Rais kapotoshwa na wasaidizi wake utenguzi wa Kairuki?

Mtoa maada inaonekana unamjua zaid uyu mama,ni kazi gani south Africa alikuwa anafanya hadi kulipwa 15,000 USD..mpaka sas amefanya lipi TIC la maana astahili kulipwa mshahara huo TZ..umesoma report ya CAG,ebu kaipitie na wew alaf uje kusema kama anasatahili kulipwa mshahara huoo...

soma hapo uone uteuzi wake, kazi ya awali na elimu yake. kama sababu ya kufukuzwa ndio iyo iliyotolewa , uyu dada ajatendewa haki
 
Attachments

  • viewer (1).png
    viewer (1).png
    42.2 KB · Views: 27
Watu wanaona wakimlaumu JPM ndio wanapata 'response' nyingi hata kwa mambo ambayo rais hapaswi kulaumiwa. Tunaelekea pabaya. Kama unashindwa kuona posho ya milioni kumi na tano huku mtu akisubiri mshahara wa milioni kumina tano halafu uwekezaji wenyewe ndio huo, basi JPM aiache tu hii nchi iende ilikokuwa inaelekea maana kila kitu kwetu ni kibaya. Mafisadi, mafisadi, wezi, wezi wakianza kushugulikiwa wanadhalilishwa, wanadhalilishwa.Kuna mtu alisema kuwahurumia na kuwasaidi watanzania ni kama kumuokoa mtu aliyeza matopeni. Akitoka huko atakuuliza umenitoa matopeni nguo ziko wapi na mimi nipo uchi.Ukimwambia sina nguo nilikuwa naokoa maisha yako atakuuliza kwa nini sasa umeniokoa. Ukimsaidia kumuelekeza njia lazima pia umpeleke.
Sijui Tufanyiwe Nini Watz Jaman.
 
Hivi tatizo hamlioni au mnasingizia halionekani?? Huyu mama misafara mingi ya rais wa awamu ya 4 alikuwemo!! Na ndie mnasema alimshawishi eti aje TZ kwa elimu gani alionayo huyo mama??hivi bongo kuna upungufu huo wa wasomi hadi huyo mama ashawishiwe aje apokee mshahara wa chini? Naangalia tu hii issue kwa jicho la tatu!! Hapa kazi tu.

Tiririka Mkuu uwafundishe jinsi ya kujenga HOJA watu humu. Nakukubali sana Mkuu!
 
Hili gazeti limenihakikishia kuwa mama alikuwa anapewa milioni 5 siyo 18 wanazozusha, Hii inanisaidia kuconnect dots kwamba Mama wamemtoa South Africa alipokuwa akilipwa Vizuri, Kufika huku Wanampa Milioni Tano tu!!!. Hii siyo Fair hata Kidogo
Kama ndo hivi bas ile sekretarieti au bodi ya mishahara nayo ni jipu.......
 
Kukaa South Africa katika nchi unayosema ina Uchumi mzuri haku justify kuwa basi lazima kila Mtu tu atalipwa pesa nyingi au anayoitaka yeye. Mkaburu ninayemfahamu Mimi na ambao ndiyo wamehodhi karibu 60% ya Utajiri na Uchumi wa South Africa huku Waingereza, Wamarekani na Waholanzi wakihodhi 30% na Waafrika wenyewe hizo 10% zilizobaki leo akupe Wewe Mwafrika Mshahara wa 35 Million Tshs! Utawapata hao hao wasiokuwa na exposure na hizi nchi ila kwa waliobahatika kuzitembelea, kuishi na hata kufanya huko Kazi nadhani watakuwa wanakucheka tu " kimtindo ".

Mkuu Kamshahara ka 35M Ni kadogo sana aisee. hapa hapa Nchi hii hii unayoishi kuna watu zaidi ya 500 wanaolipwa zaidi ya huo mshahara.

Kinachokusumbua wewe ni WIVU NA ROHO YA KOROSHO.

Wasalaam!
 
