Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

labda sijaelewa unasikitika nn, lakn embu take moment mtu na hela zake mtanzania wa namanyele, ana details gani za aina ya biashra ya kufanya nchini kenya? hajui mtu kenya, na wala asitegemee support ya ubalozi wetu kule...

wao makejipanga. wao tayr wana information za kutosha kwa kila raia wao anayetaka kwnda kuwekeza au kufanya biashr tanzania. possibly atapewa mkopo wenye riba ndogo, atasemehewa kodi kwa upande wa kenya kwa kila bidhaa atakoyo itoa kenya kupeleka tanzania, kwa miaka fulani..

pengine, kwa mkenya atakaye kuja kuwekeza huku, moja ya mashrt ya kupata mkopo kwao, lazma aajir wakenya kiasi kadhaa katika top management, na mshahar usiwe less tha amount fulani..
sisi tumejipanga kwa hili ili tuseme ok njooni?
wao wana hakika hakuna mtanzania atakaye weza kushindana nao katika ardhi yao kibiashar labda mtanznia mwenye asili ya asia.

embu tufikirie nje ya box, balaz zetu zimetupa information gani za opportunities zilizopo kenya kwa watanzania, na how easy kuzi access hizo infor kwa raia wa kawaida.
Wewe ndiye unayetakiwa ufikiri nje ya box.Ni nani huyo atakayeenda nchi ya ugeni kuwekeza bila kufanya uchunguzi wa kina.labla kama anaenda kuuza utupu.japo ata na wenyewe lazima ajiridhishe mambo mengi.Na pia lazima ujue kua hayo mapungufu yote ni vitu vinavyorekebishika ni kiasi cha mamlaka husika kuweka mambo sawa.inawezekana uko nyuma hayakufanyika kwasababu mamlaka haikua tayari ila kama mamlaka ya sasa inataka kuweka mambo sawa sidhani kama hayo mapungufu hayatajadiliwa kwa kina.
 
Tupeleke Coaster zetu na Noah kibao tukazipaki nje ya kila airport, vituo vyao vya treni, mabasi na kila hotel. Watalii wakifikia tu pale tunawasomba na kuwavusha kuja kutembelea vivutio vyetu na kulala kwenye hoteli zetu....nadhani kuunda umoja wa wafanyabiashara wa usafirishaji wa watalii kutoka kenya kuja huku tena kwa bei ndogo zaidi ya huduma hiyo hiyo kwa upande wa Kenya inawezekena.

Tupeleke magari yetu wazi yenye vikundi vya ngoma wanenguaji wakicheza singeli na wanasarakasi kuzunguka mitaa ya nairobi yakiimba nyimbo za kutangaza vivutio vyetu, full mapicha kila mahali. Open spaces zao tupeleke vikundi vya ngoma na wanasarakasi kujitangaza kila jumamosi kuwa kila kilicho bora Africa Mashariki kipo Tz. Ikiwezekana kina Diamond na Harmonize wawe wanapelekwa kufanya show bure na wizara husika na wasindikizwe na wauza asali wa tz, wauza jam wa tz, wapaka ina...yaani mpaka watuelewe...

Usiku night club zao tujiwakilishe na vikundi vya matarumbeta na baikoko wajionee mambo ya kitamaduni ya huku watamani kuja uswazi wajionee wenyewe...
Wee jamaa! 🤣 🤣 🤣
 
Waken ni wabaguzi na wanawadharau watanzania.
Hii ya working permit itakuwa ni sawa kama India ingekuwa jirani zetu. Halafu waziri mkuu wa India akasema Watanzania mnaruhusiwa kuja kufanya biashara na kazi India bila vibali. Kama Tanzania nayo wakifanya the same.
Hii itakuwa one way traffic...Kenya ndio watanufaika na Hii!
Mahoteli yote ya kitalii na foreign companies zitakuwa zimejaa wakenya!!
Hii ya working permit imekuwa inapigwa dana dana kwa upande wa Tanzania kwa muda mrefu! Kwa sababu wanajua hadhara zake!!
 
Kipindi cha Magufuli mlikuwa mnasema watanzania wanahamishia biashara zao Kenya.
Sasa mbona kwenye idadi ya walio na biashara Kenya ni ndogo sana!
 
Huo mlima Kilimanjaro haujabrandiwa kuwa wa Tz, hata kwenye issue za guide books wanaonesha kabisa mlima uko Tz ila ukiwa Amboseli Game Park unaweza pata view yake pia. Ukiwa msafiri nafkiri utaelewa nacho zungumzia hapa!
Na hapo kumbuka faida kwenyu pia, watalii wakitaka kuuona full, si tunawaleta Tz au wao wenyewe wanaweza kuja next trip huko?

yeah sure!
 
