Rais Joseph Kabila Mashakani

hata mwanaHALISI nadhan

Ni mwanaHALISI mkuu, nilikuwa nalo ntajaribu kulitafuta stoo - mkuu ukiangalia picha ya Joseph ukalinganisha na picha ya Adrien Christopher Kanambe wamefanana kama mapacha vile wala mtu haitaji vipimo vya DNA ku prove hilo.

Hila sina uhakika kama Joseph aliwahi kutumia jina la Kanambe wakati anasoma na kuishi DSM TANZANIA, alafu hili suala la kusema Joseph wakati mwingine alikuwa anaishi maisha ya kubangaiza hapa DAR naona hilo si kweli, Mzee Kabila alikuwa na Biashara zake za kuaminika akishilikiana na Kazzadi, hawakuwa na njaa wale labda useme jambo lingine siyo ukame wa fedha.

Joseph aliwahi kwenda Uchina kwenye mafunzo ya kijeshi, aliye mpeleka huko ni Kabila Sr.mwenyewe siamini kama Rwanda ilihusika na hilo; mambo mengine yakiwekwa chumvi yankosa credibility. Mimi ningebishi kama nisinge wahi kuona picha ya Joseph na Kanambe na ndio maana niliamua kuziweka kama kumbukumbu.
 
Ni mwanaHALISI mkuu, nilikuwa nalo ntajaribu kulitafuta stoo - mkuu ukiangalia picha ya Joseph ukalinganisha na picha ya Adrien Christopher Kanambe wamefanana kama mapacha vile wala mtu haitaji vipimo vya DNA ku prove hilo.

Hila sina uhakika kama Joseph aliwahi kutumia jina la Kanambe wakati anasoma na kuishi DSM TANZANIA, alafu hili suala la kusema Joseph wakati mwingine alikuwa anaishi maisha ya kubangaiza hapa DAR naona hilo si kweli, Mzee Kabila alikuwa na Biashara zake za kuaminika akishilikiana na Kazzadi, hawakuwa na njaa wale labda useme jambo lingine siyo ukame wa fedha.

Joseph aliwahi kwenda Uchina kwenye mafunzo ya kijeshi, aliye mpeleka huko ni Kabila Sr.mwenyewe siamini kama Rwanda ilihusika na hilo; mambo mengine yakiwekwa chumvi yankosa credibility. Mimi ningebishi kama nisinge wahi kuona picha ya Joseph na Kanambe na ndio maana niliamua kuziweka kama kumbukumbu.

Na kuhusu udereva wa taxi ni kweli?
 
Rais wa Congo DRC Joseph Kabila ana wakati mgumu na wa mashaka kufuatia matukio kadhaa yanayoendelea within his perimeters. Ukiachia matukio kadhaa ya kujaribu kumuua kama lile la February 27, 2011 ambapo alijeruhiwa lakini ikafanywa siri, hivi sasa ameongeza maadui baada ya rafu za uchaguzi. Ulinzi wa Kabila unafanywa na Wanajeshi wa Rwanda na usalama wake ukiratibiwa na Jenerali James Kabarebe, waziri wa Ulinzi wa Rwanda. Wakongomani wanaompinga wana sababu ya msingi. Utata wa historia yake. Yeye si raia wa DRC, wala si mtoto wa Kabila, bali ni kibaraka wa Kagame. “pot aux roses” kama wasemavyo wafaransa. Mambo yaliyokuwa sirini sasa yanabainika
Utata wa historia yake unatokana na uthibitisho wa kustaajabisha uliotolewa na unaoendelea kutolewa na watu walio karibu na historia yake kwamba Joseph Kabila hakuwa na undugu wowote na Marehemu Laurent Kabila, ni mtutsi wa Rwanda, hana uraia wa Kongo DRC na Jina analotumia sio halisi. Simulizi na shuhuda mbalimbali zimekuwa zikitolewa na watu waliokuwa karibu na familia ya Baba yake wa kufikia Laurent Kabila, na Baba yake halisi Adrien Christopher Kanambe kuhusu historia sahihi ya Rais huyo wa Congo DRC. Inasemekana kuwa, jina halisi la Rais Joseph Kabila ni Hippolyte Adrien Christopher Kanambe aliyezaliwa na pacha wake Janet Adrien Christopher Kanambe mnamo June 4, 1971 nchini Rwanda kwa Baba Mtutsi aliyeitwa Adrien Christopher Kanambe, na Mama Mtutsi aliyeitwa Marceline Makumbukuje. Adrien Christopher Kanambe, baba wa mapacha Hippolite na Janet, kama ilivyokuwa kwa Watutsi wengine, alikuwa mpinzani mkubwa wa serikali ya Rwanda iliyokuwa ikiongozwa na Rais Juvenal Habyarimana aliyekuwa Mhutu na hivyo alikuwa akiendesha harakati za uasi akiwa na kundi lake la waasi katika milima ya Manyema mpakani mwa Congo DRC (Zaire) na Rwanda. Laurent Kabila kwa upande wa pili naye alikuwa akiendesha harakati za kuiondoa madarakani serikali ya Mobutu Sese Seko hata alipokutana na Christopher Kanambe katika milima hiyo ya mpakani na wakaunganisha nguvu dhidi ya maadui zao wakubwa Mobutu na Habyarimana. Waliingia mkataba kuwa waunganishe nguvu kumuondoa Mobutu, na baada ya hapo kwa umoja huo huo wamuondoe Habyarimana. Katika umoja wao, Laurent Kabila alikuwa ndiye mkuu wa umoja huo ambapo Adrien Christopher Kanambe alikuwa mkuu wa Jeshi la Watutsi, na Jenerali Kaliste Majaliwa alikuwa mkuu wa Jeshi la Wakongomani. Kwa pamoja waliunda kundi lililoitwa PRP (Party of the Peoples' Revolution)ambalo makao yake yalikuwa Wimbi mashariki ya Congo. Mnamo mwaka 1984, PRP waliaandaa mpango kabambe wa kuuteka mji muhimu wa Moba ambao ulikuwa unashikiliwa na majeshi ya Mobutu. Kanambe alipewa jukumu la kuongoza operesheni hiyo. Hata hivyo majeshi ya Mobutu yalikuwa na nguvu zaidi na kuwasambaratisha majeshi ya PRP yaliyoongozwa na Kanambe. Waasi wengi walikufa katika operesheni hiyo na Kanambe mwenyewe kujeruhiwa. Kabila (Laurent Kabila) akiwa Wimbi alimtuhumu Kanambe kwa usaliti uliopelekea shambulio hilo kushindwa. Hivyo Kabila aliuamuru Kanambe auawe na kutoswa ziwani. Kanambe akitokea Moba alipokewa na wakongomani waasi wachache, bila kujua kinachoendelea, walitumia Boti kuelekea Wimbi ilipokuwa ngome yao kuu. Wenzake hao walimuua na kumtosa ziwa Tanganyika kama ilivyoamriwa na ndio ulikuwa mwisho wa Adrien Christopher Kanambe. Mbali ya kumtuhumu kwa uasi, lakini pia kuna madai kuwa Kabila aliamua kumuua Kanambe ili amuoe mkewe Marcelina ambaye walikuwa na mahusiano ya siri. Hippolite na Janet walikuwa na umri wa miaka 13 wakati baba yao anauawa. Baada ya hapo Kabila aliwachukua Marcelina (mjane wa Marehemu Kanambe), Hippolite na Janet na kuwapeleka Dar es Salaam ambapo aliwatafutia nyumba maeneo ya Masaki. Hippolite Kanambe (Joseph Kabila) na Janet waliendelea na elimu yake Msingi hadi Sekondari Dar es Salaam wakiwa wanajulikana kwa majina ya Hippolite na Janet Kanambe. Shule ya msingi walisoma Lumumba Primary School na Shule ya Sekondari walisoma Zanaki, Hippolite akiwa mvulana pekee. Pia miaka ya 1992/93 walihudhuria mafunzo ya awali ya Kijeshi JKT Makutupora. Kabila alikuwa na wake wapatao 12, na watoto wengi. Kutokana na harakati zake za kumngoa Mobutu, Kabila hakuzikumbuka sana familia zake na