Rais Dk. Mwinyi aitaka kamisheni ya maafa iweke mipango ya kuzuia maafa Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka kamisheni ya maafa iweke mipango ya kuzuia maafa siku zote na sio kusubiria maafa yatokee na watakeleze hayo kwa kutumia waatalam mbalimbali.

Aidha Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itatekeleza wajibu wake wa kuzuia mafuriko pia amewataka wananchi kupokea maamuzi yatakayoletwa kuhusu mipango ya kuzuia mafuriko nchini.

Amewataka wanananchi kutoa ushirikiano wanapoambiwa wahame maeneo yasiyopaswa kujengwa, kuondoa vibali maeneo hatarishi, kupisha ujenzi wa mitaro pamoja na usafi wa mitaro yenyewe.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika ziara yake ya kuwatembelea wananchi waliopata maafa baada ya mvua zinazoendelea kunyesha katika Wilaya tatu za Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwemo maeneo ya Bububu, Kibweni, Kwa Mzushi, Sebleni, Kwa Mtumwa Jeni, Kibonde Mzungu na Ziwa Maboga leo tarehe 14 Novemba, 2023.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi ameifariji familia ya Marehemu Aboubakar Abdallah mkazi wa Sebleni aliyefariki dunia kufuatua mvua hizo za vuli.

IMG-20231114-WA0016.jpg
IMG-20231114-WA0018.jpg
IMG-20231114-WA0019.jpg
IMG-20231114-WA0020.jpg
IMG-20231114-WA0014.jpg
IMG-20231114-WA0015.jpg
IMG-20231114-WA0017.jpg
IMG-20231114-WA0013.jpg
IMG-20231114-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom