Rais Dkt. Magufuli, Je unayajua ya uliempandisha cheo jeshi la Magereza? Mtumie kuondoa bajeti ya kulisha wafungwa

Simabwachi

JF-Expert Member
Mar 31, 2017
306
394
Juzi nikiwa Kibiti mkoani Pwani katika safari zangu za kutafuta mashamba nilibahatika kukutana na rafiki yangu niliekuwa nae Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na baadae kupata ajira ya kudumu ktk Jeshi la Magereza namimi kurudi mtaani. Katika mazungumzo yetu ya hapa na pale askari huyo alieacha kazi ktk Jeshi hilo alisikitika sana namna baadhi ya viongozi wa Jeshi hilo wanavyofanya mazingira ya kufanyia kazi kuwa magumu. Katika kilio chake rafiki yangu huyo alimalizia na kauli/sala/dua moja iliyonipelekea kuanzisha uzi huu, alisema "anatamani viongozi wote wa Jeshi la Magereza wawe kama SACP J. S. BUKUKU ( Mkuu wa Viwanda Msaidizi- Magereza Tanzania)-ktk utendaji wao"

Anasema kila mahali alipopita Afande Bukuku aliwacha alama njema zisizofutika sio tuu kwa askari aliokuwa akiwaongoza bali hata raia. Baadhi ya alama zilizowekwa na ACP Bukuku baadhi ya maeneo alipoongoza:-

01. Aliwahamasisha askari kujiendeleza kielimu, na alipitisha barua zao za maombi ya kwenda kusoma bila ya usumbufu wowote; hii ilisaidia askari wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa na askari wengi waliokuwa masomoni kuliko mikoa yote ya Tanzania kwa kipindi cha uongozi wake.

02. Alijenga nyumba 4 za kisasa zenye uwezo wa kuishi askari 64 na familia zao bila ya kuchangisha ata shilingi moja toka kwa askari. Bukuku alitumia rasilimali miti kwenye mapori mbalimbali na kutengeneza mbao zilizotumika kutengeneza nyumba hizi, n.k

03. Nje ya makazi ya askari: Aliomba eneo lililokua likimilikiwa na machine tools moshi ili litumiwe kwa ajili ya kilimo na askari wake, Bukuku alimgawia kila askari alietaka kulima. Askari walikuwa wakilitumia kwa kilimo tuu ili kuondoa pori, umiliki bado ulikuwa kwa machine tools.

04. Ndani ya makazi ya skari: Aligawa eneo la nusu hekari mpk hekari moja kwa maafisa na askari kwa ajili ya kulima mboga mboga na mahindi ya chakula (eneo hili maji hupatikana mda wote kwa mwaka)-alihimiza kilimo cha umwagiliaji.

05. Alilima migomba, ambayo ilizaa ndizi nzuri zilizouzwa kwa maafisa na askari ambapo mkungu mmoja uliuzwa kati ya shilingi 1,500 mpk 5000 kutegemeana na ukubwa wa mkungu. Hili lilisaidia kupunguza ukali wa maisha kwa askari wa mkoa huo.

06. Aliweza kuwapa askari wote nafasi ya kuangalia channel zote za DSTV kwa kuchangia shilingi 1000 tuu kwa mwezi; hili lilisaidia askari kutulia majumbani mwao wakati wa ligi za Ulaya na mipira mbalimbali, na vilevile kina mama majumbani kuburudika na channel mbalimbali za tamthilia n.k

07. Aliweka TV na kuziunganisha na DSTV sehemu za wahukumiwaji na mahabusu. Hivyo wafungwa waliweza kuangalia habari zinazoendelea nchini na duniani.

08. Alijenga rest house ambayo ilikuwa ikitumiwa na askari wote wa Tanzania waliokuwa wakija Kilimanjaro ama kikazi, likizo, au wagonjwa au wanawagonjwa hospitali ya KCMC. Askari hao walikua wanalala pasipo malipo yoyote kwa siku zote utakazokuwepo. Hii taarifa ilisambazwa kwa maafisa na askari wote Tanzania.

