Rais huwa hatangazi Utalii

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Kwa mara ya kwanza Dunia inaenda kushuhudia mkuu wa nchi, Rais akitangaza utalii. Rais anapoamua kutangaza utalii maana yake ni kwamba hilo Taifa analoongoza ni Taifa mfu, ni Taifa lililokufa, ni taifa jipya kabisa chini ya jua na halina raslimali zozote na wala kitu chochote, sasa inabidi atoke mkuu wa nchi aifahamishe Dunia kuwa taifa analoongoza lina sehemu za utalii.

Na Kwanza hata kama taifa halina chochote, siyo kazi ya Rais kutangaza utalii. Zipo strategies za kutangaza utalii, Samatta ni maarufu Duniani kuliko Rais Samia.

Rais anapoenda Location kama msanii wa Bongo movie kutangaza utalii,huo mkosi mzito mno kwa taifa, watalii hawaji Tanzania eti kwa sababu Rais aliwatangazia.

Wanakuja kwa sababu usalama wao utakuwa mkubwa zaidi, huwezi kwenda kutalii kwenye Taifa ambalo kiongozi mkuu wa Chama kikubwa Cha Upinzani ni Gaidi, maana yake ni kwamba hata mawaziri nao ni magaidi.

Kenya inapokea maelfu ya watalii kwa mwaka kuliko Tanzania nani alimwona Rais wa Kenya akienda location kutangaza utalii?
Yaani Serikali nzima yenye wasomi wa kada zote haina strategies za kutangaza utalii hadi Rais aende location?

Mbona ni rahisi mno kutangaza utalii kuliko ilivyo rahisi kunywa maji? Tanzania hii yenye vivutio vyote leo hata Rwanda wameanza kuwazidi kupokea watalii wengi kwa sababu ya strategies.

Rais ataenda Location zote na mtatengeneza filamu zote na watalii hamtawaona kwa sababu hamna strategies.

Nyie strategies zenu ni kuua Upinzani tu haya mengine zero kabisa.
 
Hua najiuliza sana; ni Rais Samia mwenyewe ndiye aliamua kuanza kufika location kwa ajili ya kutangaza utalii? au kuna ushauri alupewa na wasaidizi wake then akakubaliana nacho?

Je, kama watalii watakuja kwasababu ya rais kuboost kutangaza utalii; ni kwanini sasa mawaziri wote wasiende location kwa ajili ya kumsaidia mh Rais kutangaza utalii?

Kwangu mimi bado sijapata sababu rasmi ya kwanini jambo hili linatokea kwenye ardhi ya Tanzania. Hii kitu ipo kwenye bajeti ya Wizara ya Utalii? au ipo kwenye ratiba zote za Ikulu?

Je, gharama za kwenda hizo location kutangaza utalii zinalipwa na ofisi ipi.
 
Kuna Uzi wangu mrefu kuhusu hiki ulichokiandika hapa nilikuja nao mapema tu Wiki hii na Kuhoji hadi Kushangaa pia, ila kwa Masikitiko makubwa Moderators Wakauunganisha kwasababu wanazozijua Wao ambazo naziheshimu.

Ninakubaliana 100% kwa hizi Hoja zako.
Tatizo mmejaa ushamba wa Chato! Kwani Samia ndo Rais wa kwanza Duniani kufanya Royal Tour?

Tatizo mmejaa ushamba na mnaonesha wazi wazi mlivyo washamba
 
Raisi ni nembo ya Taifa, sio vibaya, mataifa yatataka kujua huyu raisi mwanamke ni nani huko Afrika Mashariki. Big up Mama.
 
Hapo ndipo utajua kuwa demokrasia yetu imepokwa. Kuna watu maarufu kwa mengi tu hata kwa weledi wa lugha za kimataifa tulitegemea hawa wazunguke nchi nzima kwa gharama nafuu kabisa kuliko hii misafara mufilisi na ving’ora tunavyoona sasa kisa kumrekodi bibi kizee kwenye filamu eti za kutangaza vivutio vyetu!

Kwanini msitumie jeshi la polisi kushurutisha watalii kuja nchini? Na hao watalii wakija basi muwawekee tozo za nywele zao.
 
Kwa mara ya kwanza Dunia inaenda kushuhudia mkuu wa nchi, Rais akitangaza utalii.
Rais anapoamua kutangaza utalii maana yake ni kwamba hilo Taifa analoongoza,ni Taifa mfu,ni Taifa lililokufa,ni taifa jipya kabisa chini ya jua,na halina raslimali zozote na wala kitu chochote,sasa inabidi atoke mkuu wa nchi aifahamishe Dunia kuwa taifa analoongoza lina sehemu za utalii
uhuru wa kuwaza bila kufikiri
 
Back
Top Bottom