Rais Dkt. John Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa IGP na familia za Askari wote waliouawa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
c1c117114b2f220b788b10d28831683a.jpg
Rais Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu na familia za Askari 8 waliuawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni wilayani Kibiti mkoani Pwani

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na walishambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es salaam - Lindi
 
Apeleke jeshi la wananchi makomandoo kumi tu wanatisha kuwamaliza hao vibaka wanaoua askari kila siku. Hivi hao ni watanzania kweli?
 
Tulisema humu kitendo alichofanya bashite na watu kuona live lakini hakuna hatua zilizochukuliwa ni dharau kwa serikali na ingelisababisha wananchi kutoogopa kufanya matukio ya kihuni kama hili.
we tulia tu,, nature is verry fair,,, usipolala usiku utalala mchana,, na for any action there is equal and opposite reaction.

Wafiwa nawapa pole ila serikali ijifunze kuona uchungu huo huo wakati raia wanatekwa na kuuwawa
 
maandiko katika kitabu cha mathayo mtakatifu " Yesu akawaambia wale theneshara akisema Kwa mtini jifunzeni" hivi sasa Tanzania wanachi wamejifunza kutoka kwa RC aliyeongoza uhalifu wa silaha na kusimamia tuko la utekaji , sasa wahalifu kumbe wamejifunza kuwa hakuna wa kuwazuia wala kuwakemea tungechukua hatua kali na madhubuti dhidi ya wahusika wa tukio la CLOUDS na lile la NAPE nadhani wahalifu wangeogopa tutegemee matukio mengi sana ya kariba hii
 
Back
Top Bottom