Kenya ni rafiki zetu wa damu wa enzi na enzi.Tuondoe mambo za passport sababu inapunguza muingiliano maana kuipata tu hio paspot ni shida
 
Kwa jinsi wakenya walivyo wabaguzi,waTz wataweza kupenya kweli huko Kenya?Au Kenyatta analijua hilo ndio maana amecheza karata yake,ili na Mama Samiah aingie kichwakichwa kuruhusu wakenya huku?!!!
Usiseme 'WATAWEZA?'... Sema 'NITAWEZA?'. Kapambane na maisha, hakuna kizuri kitakufwata bila kuchukua some risks. Na ukianguka mara tisa, simama mara ya kumi!
 
mkuu ungeona jinsi wanavyokabili matatizo yao kitaalamu usingesema kitu hapa ,
kenyans ni smart kuliko sisi no doubt.
leo sisi tumejenga barabara kituko ubungo kibaha , zebra kibao kwenye super highway, matokeo yake ni ajali za waenda kwa miguu na boda boda kila siku , na matokeo yake foleni sasa imeahamia kibaha to mlandizi, angalia thika highway uone kama kuna makosa kama hayo,
sijui nani katushauri kuweka barabara za zege vituoni, kongowe kwa mfano, angekuwa mkenya pale angeweka under pass kwa gharama hizo hizo zetu na akatatua tatizo for good.
nitajitahidi kufanya utafiti juu ya thika highway mkuu. thanks
 
Waken ni wabaguzi na wanawadharau watanzania.
Hii ya working permit itakuwa ni sawa kama India ingekuwa jirani zetu. Halafu waziri mkuu wa India akasema Watanzania mnaruhusiwa kuja kufanya biashara na kazi India bila vibali.
Mfano uliotoa ni Zero huna upeo wqa uelewa kabisa ni zero

Sisi hapa tuna wahindi kibao raia wa Tanzania ndio wanachukua dengu ,ufuta ,korosho zetu nk kwenda kuuza India wakifanya hivyo tena poa sana sababu wahindi watanzania wenzetu wataenda fungua miofisi kule badala ya kutumia middlemen walioko kule waruhusu hata leo uone tutakavyofaidi hadi soko lao la mazao yetu na madini .Jaipur kuna mtaa mzima kazi yao kutengeneza vito vya Tanzanite ambayo hupelekewa na wahindi wa kule sisi tutaenda wenyewe na kuweka Duka JAIPUR
 
Nilichogundua wapingaji wengi ni vibarua wanaofanya kazi serikalini na wanasiasa waponea siasa!!! ambao hawajui lolote ya kilichoko mitaani .NA TU VYETI TWAO WAMEKAA OFISINI na kujiita wataalamu hovyo kabisa.Wapige chini hata leo uone watakavyokonda siku mbili hawajui hata waanzie wapi maisha mtaani na waishie wapi

Sisi tunajua Kenyatta alichofanya kina maana kubwa kwa wachacharikaji wa mitaani lakini kwa vibarua wa serikali na vibarua wala kutegemea siasa na kupifga domo bungeni uamuzi huu wanauona siyo!!!

Nyie vibarua wategemea mwisho wamwezi shut up achieni watu wa mitaani wa hali ya chini kwao linaeleweka
 
mifumo yetu ya kodi ilio kandamizi na isiyo rafiki kwa wafanya biashar, hasa kwa miaka 5 nyuma, kwa mwendo wa mama itarekebiaka..

kufanya biashra ama kuwekeza kenya kama mtanzania hilo sahau, labda kuuza mitumba au kuimpot bidhaa zao za viwanda kuja kuzitupia huku
Hawa ndugu zenyu wanauza mitumba pia?
Wenye village supermarket pia nao utawaambiaje, watoke KE?
Na wako wengi tu, so acha kupotosha, kama huwezi ni wewe, wenzio wana hela ya kuja kuwekeza KE.

IMG_20210506_125027.jpg
 
Sisi kule tunampaka washona viraka vibarazani kawaida tu wakiuza nyanya sisi tutauza vitunguu
Mwambie huyo. Kule nilipozaliwa, hadi wa leo wabongo wako tu sana, wamezalia huku na wabongo wenzao, watoto wamekuwa wakubwa huku nikiwaona na sioni shida yoyote wanayopitia. Sana sana wa hapo mtaani ni fundi cherahani wabobezi sana, wanashonea wamama na dada nguo nzuri sana.
 
Nakubaliana na wewe kabisa
ila tumelala sana inabidi tuamshwe kutoka usingizi mzito, kenyans are very skilled , na kweli wana roho mbaya linapokuja swala la kazi ,kumbuka wenzetu ni mabepari by default. na ni money hungry always ,
inabidi tupate external force tuamke, ilannahisi mazingira ya kodi hapa kwetu lazima watoke mbio.
Who's not 'money hungry' in this world. Even Bill Gates & Elon Musk, still work, despite of them being super wealthier!
Ukija Tz ka mfanyabiashara, kodi iko juu, why, coz you're hungry for that extra shilling. So mambo ya pesa weka kando kabisa, hakuna asiyependa.
Hiyo issue ya roho mbaya ya wa KE, siijui, wewe kama ulitendwa na mkenya, mezea, ndio hali ya maisha hiyo,sana sana kwa hizi nchi zetu za Afrika. Kabla utoboe, utatobolewa kwanza... 😂 😂 😂
 
Kwani makubaliano ni kitanzi! ya kuwa ukisha jitia kitanzi unakufa tuu?
Tukion kuna mambo si sawa si tunarekebisha !
Wacheni woga Watanzania .
Ruhusu wakenya waje TZ wfanye kazi bila Working Permit na waanzishe biashara zao hapa.
Mimi namiliki shule, Walimu kutoka kenya ni wazuri sana Mashuleni, lakini shida kuwalipia Resiident permit kila mwaka.
Walimu wa kwetu Kiengereza hawajui, na wengi wababaishaji. Sijui inakuaje?
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom