-50 na mataifa mengineTanzania bado fursa zipo nyingi mno waje tu
Mama mjanja,hajaongelea kabisa mambo ya ajira,amesisitiza kwenye biashara tu 😀Hamna ubaya ila wakenya wakijazana tigo, voda na airtel wakaja TPB, NMB na CRDB wadogo zenu wote watakuwa wauza kashata na kutembeza kahawa! Msije kuanza kulia lia tu wakenya wamezidi
Ndio mjiandae kisaikolojia. Kuna maduka ukiingia yani wanakudharau Sana, ukiuliza TV samsung inchi 42 sh. Ngapi ? Utasikia aaah! Hiyo bei maelewano kwani wewe una sh. Ngapi? Kumbe anakudharau anajua huna hela. Hata kwenye ofisi za Umma wabongo dharau Sana. Ngoja tulare changamotoni kweli mkuu..
lengo lake ni tanzania iseme the same, ili pia waje wafanye biashr upande wa pili bila permit..
na sisi tukifuata hilo, wakenya watakuwa wame win
Unafanyanini Westland? Unafyeka nyasi au houseboy?Nipo west land
HaikuhusuUnafanyanini Westland? Unafyeka nyasi au houseboy?
Amaaaaa baaaaaa aaaaaae subutuuuuu Kina Museveni je?bado sanaPiga kelele kwa Kenyatta akee😁😁😁😁😁😁
Seriously, EA hatutakiwi kuwa na barrier zozote za kibiashara. Tuna custom union ya maneno tu lakini haifanyi kazi. Tunazuia na kubania biashara za Kenya huku tukijaza masoko kwa bidhaa za India na China. EA inatakiwa kufunguka, iwe kama nchi moja. Hapo ndiyo tunaweza fikia shirikisho la kisiasa
Zipo kibao hebu ona kukanga chips kuku tu ni fursa ambayo wala watanzania hatujaweza kuijaza ndio maana wakaletwa STEERS kama wawekezaji waje kukaanga chips kukuWatanzania wenyewe hizo fursa azitutoshi,wabaki huko kwao,bado hatujafikia uchumi wa kugawana fursa 50-50 na mataifa mengine
Uwekezaji huenda na ajira sasa Mwekezaji akija atasimama na pesa zake barabarani? Akifungua biashara atatoa ajiraNafikri wafanya biashara na wakulima wa Tz watanfuaika huko KE, na wa KE watanufaika kwa uwekezaji na kuuza bidhaa zao TZ .. lakini kuhusu ajira sijajua maana ajira bongo ni finyu kidogo .. na malipo ya mshahara yatawanufaisha kuliko huko KE
Uko sahihi mikoa mingine kama Dar es salaam nk wahindi na waarabu ndio wameijenga.Hiyo mikoa imejenga kupitia pesa za kenya na wafanyabiashara wakenya na hadi sasa uchumi wake mkubwa ni uchumi kenya.Wakenya wamewekeza sana mikoa hiyo na watu wa mikoa hiyo wanafanya biashara sana na KenyaNzuri hio Mr Kenyatta.Arusha, Tanga, Kilimanjaro,Mwanza imejengwa na pesa toka kenya.
Shida watu hamjui historia ya Kenya na Tanzania. Kutokuelewana wakenya na watanzania hasa kiserikali hakujaanza leo. Wakati wa Nyerere kulikuwa na hiyo vita ya maneno. Hadi kuitana majina. Nyang'au n.k.Bora Uhuru ni binadamu sn na kiongozi bora kabisa kuwahi kutokea Africa, shida walishindwa na Dikteta, mama kaona atakuwa Mwalimu mzuri sn
Hao waarabu na wahindi wengi ni wazawa wa toka Tanganyika. Angalia wafanya biashara wakubwa wengi ni Watanzania. Dar haijajengwa na wakenya. Acha kusifia vitu visivyo. Dar imejengwa na serikali hasa. Angalia majengo makubwa, miundo mbinu. Utakuta ni serikali na taasisi zake. Uwekezaji mwingine ni watu binafsi watanzania. Wakenya uvuna na kupeleka kwao.Uko sahihi mikoa mingine kama Dar es salaam nk wahindi na waarabu ndio wameijenga.Hiyo mikoa imejenga kupitia pesa za kenya na wafanyabiashara wakenya na hadi sasa uchumi wake mkubwa ni uchumi kenya.Wakenya wamewekeza sana mikoa hiyo na watu wa mikoa hiyo wanafanya biashara sana na Kenya
Pia kuna ubia mwingi wa biashara nyingi kati ya watanzania na wakenya.ZIngine hadi zimeandikwa majina ya watanzania lakini wamiliki ni wakenya.Wakenya ukiaminiana nao wako Tayari kukuachia pesa na Biashara uendeshe kwa niaba yao
Mimi ni mmojawapo nilishawahi kuwa Kenya nikapata fursa ya kupeleka ngozi za Ng`ombe mbichi Kenya.Sikuwa na mtaji akaniambia hakuna shida atatoa nimpe tu akaunti namba .Nikamwambia subiri kwanza nikafanye utafiti wa zinakopatikana na kiasi alikuwa akitaka nyingi.Nikazunguka kwenye machinjio ya ngombe nikakuta kuna wajanja watanzania walishawahi hiyo fursa siku nyingi wanapeleka Kenya.Nikamwambia nimeshindwa mimi .Hakuamini akadhani ni uvivu wangu tu akasema mbona wengi wanatoa huko wanasema zipo kibao? Akaja mwenyewe tukazunguka naye akakubali kuwa ni kweli
Wakenya kwenye business wako vizuri na hupenda sana ubia pia.Biashara kwao ni kama family business wanahitaji wakuamini kwanza kabla ya kuku take into their family .Watanzania wengine subira hawana wanataka from day one awe CEO wa kampuni ya MKenya!!! OOH ni haki yangu hapa ni nchini kwangu!!! Haiendi hivyo
Ila ni wajanja Sana kuwa makini Sana wao kukupiga au kukuzulumu ni dakika sifuri.Uko sahihi mikoa mingine kama Dar es salaam nk wahindi na waarabu ndio wameijenga.Hiyo mikoa imejenga kupitia pesa za kenya na wafanyabiashara wakenya na hadi sasa uchumi wake mkubwa ni uchumi kenya.Wakenya wamewekeza sana mikoa hiyo na watu wa mikoa hiyo wanafanya biashara sana na Kenya
Pia kuna ubia mwingi wa biashara nyingi kati ya watanzania na wakenya.ZIngine hadi zimeandikwa majina ya watanzania lakini wamiliki ni wakenya.Wakenya ukiaminiana nao wako Tayari kukuachia pesa na Biashara uendeshe kwa niaba yao
Mimi ni mmojawapo nilishawahi kuwa Kenya nikapata fursa ya kupeleka ngozi za Ng`ombe mbichi Kenya.Sikuwa na mtaji akaniambia hakuna shida atatoa nimpe tu akaunti namba .Nikamwambia subiri kwanza nikafanye utafiti wa zinakopatikana na kiasi alikuwa akitaka nyingi.Nikazunguka kwenye machinjio ya ngombe nikakuta kuna wajanja watanzania walishawahi hiyo fursa siku nyingi wanapeleka Kenya.Nikamwambia nimeshindwa mimi .Hakuamini akadhani ni uvivu wangu tu akasema mbona wengi wanatoa huko wanasema zipo kibao? Akaja mwenyewe tukazunguka naye akakubali kuwa ni kweli
Wakenya kwenye business wako vizuri na hupenda sana ubia pia.Biashara kwao ni kama family business wanahitaji wakuamini kwanza kabla ya kuku take into their family .Watanzania wengine subira hawana wanataka from day one awe CEO wa kampuni ya MKenya!!! OOH ni haki yangu hapa ni nchini kwangu!!! Haiendi hivyo
Kilichoua viwanda vyetu vilikufa sababu moja tulikabidhi watu wasio na elimu kuviendesha.Vilikuwa vimejaa darasa la saba na form four failure kama watendaji tofauti na EthiopiaNimeenda ethiopia bado wana maduka ya serikali. Bado wana mabasi ya umma. Wanafunzi wanakula shuleni. Ethiopia walikuwa wajamaa kama sisi. Viwanda vyao bado vipo. Ndege zao bado zipo toka miaka ya 1935. Kila kitu wanaendesha wao.