Kama ningekuwa ni Lecturer halafu nimekupa Assignment na ukaja na majibu kama haya ningekupa 0.1%. Halafu ni bora hata usingetuwekea na hayo mengineyo kwani kwa tunaojua KUFIKIRI KISAWASAWA kama huyo Dada angekuwa anajiamini na kweli ni MWELEDI asingethubutu kuja kufanya Kazi huku Tanzania huku akijua fika kuwa Mshahara wake utakuwa ni that amount. Halafu kusema kuwa alikubali kufanya Kazi kwa Mshahara huo ili kuonyesha UZALENDO wake kwa Tanzania ni HOJA nyepesi sana na MFU pia. Hufanyi Kazi kwa ajili ya UZALENDO na kama ni Kazi za UZALENDO zipo na zinajulikana.

Mwisho acha kutufanya sisi Watoto wadogo kwani kwa tunaomjua Vasco Da Gama huyo Bidada yawezekana alikuwa ni mboga yake ya fasta fasta na kuna uwezekano hata hizo Hela kweli alikuwa hapewi lakini huku kwa Vasco Da Gama alikuwa anapewa usikute hata zaidi ya huo mshahara wa TIC.

Hivi kwa AKILI tu ya kawaida kuna Mtanzania anayeweza kufanya kazi au kuwepo Ofisi fulani tena kubwa halafu akatae MSHAHARA? Kwa tunaoijua nchi hii in and out huyo Dada kuna mahala ambapo alikuwa anafaidika napo tena kwa kutumia mgongo wa Vasco Da Gama na UZI wako huu uliodhani kuwa utauanzisha ili kumtafutia sympathy kwa public basi nikuhakikishie ndiyo kwanza umeuwasha moto kwani Wapo watu wanaomjua pengine kuliko hata anavyojijua yeye au unavyomjua Wewe na sasa wataanza " kutiririka " hivyo Wewe na yeye muwe WAVUMILIVU kwakuwa mmeyataka wenyewe.

Halafu kama una uungwana jaribu kuwaomba radhi hao unaowaita " informers " wa Rais kwa kuwaambia kuwa WALIKURUPUKA na kumpelekea Bosi wao Mheshimiwa Rais UMBEA kwani umeshindwa kujua kuwa hata wao TAARIFA zao huwa ZINACHUJWA vilivyo kwa UMAKINI wake ili zisije kuleta MADHARA yoyote pindi Bosi wao Mheshimiwa Rais atakapolizungumza au kulitolea UFAFANUZI hivyo maneno uliyoyasema dhidi yao ni DHIHAKA kubwa kwao na KUWADHARAU pia.

Siku nyingine ukija na UZI wa tukio la aia hii uapoandika jaribu sana kuwa objective na siyo subjective. Naomba niishie hapa tafadhali!
Huyu mleta mada atakuwa julieth mwenyewe ama kuna mtu amepewa kazi ya kuanza kumtafutia public sympathy.hovyo kabisa.
 
Decision making process from 2013 to 2015 almost two years without reaching a decision!!!!!!!!! I have no good words to conclude
 
refer kwenye cv ya uteuzi wake iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano ikulu alipokuwa ameteuliwa.Alikuwa anafanya kazi na The Banking Association of South Africa kama meneja MKUU wa idara ya BANK na FEDHA. Nafikiri unajua maana yake..Usitake kuniambia MENEJA MKUU analipwa hela mbuzi..acheni kutetea vitu vya kijinga.

Na ndiyo maana ukawa LAST EMPEROR kwani wale EMPERORS wote wa mwanzo waliondoka na AKILI zao zote zile kubwa na nyingi na zile mbaya au makapi ya akili zao ndiyo umebaki nazo Wewe.
 
Habari wanaJF,

Kufuatia kuteguliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki taarifa za ndani zinasema bibie huyu kaonewa kwa sababu zilizoainishwa katika nukuzi ya taarifa hapa chini.

"Huyu Julieth ni mke wa Dr.Kairuki Mkurugenzi wa Mikocheni Hospital. Kabla ya kuja Tanzania alikua anafanya kazi South Afrika akilipwa mshahara wa USD 15,000. JK ndiye aliyemkuta SA akamuomba arudi nchini kuja kusaidia pale TIC baada ya Ole Naiko kustaafu. Kabla hajaja wakaset T&C kuwa her salary wont go bellow 18M Tzs.

Ikumbukwe SA alikua akilipwa 15K USD equals to 35M Tzs. Kwahiyo kukubali kulipwa 18M ni kukubali kusucrifice 17M kitu ambacho si rahisi kwa watu wengi. Lakini she did that for the sake of her country. But alipofika nchini TIC wakamwambia hawana scale ya 18M, wakataka kumlipa 5M. Huyu mama akakataa. She cant be that cheap kutoka mshahara wa 35M kule SA hadi 5M? Akamwomba JK arudi SA kuendelea na kazi yake, lakini JK akaagiza TIC wafanye salary review ili kuweza kuaccomodate madai yake. Kipindi chote hicho alikua hapokei mshahara b'se alikua hajafikia concesus na serikali. Sasa kabla TIC hawajakamilisha salary review ndio JPM akawa ametake power. Akawa anadiscourage mishahara mikubwa kwa wakuu wa mashirika ya umma.

TIC wakaogopa kuendelea na review ya Kairuki. Katika ufuatiliaji JPM akaambiwa kuna Mkurugenzi hajapokea mshahara tangu 2013. Lakini informers wake they didnt nail the whole story. Wao wakamwambia tu amekataa mshahara aliopangiwa anataka mkubwa zaidi na marupurupu makubwa. JPM akahamaki na kutengua uteuzi without knowing the truth. Hapa JPM kafanya kosa lakini simlaumu yeye, nalaumu informers wake. Basing on the facts provided huyu mama kaonewa sana and worse enough JPM hakumuita kumsikiliza. He just made decision basing from his informers.

This is typical injustice b'se principles of natural justice were abandoned. Ni bora JK angemruhusu arudi SA kuendelea na kazi yake"

Karibuni wadau.

Mkuu, unaelewa unachokiongea?

Je wewe umefanya kazi TIC?

Umefanya kitengo gani?

Unafahamu kilichokuwa kikifanyika pale TIC?

Unaifahamu Task Force ya raisi JPM na serikali yake, Scope ya kazi yake na approach yake kwa issue kama hii?

By the way mheshimiwa raisi anataka timu mpya kila mahala muhimu.

Kama wewe unafanya kazi hapo basi hufahamu kitu ila itakuwa umesikisikia tu.
 
Umemmaliza vilivyo mleta mada mkuu.huwezi kumlipa kila mkurugenzi wa shirika la umma salary aliyojipangia yeye.

unajua tatizo nchi hii kubwa ni tumezoea kupata ajira za kusimamiwa na magod fathers na tunaona huo ndio utaratibu sahihi. utaratibu huu umeua ushindani na ndio unadidimiza nchi kiumasikini.

watu wameajiriwa kushika nyadhifa kubwa lakini hawajui A wala B ya ofisi zao zinafanya nini. wamekuwa kama wafalme wa uingereza kwenye mashirika wakihusika kusaini, kusafiri, kufanya dili.

wanaingilia wataalamu kufanya maamuzi ya blanda, what they feel is only power they have lakini knowledge hakuna na maamuzi yao watu kama hawa ni ya kuonyesha wana power hivyo wanawabishia wataalamu kujionyesha wana power.

ili kuleta tija katika taasisi zetu ni jambo la kwanza uongozi urudishe competion na utaalamu katika utendaji.
 
Mkuu nimemtahadharisha kuwa alidhani akianzisha hii mada atamsaidia kumtengenezea public sympathy lakini kumbe hajui kuwa ndiyo kwanza ameshaamsha CRITICAL THINKERS ambao walikuwa wamenyamaza na sasa wanaanza KUFUNGUKA. Ameyataka mwenyewe hivyo nafurahi sana ninavyoona mnatiririka KIMANTIKI kabisa ili mumfundishe mleta mada jinsi ya kufikiri. Nimemdharau kupita kiasi muanzisha UZI halafu huko alipo usikute na yeye anatamba kabisa kujiita either intellectual or academician.
mkuu hii mada unaitendea haki kweli kweli
 
Huyu mleta mada atakuwa julieth mwenyewe ama kuna mtu amepewa kazi ya kuanza kumtafutia public sympathy.hovyo kabisa.

Sasa kakukata na Vichwa vyetu ambavyo tutamfanya awe labelled kama PUBLIC ENEMY number 1 na tena asituchezee kabisa. Hata hawa wote wanaojifanya kumtetea humu 100% na wao ni MAJIPU.
 
Ungejua vizuri kuwa huyu taasisi ni yeye ni mwenyewe,na wanaomshauri anatishia kuwafatilia kama alivyofanya kwa kijo kisimba usingesema ni taasisi.Nashangaa dada yako wa kinyarwanda anaonewa na ana haki lakini hutaki kusema ukweli kuwa kuna blunder mahali!au ndo mapenzi kwa chama?

Sasa kwa taarifa yako huyu mama ni jipu lililoiva, hapo wametumia lugha nyepesi tu kua hakuwahi kuchukua mshahara, lakini kwa sie wenye weledi hilo ni jipu haswa..na huyo mama alikua mshirika mzuri wa mukulukulu wa awamu ilopita..hizi nyingi hapa ni ngonjera tu but deep down wajanja tunajua..hapa kazi tu
 
Habari wanaJF,

Kufuatia kuteguliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki taarifa za ndani zinasema bibie huyu kaonewa kwa sababu zilizoainishwa katika nukuzi ya taarifa hapa chini.

"Huyu Julieth ni mke wa Dr.Kairuki Mkurugenzi wa Mikocheni Hospital. Kabla ya kuja Tanzania alikua anafanya kazi South Afrika akilipwa mshahara wa USD 15,000. JK ndiye aliyemkuta SA akamuomba arudi nchini kuja kusaidia pale TIC baada ya Ole Naiko kustaafu. Kabla hajaja wakaset T&C kuwa her salary wont go bellow 18M Tzs.

Ikumbukwe SA alikua akilipwa 15K USD equals to 35M Tzs. Kwahiyo kukubali kulipwa 18M ni kukubali kusucrifice 17M kitu ambacho si rahisi kwa watu wengi. Lakini she did that for the sake of her country. But alipofika nchini TIC wakamwambia hawana scale ya 18M, wakataka kumlipa 5M. Huyu mama akakataa. She cant be that cheap kutoka mshahara wa 35M kule SA hadi 5M? Akamwomba JK arudi SA kuendelea na kazi yake, lakini JK akaagiza TIC wafanye salary review ili kuweza kuaccomodate madai yake. Kipindi chote hicho alikua hapokei mshahara b'se alikua hajafikia concesus na serikali. Sasa kabla TIC hawajakamilisha salary review ndio JPM akawa ametake power. Akawa anadiscourage mishahara mikubwa kwa wakuu wa mashirika ya umma.

TIC wakaogopa kuendelea na review ya Kairuki. Katika ufuatiliaji JPM akaambiwa kuna Mkurugenzi hajapokea mshahara tangu 2013. Lakini informers wake they didnt nail the whole story. Wao wakamwambia tu amekataa mshahara aliopangiwa anataka mkubwa zaidi na marupurupu makubwa. JPM akahamaki na kutengua uteuzi without knowing the truth. Hapa JPM kafanya kosa lakini simlaumu yeye, nalaumu informers wake. Basing on the facts provided huyu mama kaonewa sana and worse enough JPM hakumuita kumsikiliza. He just made decision basing from his informers.