hivyo Hippolite (Joseph) alilazimika wakati mwingine kufanya vibarua katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ili kuweza kuitunza familia. Inasemekana alifanya ya Taxi driver na biashara ndogondogo. Mwaka 1995 Hippolite Kanambe aliamua kwenda kwao Rwanda kujaribu maisha huko, alifikia kwa mjomba wake Kanali James Kabarebe ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ulinzi wa Rwanda, na ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Usalama katika Jeshi la APR. Kabarebe alimtumia Hippolite katika shughuli zake mbalimbali na pia kama dereva wake binafsi. Mwaka 1996 alimuingiza Jeshini na baada ya mafunzo alipangiwa Division maalum aliyohusika na operesheni za Zaire ya Mobutu. Mwaka huo huo 1996 nchi za Rwanda, Burundi, Angola, Uganda na waasi wa Sudani Kusini ziliunganisha nguvu na kuunda umoja ulioitwa AFDL au ADFLC (Alliance of Democratic Forces for the Liberation of Congo-Zaire) kwa ajili ya kumsaidia Kabila na PRP yake kumngoa madarakani Mobutu. Kabila alikuwa ndiye Mkuu wa operesheni za AFDL ambapo Kabarebe (Mkuu wa Usalama Jeshi la Rwanda na Mjomba wa Hippolite) , alikuwa mshauri Mkuu wa Kabila wa masuala ya kivita. Ni wakati huu ambapo Kabila alimuita Hippolite na kumteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Watoto (Kadogos). Katika Jeshi la Kadogos alijulikana kama Major Hyppo. Baadaye, kwa ushauri wa Kabarebe, kwa lengo maalum, Kabila aliamua kumtambulisha Hippolite kama mtoto wake na kumpa jina la Joseph ( Joseph Kabila). Baada ya kumgoa Mobutu madarakani mnamo mwaka 1997 na Kabila kuwa Rais wa Congo, alimteua Kabarebe kuwa Mkuu wa Majeshi na pia alimpeleka Kabila China kwa ajili ya Mafunzo ya Kijeshi kwa muda wa miezi miwili. Hata hivyo, Kabarebe hakukaa sana na madaraka yake hayo kwani kulitokea uvumi kuwa ana mpango wa kumpindua Kabila na pia Wakongomani walilalamikia nchi yao kuvamiwa na Wanyarwanda. Kutokana na sakata hilo Kabila aliamua kumuondoa Kabarebe ambaye alirejea kwao Rwanda. Baada ya kurejea kutoka mafunzoni China, Joseph Kabila (Hippolite Kanambe) aliteuliwa kuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la DRC. Aidha, alikuwa ndiye mshauri na mtu wa karibu aliyeaminiwa sana na Mzee Kabila. Pia alikuwa na mamlaka na sauti kuliko kiongozi mwingine yeyote, na alikubalika kwa maamuzi yake mazuri na kwa kujali maslahi ya wanajeshi na watendaji wengineo. Kabila alimtelekeza Marcelina (Mjane wa Adrien Christopher Kanambe) ambaye wakati kwa wakati huo alikuwa akiishi Rwanda. Aliingia Ikulu akiwa na mkewe Sifa Mahaya. Mnamo mwishoni mwa Oktoba, 2000 Kabila aliwekewa sumu kwenye Chakula na kunusurika kifo baada ya kuwahishwa hospitali. Uchunguzi uliofanywa na Idara ya Ulinzi wa Rais ulimhusisha moja kwa moja mkewe Sifa. Mzee Kabila aliamuru Sifa awekwe Jela wakati uchunguzi unaendelea. Mchana wa tarehe 16 Januari 2001, Mzee Kabila aliuawa kwa kupigwa risasi na Askari mtoto aliyeitwa Rashisi Kasereka (Kadogos !) aliyekuwa mlinzi wake ambaye naye aliuawa kwa kupigwa risasi na askari aliyekuwepo katika tukio hilo. Sifa ambaye muda wote iliaminika kuwa yupo Jela, alionekana akiwa na Joseph katika mazishi ya Mzee Kabila. Baada ya kuuawa kwa Laurent Kabila mnamo 2001, Joseph Kabila alichukua madaraka ya Urais wa mpito. Katika uchaguzi wa Rais wa 2006 aligombea na kushinda na amekuwa Rais wa DRC mpaka hivi sasa. Miaka zaidi ya 10 imepita tangu “Baba yake” auawe. Hata hivyo Rais Joseph Kabila amekuwa akipinga pendekezo lolote la kuendeleza uchunguzi wa kifo hicho japokuwa watu zaidi ya 50 wamewekwa kizuizini bila mashtaka kuhusiana na mauaji hayo. Katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari, Kabila iliwahi kuulizwa na Mwandishi wa France 24, Arnaud Zajtman kuhusu suala hilo. Ambapo alijibu “Mara kadhaa nimemjibu kuhusu suala hilo, na leo jibu langu ni lilelile. Makosa yaliyofanyika wakati wa kipindi cha mpito ni kudhani kuwa tunaweza kufikia maelewano bila mahakama.” Viongozi wa dini mbalimbali na wapigania haki za binadamu wamekuwa wakishinikiza kufanyika kwa uchunguzi ili wauaji wajulikane na sheria ichukue mkondo wake, na hao ambao wamewekwa kizuizini pengine bila hatia waweze kuachiwa huru.
Kabila anasumbuliwa na mzimu wa Etienne Tshisekedi ...
 
