Dkt. Mwinyi asisitiza mazoezi kuepuka magonjwa yasiyoambukiza

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
740
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Oktoba 29, 2023 Zanzibar, amewasihi Watanzania kuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa yasioambukiza.

Dkt. Mwinyi amesema hayo mara baada ya kushiriki msimu wa tatu wa mbio za Zanzibar International Marathon zilizolenga kutangaza na kuhamisha Utalii katika visiwa hivyo.

Kwa upande wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewapongeza waandaji wa marathon hiyo, huku akiwataka wakazi wa Zanzibar kujiandaa kwa michuano ya AFCON itakayofanyika mwaka 2027 ambapo kwa Zanzibar Uwanja wa Aman utatumika.

Mbio hizo zimejumuisha wakimbiaji wa umbali wa KM5, KM10 na KM21 ambapo washindi mbalimbali wamezawadiwa fedha taslimu na kompyuta mpakato.
IMG-20231029-WA0010.jpg
IMG-20231029-WA0008.jpg
IMG-20231029-WA0009.jpg
IMG-20231029-WA0011.jpg
IMG-20231029-WA0013.jpg
IMG-20231029-WA0012.jpg
IMG-20231029-WA0014.jpg
IMG-20231029-WA0015.jpg
IMG-20231029-WA0016.jpg
IMG-20231029-WA0007.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom