Rais ateua makamishina wa kuu wapya wapolisi


Obama wa Bongo

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
5,138
Likes
3,617
Points
280
Obama wa Bongo

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
5,138 3,617 280
04/12/2013


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wanne wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa nafasi za madaraka katika Jeshi hilo kufuatia mabadiliko ya muundo wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka waliopandishwa vyeo kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na ambao wote walikuwa ni Naibu Kamishna wa Polisi

ni DCPErnest Mangu, DCP Thobias Andengenye, DCP Abdulrahaman Kaniki na DCP Hamdan Omari Makame.

Rais pia amempandisha cheo SACP Athuman Diwani kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.

Walioteuliwa katika nafasi za madaraka katika Jeshi la Polisi ni CP Clodwing Mtweve ambaye anakuwa Kamishna wa Fedha na Utaratibu wa Ugavi na Usafirishaji wa Watu na Vitu (Logistics),CP Paul Chagonja ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Isaya Mungulu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya jinai (DCI), CP Mussa Ali Mussa ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Jamii.

Wengine ni CP Hamdan Omari Makame ambaye anakuwa Kamishana wa Polisi, Zanzibar; CP Ernest Mangu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Jinai, CPThobias Andengenye ambaye anakuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, CP Abdulrahman Kaniki ambaye anakuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Ushahidi wa Jinai na CP Abdulrahman Diwani ambaye anakuwa Naibu Mkurugenzi wa DCI.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
[/COLOR][/LEFT]
 
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,232
Likes
7,103
Points
280
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,232 7,103 280
Kizungu cha haya madaraka ni nin?

CP Ernest Mangu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Jinai, CP Abdulrahman Kaniki ambaye anakuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Ushahidi wa Jinai na CP Abdulrahman Diwani ambaye anakuwa Naibu Mkurugenzi wa DCI.
 
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
5,210
Likes
707
Points
280
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
5,210 707 280
Nani amechukua nafasi ya SEMBE "Mtweve"???
 
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Messages
571
Likes
75
Points
45
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2007
571 75 45
IKULU vipi na statement ya leo? Kwamba Diwani anamrithi Manumba?
 

Forum statistics

Threads 1,273,205
Members 490,323
Posts 30,473,954