Rais wetu kipenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, jana alifanya yale ambayo huwa anayapatia kweli kweli!!
Kwa kutumia umahiri na ustadi wa hali ya juu! Bila shaka aki-apply mbinu za kijeshi alizojifunza JKT, Mheshimiwa Magufuli aliingia bandarini kwa staili ya kushitukiza! Hilo likawafanya wana-bandari wapigwe butwaa huku wengine mioyo yao ikipiga mkamba; puh!
Hawakutarajia ugeni wa Mheshimiwa!!!
Mbinu hizi za kijeshi, na bila shaka zikijumuisha zile za kijasusi; zilimwezesha Mheshimiwa Rais wetu aweze kukamata makontena kadhaa yaliyojaa dhahabu!!!
Huku akionekana kujawa na uchungu kwa nchi yake, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alisema:
Mnyetishaji wangu akawahi kunitumia meseji kuhusu kilichokuwa kinaendelea bandarini na akaniambia wazi kwamba; "...Ndugu yangu chige, kama noma na iwe noma lakini leo ama nipate utajiri kwa kupora donge la dhahabu au nile shaba wakati na-test zari!"
Akamalizia kwa kizungu kwamba eti "get rich or die trying!"
Ingawaje mimi ni mtoto wa askari niliyekulia kwenye kota za askari na hivyo nimeanza kuziona bunduki tangia nikiwa kinda lakini hadi leo nazeeka bado naziogopa sana bunduki!!!
Ikitokea nimekaa na mtu aliyebeba bunduki, ile akianza kuchezea tu kochoo; kochoo... mi huyoooo naondoka zangu!
Wahenga hawakuwa wajinga walipotutahadhalisha kwa kusema "konkoriko mlango wa chuma, ukiufungua hauna huruma!"
Kwa kufahamu hayo, kauli ya mshikaji wangu ilikosa mvuto, si duniani tu bali hadi akhera! Kwamba, kama vipi poa tu na hata kama kupigwa shaba yupo tayari ni kauli ambayo iliyafanya mapigo ya moyo wangu yakaribie kuketi kwenye sofa!
Nikaogopa na kutishika kweli kweli! Nikajawa na hofu mithili ya mtu aliyekoswa koswa kwa gari moshi inayosafiri kwa kasi ya umeme!!
Mapigo ya moyo wangu nayo yakaanza kusikika... puh! Puh! Mithili ya saa mbovu yenye mishale ya chuma chakavu!!!
Sikuwa tayari kumpoteza swahibu yangu akiwa angali bado kijana. Kwahiyo, kwa kuchelea kupoteza japo sekunde ya ziada, hapo hapo nikamvutia waya ili anitabainishie nini maana ya kwa kauli yake ile ya kuogofya!!
Baada ya kumpigia simu; bila hofu aliongea kwa kujiamini kabisa: "...chige, kama nilivyokuambia Mheshimiwa kayaotea makontena kadhaa yenye lumbesa ya dhahabu! Na ninavyomfahamu Mheshimiwa, huyu bwana hapendi ujinga kwahiyo lazima ataamuru yafunguliwe hapa hapa!!!"
Kwa mbaaaali nikaanza kumwelewa lakini nikajifanyisha ujuha na kuhoji "...Kwahiyo?"
Kuonesha ameamua akajibu: "... Najua makontena yakifunguliwa lazima mijidonge ya dhahabu idondoke!! Ikidondoka tu; lazima nianze nalo moja na kujitosa nalo baharini!"
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu; nami taswira ya utajiri ikaanza kunipitia akilini mwangu!! Tamaa ikanijaa! Harufu ya mavumba ikajaa kwenye pua zangu! Nikauona u-Bakhresa huu unanijia kwa kasi ya mwanga!
Nikajikuta nimeganda kimyaaa!! Sitikisiki wala sijongei!! Macho nayo yalishaachana na kibarua cha kupepesa hadi jamaa aliponigutua na kuhoji eti nasemaje!!!
Sina hakika kama nilijipa muda wa kufikiria japo mara mbili lakini nilijikuta tu nikiropoka: "...Mwana, golden chance never come twice! Test zari na kama vipi, niandae usafiri kabisa ili ukichomoka tu; tupotee mamoja!"
Kwa bahati mbaya, tofauti na mshikaji wangu alivyotaraajia kwamba makontena yaliyojaa dhahabu yangefunguliwa; yakaenda kufunguliwa makontena mengine yenye madudu gani sijui!!! Marapurapu si marapurapu; misulupwete si misulupwete... yaani tafrani!
Sijui ni kwamba funguo za kufungulia makontena yaliyojaa dhahabu zimepotea, au makusudi tu!!!
MY TAKE:
Namshauri Rais wangu apeleke kikosi cha JWTZ chenye silaha mzito mzito kama vile vifaru na mizinga pale bandarini ili kuilinda mikontena iliyojazwa midhahabu yetu!!!
Aidha, ahakikishe kunakuwa na helikopta za kijeshi zitakazokuwa zinarandaranda eneo la tukio manake asipofanya hivi; siku akirudi tena kwenda kuyafungua, atakuta mijidonge yote ya dhahabu imebebwa na kubaki na mchanga peke yake usiofaa hata kwa kutengeneza matofali!!

Maneno siyo yangu abadani... huyu hapa:Kwa taarifa nilizonazo, nikizisema hapa mnaweza mkalia! Dhahabu iliyopo humu ndani! Kwa Mtanzania yeyote anayeipenda Tanzania... atalia! Kwa mali zilizomo humu...!
.

"Akili za mbayuwayu, changanya na zako!"