Mkuu nadhani hata humu imekuwemo tena nadhani mwezi uliopita kama si mwezi huu. Niliisoma ila ina tofauti kidogo. Hii imeonyesha kwamba Joseph Kabila alisoma dar lakini ile ya mwanzo haikusema hivyo ilisema kwamba alisoma Rwanda. Ukweli ni kwamba Joseph alisoma Zanaki (Jioni ama Taasisi). Lakini pia najua kwamba mama yake Kabila ni huyu Sifa kama habari ya mwanzo ilivyosema ila hii ya sasa inaonyesha mama wa kabila siyo Sifa. Ukweli ni kwamba mama wa Joseph ni Sifa na walikuwa wakiishi wote jijini Dar.
Habari nyingine zinashabihiana. Huenda kweli Joseph si Kabila!

Mambo magumu kweli. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Mzee Kabila alisaidiwa na Watutsi kuingia madarakani. Watutsi wakiwa na dhana yao ya bahima empire walikuwa na mpango wa kumtumia kabila na kisha kimtupa na wao kuchukua utawala kwa kupitia watu kama Joseph, Kabarebe ama Bizima Karaha (aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Mzee Kabila). Kumbukumbu pia zipo kwamba baada ya kuchukua madaraka mzee kabila alishtukia mpango wa watutsi na kuamua kuwafukuza na hapo ndipo umauti ukamkuta na Joseph kuchukua madaraka kutimiza mpango wa watutsi. Huenda kuna kaukweli kuwa Joseph ana damu ya.Kitutsi.

Mkuu Joseph sio damu ya Kabila na historia ya yeye kuishi na kusoma bongo ni ya kweli . Pia ameshawahi kujichanganya mara mbili katika Interview ya BBC na ALJAZEERA Kuhusu maisha yake ya ujana . Pia wafaransa hawamtaki Joseph coz ana Idiology za Kimarekani zaidi ya za kifaransa . Soon aibu kubwa itamfika bwana Joseph ,nilikuwa na baazi ya wakongo wansema wazi hali ni tete kuhusu yeye kuwa raisi wa kongo ili hali si mkongomani.

Kuhusu pacha wake (dada yake ) taarifa ni kwmba bado yupo Dar na ana kampuni kubwa sana ya kusafirisha mizigo kutoka Dar kwenda Central Africa .
 
habari kama hii iliishatoka kwenye gazeti la raia mwema? sema wa tz (kama wakenya wanavyotuita) hatusomiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!

Ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kununua magazeti? Pia una uhakika kila sehemu ya Tanzania magazeti yanafika? Mfano mie hapa Chala ninaweza kukaa mwezi sijaona gazeti lolote la kiswahili zaidi ya haya ya Kichina na Kijapani ya kufungia maandazi so please dont judge wrong mtoa mada
 
Mkuu Kim Kardash unajua watu wanadhani kila mtoto ni mtoto, nimesoma hiyo post ya kwanza nimecheka tu. Nimefurahi kuwa umeweka na apicha ili watu wajue kuwa hapa JF si rahisi kudanganya watu.

Mkuu naona Kim Kardash ana a treasure trove ya picha za famila ya Kabila Sr., can he come clean and tell us why is conveniently avoiding kutuonyesha picha ya Adrien Christopher Kanambe!

Watu siyo wajinga kihivyo, tuonyeshe picha ya Kanambe ili wana JF wa draw their own conclusion; tukisha ona picha hiyo sina shaka itamaliza utata uliopo.

Kumbuka Kabila Sr hakuwa peke yake wakati akipigana vita vya msituni against Mobutu, alikuwa anashirikiana na Wacongomani, Watutsi nk - Mzee Kabila alikuwa na mkewe, vile vile Adrien Kanambe naye alikuwa na mkewe i.e familia ya Mzee Kabila Sr na familia ya Kanambe walikuwa wanaishi KAMBI moja huko misituni.

Mimi niliwahi kusoma somewhere na hata hapa wanajeshi Wacongomani wanesema kilicho tokea kwa Kanambe baada ya kikosi alichokuwa anaongoza kupigwa vibaya sana na majeshi ya MOBUTU, tukio hilo lilimkasilisha sana Kabila Sr. akatoa amri kwamba Kanambe atoswe ndani ya ziwa Tanganyika. Swali ni: Je, nini kiliwasibu familia ya Kanambe baada ya yeye kuuwawa? Ninaposema familia nina maana ya Mkewe Kanambe na watoto wake wawili kama sikosei?

The CRUX of the matter here is one "Adrien Christopher Kanambe" na uhusiano na familia ya the late Kabila Sr. ya sasa hivi; tusijaribu ku-derail mambo hapa.
 
Na kule Danganyika nako utasikia Chenkapa alikuwa mmakonde na huyu raisi wa Tiefutiefu inasemekana ni nasaba za kina Kagame!!

Historia nzuri zaidi ni ya raisi Mwinyi kuwa raisi wa Zanzibar na mapinduzi ya zanzibar kuongozwa na Okelo!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom