DOKEZO Rais ingilia kati ubadhirifu katika ujenzi wa jengo la abiria Mwanza Airport

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Busara itumike Ramani ya jengo ipitiwe upya na uchunguzi ufanyike kwa kina hatua zichukuliwe. Picha nenda you tube.
 
Kwa sasa ni wazi kuna hujuma kubwa ya ujenzi ya uwanja wa ndege wa Mwanza. Nimebahatika kupitia pale kama raia na mlipa kodi wa nchi hii na kuangalia ujenzi ulivyo jengo lile ni kiwango cha chini mno kati ya miradi inayoendeshwa na serikali ya awmu ya sita.

Mkuu wa Mkoa Malima alikuwa na haki ya kuvunja kamati hiyo. Jengo hilo ni dogo mno,halikidhi kwa mahitaji ya Mwanza, inazidiwa kwa uzuri na stand ya mabasi ya Nyamhongolo shame to contractors! Serikali ichukulie uzito wa pekee kuhusu jengo hilo la abiria (pax terminal) vinginevyo itaumbuka.

Hivyo nashauri yafuatayo:

Kupanua jengo hilo liendane na hadhi ya kimataifa kwa kubadilisha mchoro na kufumua uchafu wote. Hili sio jengo la abiria ni godown tu, aibu. Rais Samia weka nguvu zako binafsi uache legacy kanda ya ziwa.

Haraka jengo lipewe TAA na watafute mkandarasi mwenye uwezo kufanya marekebisho makubwa kukidhi mahitaji ya kimataifa na siyo kwa utaratibu wa force account, jengo la abiria airport siyo jengo la shule ya msingi au sekondari. Jengo zuri abiria la uwanja ndege ni kivutio pia kimataifa na utalii unaanzia hapo.

Tayari Mwanza ina ushindani na Kisumu kibiashara kikanda huku kwenye eneo la maziwa makuu. Hivyo ,serikali iweke bajeti inayotosheleza kujenga jengo lenye hadhi ya kimataifa Mwanza jiji la pili nchini. Bn 19 hazitoshi labda kwa jengo la soko la wilaya. Inahijika bn 100+ at least ili kupata jengo lenye hadhi ya kimataifa, parking kubwa na nzuri, mitambo ya kisasa na workmanship nzuri ya jengo lenyewe siyo kutuwekea vigae vya sakafu low quality na ngazi za chuma kama godown badala ya kuweka angalau ngazi za chuma za crome. Aibu kubwa.

Mhe. Rais ingilia kati uwanja ubomolewe sehemu kubwa ili kuendana na mahitaji ys intern airport maana hata sehemu ya customs,immigration,afya, security checks na laggage conveyor machines hazitatosha na hakuna transit lounge. Hii hatari!. Katika majengo mapya yaliyowahi kujengwa airport Mwanza. Hilo ndilo la mwisho halilingani na thamani na matarajio ya wananchi
Serikali ilisinzia kidogo kwa hili.

Nchi itajengwa na wazalendo.
Mtu aliyeharibu uwanja huo ni JPM, mkurupukaji na Mzee wa teni pasenti. Bahati mbaya kafa kabla hajaumbuliwa
 
Magufuli hayupo kwa sasa tugange yajayo,taasisi ya Rais ipo serikali ni ile ile ya CCM ipo,Ilani ni ileile. Tusiruhusu makosa yaliyotokea kwenye jengo hili yaendelee sasa hivi ni awamu nyingine. Yarekebishwe kwa maslahi ya Taifa. Jengo hili TAA walipitie upya hii ni aibu!
 
Bonge la point. Hata mimi theory hii ya kutopenda uwanja wa Mwanza ili kuupendelea wa Chato ilinipita pembeni.
Hiki ni kiwango kikubwa sana cha ubinafsi alichokuwa nacho jiwe, ni aibu kubwa.
Anyway, limeshatokea hilo basi mimi nadhani jambo moja lingefanyika nalo ni kuhamisha Kamandi ya jeshi la anga Mwanza na kuipeleka Chato wautumie ule uwanja usikae bure tuu maana kuutumia kibiashara ni hasara wanaweza kutumia Bukoba.
Kisha nguvu mpya ikawekwa hapo Mwanza na kuacha tabia za kuingiza siasa humo. Maana ki mara kadhaa tumesikia eti kamati ya siasa ya CCM, mara mwenyekiti wa CCM na katibu wanatembelea utekelezaji wa mradi na KUPONGEZA kumbe hakuna la maana linaendelea.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Uedanganywa nawe ukadanganyika.

Mpango wa JPM ulikuwa kuvijenga viwanaj vya ndege kila mkoa. Chato inachukua nafai ya geita na sio mwanza.

Ungeongelea kuhusu uwanja wa geita na chato lambda.

Uwanja wa Mwanza uliachwa kwenye hari nzuri ya ujenzi. lambda wewe ni mgeni kwa mwanza.
 
Msikilize mkuu wa mkoa RC Adam Malima alipotembela airport hivi karibuni ujue hali ya ufisadi kwenye jengo hilo na sub standards zake ndipo utajua nini watu wanasema, acheni kutetea uozo.
 
Msikilize mkuu wa mkoa RC Adam Malima alipotembela airport hivi karibuni ujue hali ya ufisadi kwenye jengo hilo na sub standards zake ndipo utajua nini watu wanasema, acheni kutetea uozo.
Huyu Malima ndio kaja kuharibu kabisa kwa kujifanya financial advisor, mkuu wa mkoa aliyekuwepo alikuwa amefikia hatua nzuri ya kukabidhi Taa, ila huyu financial advisor Toka amekuja hakuna analofanya mwanza.
Kama kuna ubadhirifu si watu wakamatwe?
 
Nchi itajengwa na wazalendo.
Mimi husema hivi, kwenye maswala kama haya, watendaji wanapokosa aibu kabisa kuvuruga kazi za waTanzania, kuna sababu zipi za kuendelea kuwapa heshima hawa watu?

Hilo jengo katika mipango ya ujenzi wake wote, ni lazima kuna watu wanaojulikana kuisimamia hiyo kazi toka mwanzo hadi mwisho, na ni hawahawa watu, au baadhi yao wanaovuruga kazi hiyo, tena kwa kiburi na kujua hawatafanywa lolote na yeyote.

SKwa hiyo mimi nasema hivi, ni wakati mwafaka wa kutafuta njia za kupambana na hawa wahuni, hata kwa njia zisizo rasmi.
Hawa watu wana majina, na wana vyeo. Unapokuja hapa JF na kulialia kijumla tu namna hii inatia masikitiko kwetu sote.
Inabidi sasa pawepo na utaratibu wa kuwataja waziwazi hawa watu, jamii iwatambue na kuwajua. Kuna njia nyingi sana za kutaja na watu wakajua ni akina nani hawa wanaotuvuruga na kutukwamisha katika juhudi zetu za kutafuta maendeleo.

Hata kama hawwafikishwi mahakamani, kuwataja hadharani ni sawa na kuwafikisha kwenye mahakama ya umma.
 
Back
Top Bottom