Rais Dkt. Magufuli amtembelea Mzee Sitta kumjulia hali

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,103
Reaction score
10,787
Rais Magufuli amemjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta ambaye anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es Salaam na hali yake inaendelea vizuri.
10.jpg

=========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Septemba, 2016 amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi.

Katika Mazungumzo hayo, wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM wamelalamikia kutolipwa mishahara yao kwa miezi saba, kutotolewa kwa michango ya wafanyakazi kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha, kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa madeni wanayozidai taasisi za Serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao yao.

Wafanyakazi hao pia wamemueleza Dkt. Magufuli kuwa Bodi na Menejimenti ya kampuni ya vyombo vya habari vya chama inayoendesha Gazeti la Uhuru na Redio Uhuru zimeshindwa kuendesha vyombo hivyo na wamemuomba aingilie kati ili kuvinusuru vyombo hivyo ambavyo kwa sasa vina hali mbaya kutokana na kukabiliwa na madeni makubwa, na biashara yake imeshuka kwa kiasi kikubwa.

Akijibu malalamiko hayo Rais Magufuli aliyetembelea ofisi za Gazeti la Uhuru akitokea Ofisini kwake katika jengo la Makao Makuu ya chama, Ofisi Ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam amemuagiza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana kuhakikisha mishahara yote wanayodai wafanyakazi inayofikia Shilingi Milioni 609 inalipwa ndani ya Mwezi huu wa Tisa, ameagiza kupatiwa orodha ya taasisi za Serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia ameagiza deni linalodaiwa na NSSF kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi lilipwe.

Kuhusu malalamiko dhidi ya Bodi na Menejimenti ya Kampuni hiyo, ajira za wafanyakazi, mafao kwa wastaafu, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti na mazingira magumu ya kazi Dkt. Magufuli ameahidi kuyafanyia kazi.

Aidha, Dkt. Magufuli amewapongeza wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa na amewakikishia kuwa anatambua umuhimu wao na kwamba atahakikishia anaboresha hali ya chombo hicho muhimu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta ambaye anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es Salaam na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

19 Septemba, 2016
 
Binadamu tunapoishi tusiishi kwa kuji sahau

Ova
 
Pole zake Mzee Sitta.....sijui nini kinamsumbua, maana kweli hata muonekano ni kama amedhoofu HV, namuombea Afya njema.
 
Rais Magufuli amemjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta ambaye anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es Salaam na hali yake inaendelea vizuri.View attachment 403192

Gerson,hii ungemuachia Ole Sendeka nae.Unakaba mpaka penalti!!!
 
Augue pole Mzee Samweli Sitta natuma Mungu atazidi mjalia afya njema, ila kuna haja ya kujifunza kulinda vinywa vyetu maana wengi walimtabiria mabaya aliyekuwa kada mwenzao, ila kwa sababu walitofautianaa kisiasa wakaona wamwadhibu kwa kuaminisha Dunia kuwa anaumwa huku tukiamini sisi wengine wote tu na afya iliyo njema, cha msingi kila kitu ni kumuomba na kumwachia Mungu ju ya uhalali wa maisha na afya zetu hapa duniani
 
jamani ziara za kichama nazo zina repotiwa toka ikulu sasa msemaji wa chama atasema kwenye lipi .
Leo mzee sitta hajaombewa kama alivyoombewa mzee malechela mana wakati malechela anaombewa kuna mtu alikua anapiga picha leo naona picha ya cheko tu.
Na hayo mambo ya kuto lipwa hayapo hapo tu aje na huku kwenye makampuni ya wahindi/ wachina
 
Pole zake Mzee Sitta.....sijui nini kinamsumbua, maana kweli hata muonekano ni kama amedhoofu HV, namuombea Afya njema.
Akienda kwa mganga wa kupiga lamuri, ataambiwa kalogwa na watz, kwa kuwaruhusu maccm wachafue katiba kwa kusiliba uchafu wao kwenye maoni waliotoa kwenye rasimu ya Warioba.
 
Pole sana Mzee Sitta. Ni vizuri sasa ukajifunza kulinda kinywa chako juu ya Afya za wengine walioumbwa na Mungu. Ile laana wa kumuombea mabaya Lowassa iliyofanywa na makada wa CCM mwaka jana ni lazima itawatafuna makada wote wa CCM, mpaka waje hadharani kumuomba msamaha Lowassa na kutubu kwa Muumba.

"mtukufu" naye anapaswa sasa kwenda Kagera kuwapa pole waathirika. Aache mambo yake ya ajabu ajabu.

Vipi tena UN hajakwenda? Mbona bado yupo Dar anazurura tu kwenye ofisi za Propaganda za CCM?
 
Hivi gazeti la uhuru linashika namba ngapi kwa mauzo?
 
Ukiona="Nkubaujuepost: yamezidi,Ungaber: 339746"]Mwanzoni si walibisha kuwa haumwi?[/QUOTE]
Ukiona hivyo ujue maji yamezidi Unga. Ugonjwa ni noma aisee!
 
Anamalizia kozi pale Migo kwa Ras Simba

Back
Top Bottom