Dkt Mwigulu Nchemba Ammiminia sifa na pongezi Rais Samia kwa kuendelea Kuaminiwa na Viongozi Mbalimbali Duniani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
23,549
17,373
Ndugu zangu Watanzania,

Waziri wa Fedha Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba Amemmiminia sifa na pongezi Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,kwa kuendelea kubeba imani na kuendelea kuaminika na viongozi wenzake Duniani Kwote.

Hii ni baada ya Rais wetu mpendwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) .ambapo Dkt Mwigulu Nchemba ambaye amewahi kuandika historia chuo kikuu cha Dar es salaam kwa kupata daraja la kwanza katika uchumi yaani First Class.

Kwa ambao wamefika chuo wanafahamu ugumu wa kupata daraja hili .maana wengine wanaishiaga kusapua tu kila muhula na wengine ku disco kabisa au wengine kutandika makarai matupu utafikiri mafundi ujenzi.

Lakini huyu Field Marshal au waweza kumwita Mr Clean kama ambavyo wengi hupenda kumwita aliweza kupata daraja la kwanza.Ndio maana aliweza kupata hata nafasi ya kufanya kazi BOT yaani Benki kuu ya Tanzania. Hapo waweza kujuwa hiki ni kichwa cha namna gani .ndio maana hata akisimama Bungeni kutolea ufafanuzi jambo linalogusa wizara yake huongea kwa kujiamini sana na kwa Takwimu.

Ushauri wangu kwa mr clean Dkt Mwigulu Lameck Nchemba ni kuendelea kuchapa kazi usiku na mchana kumsaidia Mheshimiwa Rais na kuhakikisha unatekeleza vyema sana maagizo na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa. Msaidie Mama kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote .

Lakini pia inapotokea kuna taarifa za upotoshaji zinazogusa wizara yako zimetolewa na watu wenye nia ovu ya kuchonganisha serikali na wananchi,basi ni vyema uwe una jitokeza haraka kutoa ufafanuzi.kama ambavyo umekuwa ukifanya ukiwa Bungeni.Fanya kazi na jiandae kumtafutia Mheshimiwa Rais kura za ndio za Urais hapo Mwakani.
Screenshot_20240818-203727_1.jpg


Kazi iendelee , Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mwigullu PhD anafukuzia uPM
Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba au waweza Kumwita Mr Clean ni akili kubwa, mchapa kazi na mzalendo kwelikweli kwa Taifa letu.ndio maana pamoja na kuwa katika wizara nyeti katika nyakati tofauti tofauti ndani ya serikali na hata chamani lakini hajawahi kuwa na kashifa ya aina yoyote ile ya rushwa au ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka. Yeye ni kazi kazi tu.ndio maana anaendelea kufanya vyema sana katika wizara ya Fedha ambayo ndio moyo wa wizara zote.
 
Back
Top Bottom