Wakuu mtakubaliana na mimi kuwa toka rais wetu aapishwe, hajawahi kutoka nje ya bara letu la Afrika.
Ninaelewa kuwa rais kwa kipindi chote hicho amekuwa na kazi nzito ya kusafisha uozo wa serikali zilizopita hasa ukizingatia operesheni yake ya kutumbua majipu.
Lakini pia ifahamike kuwa kama rais ni vema pia akapata nafasi ya kukutana na marais wenzake katika kubadilishana uzoefu wa kiuongozi. Ninachojua ni kwamba hakuna mtu ambaye amekamilika na wakati mwingine tunahitaji pia kujifunza kutokana na mazuri ya wenzetu.
Sasa basi ni lini rais ataamua kwenda kupata uzoefu zaidi wa kiuongozi kutoka kwa marais wenzake?
Nawasilisha.