Na huu ndio ukweli niko na mtu yuko Bandarini kitengo ananiambia hii ishu itachukua heading DuniA Nzima.. Rais magufuli ni noma asee ndo maana mafisadi wanatumia kila njia kutoa watu kwenye direction. Story nyingi za kujaza junks kichwani. Pumbafu Sana wale wote wasiotakia Mema hii nchi.. Go magufuli go Bravo magufuli.. Ifanye tanzania kuwa taifa la mfano DuniA Nzima
Nani akamdanganye Makonda?!Kamdanganye Makonda
Hivi kuna watu wanaamini yaliyotokea bandarini jana ni kweli?
Mwenyezi Mungu alipumzika siku ya saba. Mwanadamu akaona ni muhimu kuwa na mapumziko pia. Shuleni baada ya vipindi kadhaa kunakuwa na pumziko na kunakuwa na likizo baada ya nusu muhula na mwisho wa muhula. Kazini pia kunakuwa na likizo.
Tusipotumia vipindi vya mapumziko kwa makusudio yake akili huchoka mapema. Tusitarajie mapya toka kwa mtu asiyekuwa na likizo.
Ukikua utapata uwezo wa kuzielewa threads za watu wazima; but nice try!!!
Kwahiyo issue ya Clouds na Makonda ndio serious issue....nyingine sio issue.???Hana jipya huyu kila siku kulialia na kulalamika, sasa anamlalamikia nani ikiwa ana mamlaka yote?!! Tunataka uchumi upande na uonekane moja kwa moja kwa wananchi kuwa unapanda na siyo takwimu uchwara tu za kwenye makaratasi. Kama hawezi kazi apishe wenye uwezo wa kuongoza nchi waitumikie.
Rais anatetea jambazi mvamizi na fisadi wa elimu halafu bado mnaleta ngonjera za kumpigia makofi na kumshangilia mtu wa namna hii!!! Huyu kwa nchi yenye watu waliostaarika hakupaswa hata kuwa kiongozi wa mtaa.
Kama ni kweli kwa nini yasingefunguliwa leo (jana)?
MY TAKE:
Namshauri Rais wangu apeleke kikosi cha JWTZ chenye silaha mzito pale bandarini!! Aidha, ahakikishe kunakuwa na helikopta za kijeshi zitakazokuwa zinarandaranda eneo la tukio manake asipofanya hivi; siku akirudi tena kwenda kuyafungua, atakuta mabonge ya dhahabu yote yametolewa na kubaki mchanga peke yake!!!!
Mkuu ukiniuliza mimi utakuwa unanionea!!!!Kama ni kweli kwa nini yasingefunguliwa leo (jana)?
Rais wetu kipenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, jana alifanya yale ambayo huwa anayapatia kweli kweli!!
Kwa kutumia umahiri mkubwa kabisa, bila shaka aki-apply mbinu za kijeshi alizowahi kujifunza JKT, Mheshimiwa Magufuli aliingia bandarini kwa kushitukiza hali iliyowafanya watu wa pale wapigwe butwaa huku wengine mioyo yao ikipiga mkamba kwa sababu hawakutarajia kutokea Mheshimiwa huyo!!!
Mbinu hizi za kijeshi, na bila shaka zikichanganyika na mbinu za kijasusi; zilimwezesha Mheshimiwa Rais wetu aweze kukamata makontena kadhaa yaliyojaa dhahabu!!!
Huku akionekana kujawa na uchungu dhidi ya nchi yake, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alisema:
Video kwa Hisani ya Comrade William John Malecela. a.k.a Mzee wa Totoz!!!Mnyetishaji wangu aliwahi kunitumia meseji kuhusu kilichokuwa kinaendelea bandarini na akaniambia wazi kwamba; "...Ndugu yangu chige, kama noma na iwe noma lakini leo ama nipate utajiri kwa kupora donge la dhahabu au nile shaba wakati na-test zari!" Akamalizia kwa kizungu kwamba eti "get rich or die trying!"
Ingawaje mimi ni mtoto wa askari niliyekulia kwenye kota za askari na hivyo nimeanza kuziona bunduki tangia nikiwa mtoto lakini hadi leo nazeeka bado naziogoa sana bunduki!!! Kauli ya mshikaji wangu kwamba, kama vipi poa tu na hata kama kupigwa shaba yupo tayari ni kauli ambayo ilifanya mapigo yangu ya moyo yakaribie kula pozi!
Niliogopa! Nilitishika! Nikajawa na hofu mithili ya mtu aliyekoswa koswa na gari moshi inayosafiri kwa kasi ya umeme!! Hofu yangu ilikuwa kweupe kiasi cha kuweza kuonekana hata na mtu aliyekuwa meta kadhaa kutoka nilipokuwa nimesimama!!
Mapigo yangu ya moyo nayo yalikuwa yanasikika mubashara mithili ya saa mbozi yenye mishale ya chuma chakavu!!!
Kwakweli sikuwa tayari kumpoteza rafiki yangu akiwa bado kijana, kwahiyo, pasi na kupoteza japo sekunde, hapo hapo nikamvutia waya ili aniambie anamaanisha nini kwa kauli yake ile ya kuogofya!!
Baada ya kumpigia simu; bila hofu aliongea kwa kujiamini kabisa: "...chige, kama nilivyokuambia Mheshimiwa kayaotea makontena yenye nyomi la dhahabu! Na ninavyomfahamu Mheshimiwa, huyu bwana hapendi ujinga kwahiyo lazima ataamuru yafunguliwe!!!"
Kwa mbaaaali nikaanza kumwelewa lakini nikajikausha na kuhoji "...Kwahiyo?"
Kuonesha ameamua akajibu: "... Najua makontena yakifunguliwa lazima madonge ya dhahabu yadondoke!! Yakidondoka tu; lazima nidake moja na kujitosa nalo baharini!"
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu; nami taswira ya utajiri ikaanza kunipitia akilini mwangu!! Nikajikuta nimeganda kimyaaa!! Sitikisiki wala sipepesi hadi jamaa aliponigutua na kuhoji eti nasemaje!!!
Sina hakika kama nilijipa muda wa kufikiria japo mara mbili lakini nilijikuta tu nikiropoka: "...Mwana, golden chance never come twice! Test zari na kama vipi, niandae usafiri kabisa ili ukichomoka tu; tupotee mamoja!"
Kwa bahati mbaya, tofauti na mshikaji wangu alivyotaraajia kwamba makontena yaliyojaa dhahabu yatafunguliwa; yakaenda kufunguliwa makontena mengine yenye madudu gani sijui!!!
Sijui ni kwamba funguo za kufungulia makontena yaliyojaa dhahabu zimepotea au vipi!!!
MY TAKE:
Namshauri Rais wangu apeleke kikosi cha JWTZ chenye silaha mzito pale bandarini!! Aidha, ahakikishe kunakuwa na helikopta za kijeshi zitakazokuwa zinarandaranda eneo la tukio manake asipofanya hivi; siku akirudi tena kwenda kuyafungua, atakuta mabonge ya dhahabu yote yametolewa na kubaki mchanga peke yake!!!!