09. Alihimiza maendeleo, kujiwekea akiba, na kujiunga katika SACCOS

10. Kubwa zaidi anasema Bukuku hakuwa tayari kuona askari hapandi cheo au anafukuzwa kazi kutokana na offence ambazo hazikua na mashiko kama kupotelewa na mfungwa, na baadae kupatikana.

Bukuku alifanya hayo ata alipohamishiwa Jiji la Dar es Salaam ambapo hakukaa sana, na baadae kuhamishiwa Jiji la Tanga, na sasa ni Mkuu wa Viwanda-Msaidizi Tanzania.

Aliendelea na kusema sio mikoani tuu bali ata makao makuu bado Bukuku anaonyesha utofauti, akatoa mfano mmoja kuwa Bukuku alitengeneza lift ya ghorofa kwa pesa yake ya mfukoni, lifti hiyo ilikuwa imekaa zaidi ya miezi 9 bila kutumika kwa kutokukarabatiwa anasema hizo ni sifa anazozipata kwa watu wa pembeni

Pamoja na yote hayo mpashaji habari wangu huyo alisema anahisi maendeleo ya Bukuku mkoani Kilimanjaro kuna walioyachukia, hii ilipelekea mpaka Afande Aziza Mursali kwenda Moshi na kutoa amri ya kufyekwa kwa hekari zaidi ya 20 za migomba na ndizi zake (MUNGU amlipe huyu afande kadri ya matendo yake). Kilichonishangaza mimi na mpashaji habari wangu ni kutopanda cheo kwa afande Bukuku toka mwaka 2004 mpaka mwezi wa 5, 2017 Rais JPM alipompandisha. Jee, ni kweli majeshini pia kuna kubaniana kama huku Uraiani?? Ni kwanini askari mleta maendeleo kama huyo serikali imeshindwa kumtumia katika kauli yake ya “HAPA KAZI TUU??”

Kwa maoni yangu kama sifa za huyo afande Bukuku ni kweli, nashauri angepewa jukumu la kusimamia mapori yote ambayo hayajaendelezwa Tanzania azalishe kwa kutumia wafungwa na wale vijana ambao hawana pa kula wala pa kulala awaweke makambini wafanye kazi za uzalishaji mazao ya chakula na biashara. Mavuno yatakayopatikana yakalishe wafungwa magerezani na ziada isaidie hao vijana katika kuwapa mitaji ya kuendeleza baadhi ya mashamba kwa manufaa yao na vizazi vyao. Nimesema ivyo kwa sababu ya sifa alizokuwa nazo huyo afande ya kuendeleza mapori yote yaliyokuwa yamekaa bila kulimwa au viwanda kuendelezwa/kujengwa katika mkoa wa Kilimanjaro.

Askari wetu sio watu wa kukosa nyumba za kuishi iwe za kwao binafsi au za kujengewa na serikali..viongozi hawa wangekuwa na maono wasingekosa mapori yaliyotelekezwa na kina Rais mstaafu Mkapa, Mwinyi n.k, Sumaye n.k kutenga na kujenga nyumba za askari wao...ktk mapori hayo wangepata mbao, kuni, na mkaa. Watendaji kazi wanao kuna askari na wafungwa wengi ni mafundi waliobobea ktk ujenzi wa kila namna lkn hawatumiwi, awamu hii tunataka viongozi wanaojiongeza
 
Bukuku yupi? Ni yule aliekua Gereza la Lilungu Mtwara miaka ya 1999 hadi miaka ya 2000? Na alikua na mtoto wake mmoja marehemu wa kike kwa jina la Suma alikufa kwa ajari? Kama ni yeye nitakuja kutoa ya moyoni na mimi kwa kumfahamu kwangu huyu mzee na nitashangaa kwa kweli kama bado hajapewa nyadhifa za juu katika jeshi la Magereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maafisa wengi katika idara nyingi za serikali wana tabia ya kuwabania watu waliochini yao hasa wale wabunifu na wenye uwezo wa kuongoza pengine kwa kuhofia kuhatarisha nafasi zao. Watu kama hawa hupendwa sana na viongozi wa kisiasa kwani huwaona kama mtaji wa kisiasa (wana nafasi kubwa ya kufanya mazuri) hivyo wanasiasa husaidia kutengeneza mazingira na hatimaye huwapa nafasi za wale waliokuwa juu
 