This is typical injustice b'se principles of natural justice were abandoned. Ni bora JK angemruhusu arudi SA kuendelea na kazi yake"

Karibuni wadau.
***common sense arguments***
mkuu, are you supposed to mean that, this lady has been working in that center since 2013 without having valid contract documents in her hands??? if not so, how does the salary provision in the stand in this regard???
JK akaagiza TIC wafanye salary review ili kuweza kuaccomodate madai yake. Kipindi chote hicho alikua hapokei mshahara b'se alikua hajafikia concesus na serikali.
how many decades does the salary review process takes??? and how comes this lady kairuki was willing to keep serving when knowing the dispute was yet unsettled???
 
Hili gazeti limenihakikishia kuwa mama alikuwa anapewa milioni 5 siyo 18 wanazozusha, Hii inanisaidia kuconnect dots kwamba Mama wamemtoa South Africa alipokuwa akilipwa Vizuri, Kufika huku Wanampa Milioni Tano tu!!!. Hii siyo Fair hata Kidogo

Kwani Mshahara ni lazimauwe mkubwa bila kujali aina ya kazi au kitu gani unachozalisha ili mradi ulifikia mshahara wa juu? Fair maana yake nini? Je inahusisha upande mmoja kunufaika na mwingine kuumia? Maan mimina maneno ya kizungu tuna ugomvi.
 
Hahahaaa,asante Kagame mdogo

Ulipomtaja tu Rais wangu Paul Kagame nimefurahi mno na nafurahi pia nanyi Tanzania kuongozwa na Msubi John Magufuli ambaye hana tofauti na Watutsi kwa UTENDAJI mzuri wa Kazi, UTHUBUTU, KUJIAMINI na MAAMUZI magumu na ya mwisho. Sitoshangaa huko mbele nikija kusikia Rais wa Tanzania ana asili ya huku Kwetu nchini Rwanda hasa wa Kabila letu LILILOBARIKIWA na Mwenyezi Mungu la WATUTSI.
 
Mkiona rais jpm yupo sahihi kutumia taarifa potofu za informer, basi rais jpm alikosea kumfuta kazi mama anna kilango malechela.

Nasema hapana raisi.hajamwonea huyu mtaalamu wala mama kilango.Nianze na mama Anne Kilango.Huyu kwa vyovyote asingweza kwenda na kasi ya raisi Magufuli.Huyu na wengi wa aina yake walizoea kufanya kazi kwa mazoea tu.Kuagiza kuletewa taarifa na kuandaliwa yeye abebe sifa.Alikuwa na vyombo vyote mkoani kwake na viko chini yake.Kwani unafikiri alichokifanya raisi kugundua uozo wa watumishi hewa Shy ni nini?Alimwagiza afisa wa usalama wa taifa mkoa kumtafutia ukweli wa watumishi hewa mkoani Shinyanga.Kwa wilaya tatu tu wakawa wameshawagundua 45 na hadi sasa ni zaidi ya 200.Chombo hicho angeweza kukitumia Kilango na kuoanisha na taarifa alizoletewa na watendaji.wake kabla hajamdanganya raisi na kulisababishia taifa hasara.Tuje kwa huyo mtaalamu alieajiriwa toka 2013 bila kuchukua mshahara hata mwezi mmoja.Hivi kwa ukubwa wa nafasi yake hakujiuliza kuwa ikibainika kwa miezi yote 30 akifanya kazi bila kuchukua ujira kiongozi wake wa nchi angemwelewaje?Ni mjeuri akitaka kushindana na serikali kwa kuiziria mishahara au amweleweje?Atamwelewa anaishi kwa jeuri ya rushwa na madili makubwa kwenye nafasi yake?Hivi kwa nafasi na cheo chake kikubwa ikulu si anaenda akipenda?Ni kwa nini hakufikiria katika uongozi wa raisi kwa miezi sita kwenda kumwona na kumweleza shida ya mshahara wake?Mnatakiwa mtofautishe uongozi wa Kikwete na Magufuli wa hapa kazi tu.Kwa hili namsafisha raisi na lawama zozote.
 
Back
Top Bottom