Sisi wapi tunakosea? Hatuwezi wategemea wakenya kutukuzia uchumi.
Sio wote wako wengine matapeliIla ni wajanja Sana kuwa makini Sana wao kukupiga au kukuzulumu ni dakika sifuri.
Umeongea vema. Lakini nikukumbushe. Wakati wa Nyerere viwanda viliendeshwa na hao hao unao waita darasa la saba. Na walifanikiwa na kulikuwa na soko. Viwanda havikufa wakati wa Nyerere vimekufa wakati wa kubinafsishwa. Lakini pia si kweli kuwa walioendsha viwanda hawakuwa wasomi. Nyerere alisomesha watu. Walisoma ndani na nje ya nchi. Na wengi wa viongozi leo ni hao waliosomeshwa wakati huo.Kilichoua viwanda vyetu vilikufa sababu moja tulikabidhi watu wasio na elimu kuviendesha.Vilikuwa vimejaa darasa la saba na form four failure kama watendaji tofauti na Ethiopia
Pili Soko la ndani halikuwepo la kutosha ku justify uwepo wa viwanda vyetu.Watu wengi walikuwa maskini wasio na uwezo wa kununua bidhaa zilizozalishwa kwa wingi na viwanda.Hivyo ma godown yakaanza kujaa bidhaa zisizo na soko
Mfano mmoja nilipewa wa kiwanda kiko Pugu road kilikuwa kinaitwa Light SOURCE kilikuwa kinatengeneza balbu .Nyumba zenye umeme zilikuwa chache Tanzania nzima huku kiwanda kinaunguruma usiku na mchana kuzalisha balbu.Zikakosa soko .Mtu akiomba likizo badala ya kulipwa nauli hela taslimu alikuwa anapewa box la balbu zinazolingana na pesa ya nauli yake akauze apate hiyo pesa yake.Wengi walitupa mabox ya Balbu jalalani na kwenda kushtaki vyama vya wafanyakazi kuwa mwajiri anawalipa bidhaa badala ya cash kama sheria ya kazi inavyotaka!!!
Tatu viwanda hivyo bidhaa walizokuwa wakitengeneza hazikuwa za viwango vya kimataifa zilikuwa duni zikawa haziuziki nje sasa machine na spea unaagiza nje wakati bidhaa hazina soko kubwa ndani wala nje.Shida ya pesa za kigeni ikatokea sababu ya mavita ya Uganda nk kwani pesa nyingi zilielekezwa vitani kunua vifaa vya kivita na kugharimia vita miviwanda ikaanza kufa kwa kukosa maintanance na baadaye miviwanda hiyo ikapitwa na teknolojia na hela za kuagiza mitambo ya teknolojia mpya serikali ikawa pesa haina za kigeni ndio miwiwanda ikafa ni si viwanda tu bali kuna hata mashirika ya umma yaliathirika na mabadiliko ya teknolojia kwa kiasi kikubwa mfano kampuni ya simu mitambo yao ya simu na miwaya yao ya nguzo ya simu za majumbani iliathirika baada ya ujio wa teknolojia ya simu za mikononi.Suppliers wenyewe wa Simu za kukoroga kama za kampuni ya Simu yetu kampuni zao zikafa ulaya na marekani baada ya wagunduzi wa teknolojia ya simu za mikononi kuingia sokoni.Na teknolojia ikiingia mpya sokoni bei yake huwa ghali mno au wenyewe hawataki kuiuza wanataka tu kuwekeza wao kama binafsi
Ethiopia bahati yao ni kuwa wao walikuwa na watendaji wazuri na wasomi na stable kwa pesa za kigeni soko la ndani na nje likiwa lipo na bidhaa zao kuwa kwenye viwango vya kimataifa kuanzia Ethiopian Airline nk
Mwisho vilikufa sababu vilikuwa haviendeshwi kibiashara ilikuwa kihuduma zaidi!!! Unakuta viongozi au bodi zimejaa wajumbe wa nyumba kumi ,wanasiasa wa chama tawala na vyama vya wafanyakazi nk watu ambao vichwani kibiashara wako weupe kichwani
Nakumbuka Bodi ya Tanesco mwenyekiti wake alikuwa Mkereketwa wa Tanu darasa la saba!!!