Si
Kama unataka ujumbe huu umfikie yule aliyesema hapangiwi, tafadhali tafakari tena, unamharibia mwenzio.
Sina nia hiyo bali ni ku appreciate alichokfanya, kwa maana ukisikia Resources Utilization ndio hiyo aliyofanya huyo afande, kitu ambacho vijana wengi inawashinda...ila on serious note kama watamtupia jicho anaweza akabadili kitu wakimpa nafasi
 
SACP Joel S. Bukuku ni Msomi katika Masuala ya Uongozi na Utawala kutoka formely known as IDM Mzumbe.

Ni mmoja kati ya Maafisa wasomi katika jeshi la Magereza,Tanzania Prisons Services.

He has almost reached retiring age,ni Mzee mmoja makini sana.
Hata ile TPS SACCOSS ni ubunifu wake.
 
Bukuku yupi? Ni yule aliekua Gereza la Lilungu Mtwara miaka ya 1999 hadi miaka ya 2000? Na alikua na mtoto wake mmoja marehemu wa kike kwa jina la Suma alikufa kwa ajari? Kama ni yeye nitakuja kutoa ya moyoni na mimi kwa kumfahamu kwangu huyu mzee na nitashangaa kwa kweli kama bado hajapewa nyadhifa za juu katika jeshi la Magereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeambiwa ndio yeye mkuu aliekuwepo huko Gereza Lilungu, inasemekana toka 2004 hajawai panda cheo pamoja na utendaji wake wa kuacha alama chanya kila anapopita, pongezi ziende kwa Rais Magufuli kwa kumkumbuka kiongozi huyu..
Long Life SACP J.S. Bukuku huko ulipo
 
Nimeambiwa ndio yeye mkuu aliekuwepo huko Gereza Lilungu, inasemekana toka 2004 hajawai panda cheo pamoja na utendaji wake wa kuacha alama chanya kila anapopita, pongezi ziende kwa Rais Magufuli kwa kumkumbuka kiongozi huyu..
Long Life SACP J.S. Bukuku huko ulipo
Basi kama ndie niseme tu kwamba uliyoyaandika ni kweli tena kweli tupu namfahamu huyu dingi na akikaa sehemu lazima aache alama njema kwa utendaji wake uliotukuka alifanya mengi makubwa lakini kwa miaka ile na cheo alichokawanacho nimeshangaa kusikia bado yupo Magereza na ajawa Kamishna wa Magereza mi nikajua labda kastaafu aiseeh Mh Rais nakuonba mtumie huyu mzee katika utawala wako hutojutia uamuzi wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo naona unapiga ramli kama mganga wa kienyeji a.k.a sangoma! Kwanini yusiongelee kitu kilicho na ushahidi wa dhahiri hadharani?

kama aliekuwa msemaji wa jeshi la wananchi alikuwa na kadi yachama na alipostaafu tu akala shavu ajabu lipi kwa kina kitila kuwa na kadi za ccm
 
Jeshi la magereza liliharibiwa sana na yule mzee aliyetumbuliwa na kulazimishwa ku-resign..tenda zote za jeshi hilo ana mkono, magari ya jeshi yanatumika kukatia majani ya mifugo yake na madudu mengi mengine...
 
Bukuku yupi? Ni yule aliekua Gereza la Lilungu Mtwara miaka ya 1999 hadi miaka ya 2000? Na alikua na mtoto wake mmoja marehemu wa kike kwa jina la Suma alikufa kwa ajari? Kama ni yeye nitakuja kutoa ya moyoni na mimi kwa kumfahamu kwangu huyu mzee na nitashangaa kwa kweli kama bado hajapewa nyadhifa za juu katika jeshi la Magereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu na wewe sema tukusikie
 
Back
Top Bottom