Rais Joseph Kabila Mashakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Joseph Kabila Mashakani

Discussion in 'International Forum' started by Martinez, Jan 8, 2012.

 1. M

  Martinez JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  [FONT=&amp]Rais wa Congo DRC Joseph Kabila[/FONT][FONT=&amp] ana wakati mgumu na wa mashaka kufuatia matukio kadhaa yanayoendelea within his perimeters. Ukiachia matukio kadhaa ya kujaribu kumuua kama lile la February 27, 2011 ambapo alijeruhiwa lakini ikafanywa siri, hivi sasa ameongeza maadui baada ya rafu za uchaguzi. Ulinzi wa Kabila unafanywa na Wanajeshi wa Rwanda na usalama wake ukiratibiwa na Jenerali James Kabarebe, waziri wa Ulinzi wa Rwanda. Wakongomani wanaompinga wana sababu ya msingi. Utata wa historia yake. Yeye si raia wa DRC, wala si mtoto wa Kabila, bali ni kibaraka wa Kagame. “pot aux roses” kama wasemavyo wafaransa. Mambo yaliyokuwa sirini sasa yanabainika[/FONT]
  [FONT=&amp]Utata wa historia yake unatokana na uthibitisho wa kustaajabisha uliotolewa na unaoendelea kutolewa na watu walio karibu na historia yake kwamba Joseph Kabila hakuwa na undugu wowote na Marehemu Laurent Kabila, ni mtutsi wa Rwanda, hana uraia wa Kongo DRC na Jina analotumia sio halisi.[/FONT] [FONT=&amp]Simulizi na shuhuda mbalimbali zimekuwa zikitolewa na watu waliokuwa karibu na familia ya Baba yake wa kufikia Laurent Kabila, na Baba yake halisi Adrien Christopher Kanambe kuhusu historia sahihi ya Rais huyo wa Congo DRC.[/FONT] [FONT=&amp]Inasemekana kuwa, jina halisi la Rais Joseph Kabila ni Hippolyte Adrien Christopher Kanambe aliyezaliwa na pacha wake Janet Adrien Christopher Kanambe mnamo June 4, 1971 nchini Rwanda kwa Baba Mtutsi aliyeitwa Adrien Christopher Kanambe, na Mama Mtutsi aliyeitwa Marceline Makumbukuje. [/FONT] [FONT=&amp]Adrien Christopher Kanambe, baba wa mapacha Hippolite na Janet, kama ilivyokuwa kwa Watutsi wengine, alikuwa mpinzani mkubwa wa serikali ya Rwanda iliyokuwa ikiongozwa na Rais Juvenal Habyarimana aliyekuwa Mhutu na hivyo alikuwa akiendesha harakati za uasi akiwa na kundi lake la waasi katika milima ya Manyema mpakani mwa Congo DRC (Zaire) na Rwanda. [/FONT] [FONT=&amp]Laurent Kabila kwa upande wa pili naye alikuwa akiendesha harakati za kuiondoa madarakani serikali ya Mobutu Sese Seko hata alipokutana na Christopher Kanambe katika milima hiyo ya mpakani na wakaunganisha nguvu dhidi ya maadui zao wakubwa Mobutu na Habyarimana. Waliingia mkataba kuwa waunganishe nguvu kumuondoa Mobutu, na baada ya hapo kwa umoja huo huo wamuondoe Habyarimana.[/FONT] [FONT=&amp]Katika umoja wao, Laurent Kabila alikuwa ndiye mkuu wa umoja huo ambapo Adrien Christopher Kanambe alikuwa mkuu wa Jeshi la Watutsi, na Jenerali Kaliste Majaliwa alikuwa mkuu wa Jeshi la Wakongomani. Kwa pamoja waliunda kundi lililoitwa PRP ([/FONT][FONT=&amp]Party of the Peoples' Revolution)[/FONT][FONT=&amp]ambalo makao yake yalikuwa Wimbi mashariki ya Congo.[/FONT] [FONT=&amp]Mnamo mwaka 1984, PRP waliaandaa mpango kabambe wa kuuteka mji muhimu wa Moba ambao ulikuwa unashikiliwa na majeshi ya Mobutu. Kanambe alipewa jukumu la kuongoza operesheni hiyo. Hata hivyo majeshi ya Mobutu yalikuwa na nguvu zaidi na kuwasambaratisha majeshi ya PRP yaliyoongozwa na Kanambe. Waasi wengi walikufa katika operesheni hiyo na Kanambe mwenyewe kujeruhiwa.[/FONT] [FONT=&amp] Kabila (Laurent Kabila) akiwa Wimbi alimtuhumu Kanambe kwa usaliti uliopelekea shambulio hilo kushindwa. Hivyo Kabila aliuamuru Kanambe auawe na kutoswa ziwani. Kanambe akitokea Moba alipokewa na wakongomani waasi wachache, bila kujua kinachoendelea, walitumia Boti kuelekea Wimbi ilipokuwa ngome yao kuu. Wenzake hao walimuua na kumtosa ziwa Tanganyika kama ilivyoamriwa na ndio ulikuwa mwisho wa Adrien Christopher Kanambe. Mbali ya kumtuhumu kwa uasi, lakini pia kuna madai kuwa Kabila aliamua kumuua Kanambe ili amuoe mkewe Marcelina ambaye walikuwa na mahusiano ya siri. Hippolite na Janet walikuwa na umri wa miaka 13 wakati baba yao anauawa.[/FONT] [FONT=&amp]Baada ya hapo Kabila aliwachukua Marcelina (mjane wa Marehemu Kanambe), Hippolite na Janet na kuwapeleka Dar es Salaam ambapo aliwatafutia nyumba maeneo ya Masaki. [/FONT] [FONT=&amp]Hippolite Kanambe (Joseph Kabila) na Janet waliendelea na elimu yake Msingi hadi Sekondari Dar es Salaam wakiwa wanajulikana kwa majina ya Hippolite na Janet Kanambe. Shule ya msingi walisoma Lumumba Primary School na Shule ya Sekondari walisoma Zanaki, Hippolite akiwa mvulana pekee. Pia miaka ya 1992/93 walihudhuria mafunzo ya awali ya Kijeshi JKT Makutupora.[/FONT] [FONT=&amp]Kabila alikuwa na wake wapatao 12, na watoto wengi. Kutokana na harakati zake za kumngoa Mobutu, Kabila hakuzikumbuka sana familia zake na hivyo Hippolite (Joseph) alilazimika wakati mwingine kufanya vibarua katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ili kuweza kuitunza familia. Inasemekana alifanya ya Taxi driver na biashara ndogondogo. [/FONT] [FONT=&amp]Mwaka 1995 Hippolite Kanambe aliamua kwenda kwao Rwanda kujaribu maisha huko, alifikia kwa mjomba wake Kanali James Kabarebe ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ulinzi wa Rwanda, na ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Usalama katika Jeshi la APR. Kabarebe alimtumia Hippolite katika shughuli zake mbalimbali na pia kama dereva wake binafsi. Mwaka 1996 alimuingiza Jeshini na baada ya mafunzo alipangiwa Division maalum aliyohusika na operesheni za Zaire ya Mobutu.[/FONT] [FONT=&amp]Mwaka huo huo 1996 nchi za Rwanda, Burundi, Angola, Uganda na waasi wa Sudani Kusini ziliunganisha nguvu na kuunda umoja ulioitwa AFDL au ADFLC (Alliance of Democratic Forces for the Liberation of Congo-Zaire) kwa ajili ya kumsaidia Kabila na PRP yake kumngoa madarakani Mobutu.[/FONT] [FONT=&amp] Kabila alikuwa ndiye Mkuu wa operesheni za AFDL ambapo Kabarebe (Mkuu wa Usalama Jeshi la Rwanda na Mjomba wa Hippolite) , alikuwa mshauri Mkuu wa Kabila wa masuala ya kivita. Ni wakati huu ambapo Kabila alimuita Hippolite na kumteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Watoto (Kadogos). Katika Jeshi la Kadogos alijulikana kama Major Hyppo. Baadaye, kwa ushauri wa Kabarebe, kwa lengo maalum, Kabila aliamua kumtambulisha Hippolite kama mtoto wake na kumpa jina la Joseph ( Joseph Kabila). [/FONT] [FONT=&amp]Baada ya kumgoa Mobutu madarakani mnamo mwaka 1997 na Kabila kuwa Rais wa Congo, alimteua Kabarebe kuwa Mkuu wa Majeshi na pia alimpeleka Kabila China kwa ajili ya Mafunzo ya Kijeshi kwa muda wa miezi miwili. Hata hivyo, Kabarebe hakukaa sana na madaraka yake hayo kwani kulitokea uvumi kuwa ana mpango wa kumpindua Kabila na pia Wakongomani walilalamikia nchi yao kuvamiwa na Wanyarwanda. Kutokana na sakata hilo Kabila aliamua kumuondoa Kabarebe ambaye alirejea kwao Rwanda. [/FONT] [FONT=&amp]Baada ya kurejea kutoka mafunzoni China, Joseph Kabila (Hippolite Kanambe) aliteuliwa kuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la DRC. Aidha, alikuwa ndiye mshauri na mtu wa karibu aliyeaminiwa sana na Mzee Kabila. Pia alikuwa na mamlaka na sauti kuliko kiongozi mwingine yeyote, na alikubalika kwa maamuzi yake mazuri na kwa kujali maslahi ya wanajeshi na watendaji wengineo. [/FONT] [FONT=&amp]Kabila alimtelekeza Marcelina (Mjane wa Adrien Christopher Kanambe) ambaye wakati kwa wakati huo alikuwa akiishi Rwanda. Aliingia Ikulu akiwa na mkewe Sifa Mahaya. Mnamo mwishoni mwa Oktoba, 2000 Kabila aliwekewa sumu kwenye Chakula na kunusurika kifo baada ya kuwahishwa hospitali. Uchunguzi uliofanywa na Idara ya Ulinzi wa Rais ulimhusisha moja kwa moja mkewe Sifa. Mzee Kabila aliamuru Sifa awekwe Jela wakati uchunguzi unaendelea. [/FONT] [FONT=&amp]Mchana wa tarehe 16 Januari 2001, Mzee Kabila aliuawa kwa kupigwa risasi na Askari mtoto aliyeitwa Rashisi Kasereka (Kadogos !) aliyekuwa mlinzi wake ambaye naye aliuawa kwa kupigwa risasi na askari aliyekuwepo katika tukio hilo. Sifa ambaye muda wote iliaminika kuwa yupo Jela, alionekana akiwa na Joseph katika mazishi ya Mzee Kabila. [/FONT] [FONT=&amp]Baada ya kuuawa kwa Laurent Kabila mnamo 2001, Joseph Kabila alichukua madaraka ya Urais wa mpito. Katika uchaguzi wa Rais wa 2006 aligombea na kushinda na amekuwa Rais wa DRC mpaka hivi sasa. Miaka zaidi ya 10 imepita tangu “Baba yake” auawe. Hata hivyo Rais Joseph Kabila amekuwa akipinga pendekezo lolote la kuendeleza uchunguzi wa kifo hicho japokuwa watu zaidi ya 50 wamewekwa kizuizini bila mashtaka kuhusiana na mauaji hayo. [/FONT] [FONT=&amp]Katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari, Kabila iliwahi kuulizwa na Mwandishi wa France 24, Arnaud Zajtman kuhusu suala hilo. Ambapo alijibu “Mara kadhaa nimemjibu kuhusu suala hilo, na leo jibu langu ni lilelile. Makosa yaliyofanyika wakati wa kipindi cha mpito ni kudhani kuwa tunaweza kufikia maelewano bila mahakama.”[/FONT] [FONT=&amp]Viongozi wa dini mbalimbali na wapigania haki za binadamu wamekuwa wakishinikiza kufanyika kwa uchunguzi ili wauaji wajulikane na sheria ichukue mkondo wake, na hao ambao wamewekwa kizuizini pengine bila hatia waweze kuachiwa huru.[/FONT] [FONT=&amp][/FONT]
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu thank you for input,ccm wanaogopa sana wakisikia hizo taarifa
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  dah mkuu thanks kwa information hizo sasa huyo pacha wake atakuwa wapi sasa hivi
   
 4. B

  Bijou JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  habari kama hii iliishatoka kwenye gazeti la raia mwema? sema wa tz (kama wakenya wanavyotuita) hatusomiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nditi please edit adress ya attachment yako!
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aksante
  nasubiri Kabila aje kutoa ufafanuz
   
 7. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dah!! si mchezo kaka, asante kwa taharifa.
  Mtu anayefahamu hali jinsi ilivyo pale DRC atujuze, nasikia jeshi limegawanyika, wapo wanaomtii Rais halali Tshisekedi na wapo wanaomtii Rais wa tume Joseph Kabila.
  Wenye taharifa zaidi ya hali jinsi ilvyo DRC watujuze hapa
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hata mwanaHALISI nadhan
   
 9. N

  Nguto JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,650
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Yes hata mimi nilishaisoma. Nashangaa wa congo wako kimya!! Kulikoni?
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani hata humu imekuwemo tena nadhani mwezi uliopita kama si mwezi huu. Niliisoma ila ina tofauti kidogo. Hii imeonyesha kwamba Joseph Kabila alisoma dar lakini ile ya mwanzo haikusema hivyo ilisema kwamba alisoma Rwanda. Ukweli ni kwamba Joseph alisoma Zanaki (Jioni ama Taasisi). Lakini pia najua kwamba mama yake Kabila ni huyu Sifa kama habari ya mwanzo ilivyosema ila hii ya sasa inaonyesha mama wa kabila siyo Sifa. Ukweli ni kwamba mama wa Joseph ni Sifa na walikuwa wakiishi wote jijini Dar.
  Habari nyingine zinashabihiana. Huenda kweli Joseph si Kabila!

  Mambo magumu kweli. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Mzee Kabila alisaidiwa na Watutsi kuingia madarakani. Watutsi wakiwa na dhana yao ya bahima empire walikuwa na mpango wa kumtumia kabila na kisha kimtupa na wao kuchukua utawala kwa kupitia watu kama Joseph, Kabarebe ama Bizima Karaha (aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Mzee Kabila). Kumbukumbu pia zipo kwamba baada ya kuchukua madaraka mzee kabila alishtukia mpango wa watutsi na kuamua kuwafukuza na hapo ndipo umauti ukamkuta na Joseph kuchukua madaraka kutimiza mpango wa watutsi. Huenda kuna kaukweli kuwa Joseph ana damu ya.Kitutsi.
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu, unataka kuwahi pacha wa rais wa DRC?
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  dah! Yaelekea hypo alitonywa kuwa mzee adrien aliuawa na mzee kabila hivyo akamuagiza kadogos kwenda kummaliza
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Ok Nimeipenda ila ukitaka kupata uhondo zaidi wa story hii kwa picha ingia kwene Youtube utafuta kwa mojawapo ya title hizi; Murder in Kinshasa au hii hapa Who Killed Kabila? Utapata bonge la documentary hadi raha! Thanks, mimi nilii-download waweza PM ili nikuelekeze na wewe uone shuhuda za ajabu!!!
   
 14. m

  matendo Member

  #14
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna raha gani kung'ang'ania madaraka na hali wananchi hawakutaki na maisha yako yako matatani?.
   
 15. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Anaishi Masaki na anamiliki kampuni ya kusafirisha mizigo kwenda huko huko kwa kaka yake! Ngapi ngapi za kubadilishia mavogue anazo sio kidogo!
   
 16. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Very truu nilishaga iona, nadhani imeandaliwa na aljazeera kama sikosei, ina kama dakika 45 hivi, imetulia sana. Kuna watu wanaozea jera bila hatia wakati wengine wako ubelgiji wanaponda raha na ndio wahusika. Anyway that is devoloping Africa!
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Anaishi kwenye nyumba ya Joseph!
   
 18. m

  matendo Member

  #18
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anafamilia masaki au yuko alone?
   
 19. m

  matendo Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mdada yuko na family au anaishi alone?
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ukiangalia hii documentary ya al jazeera utapata mwanga wa kifo cha kabila

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...