Rais Asiyependa kuumiza kichwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Asiyependa kuumiza kichwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, Feb 16, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ninafikiri wengi mtakubaliana na mimi kwamba tumejaliwa rais ambaye hapendi kuumiza kichwa kufikiri jinsi ya kutatua matatizo sugu ya wananchi wake kama umeme, Mauaji ya Arusha, migomo vyuo vikuu, matokeo mabaya ya kidato cha nne n.k. Ninafika mahali najiuliza hivi kama asipokuwepo nini kitaharibika kwa sababu uwepo wake au kutokuwepo kwake haku make any difference. Ingetosha tu kwa mawaziri wachache committed kuwepo na nchi ingekwenda tu.

  Nasema hivi kwa sababu wakati nchi yetu imo katika matatizo makubwa yanayopelekea uchumi kwenda kombo ambapo tayari inflation imekwenda juu kutokana na shida ya umeme, rais huyu bado yuko kimya. Humsikii kabisa yeye kama baba wa familia ya nchi hii akiingilia kati na kutoa utatuzi wowote na badala yake ana katabia ka kutupia mawaziri wake mpira bila hata kuwapa hint ya nini kifanyike.

  Rais wetu amekuwa mtu asiyependa kuumiza kichwa ktk kutatua matatizo makubwa ya watanzania bali yeye amekuwa akipendelea kufanya vitu virahisi rahisi ambavyo actually vilitakiwa vifanywe na wakuu wa Wilaya, wakuu wa mikoa au mawaziri.

  Kwa mfano, wakati wabunge na mawaziri na watanzania wanaumiza vichwa jinsi ya kuondokana na matatizo ya umeme, yeye rais anapanda ndege kwenda kufukua nyayo za binadamu wa kale Ngorongoro.Baada ya kuzungukia miradi yake serengeti anarudi tena Tumbi kufungua kituo cha akina mama.

  Hivi huyu amekuwa rais wa kufungua mikutano ,semina, kuhudhuria mazishi, kushuhudia matukio, kuwa mgeni rasmi n.k. Hivi vyote ni vitu rahisi ambavyo hata wakuu wa wilaya wengeweza kuvifanya na siyo rais anaomba Mungu ije barua ya mwaliko ili ajifanye yuko busy.

  Hivi haya ndo tuliyomchagua ayafanye? ni kwa nini ni mwoga wa kuingilia kutoa solution badala ya vijembe kama rais? Hivi yeye kama rais aliyejidai capable uwezo wake umefika wapi katika kufanya tatizo la umeme historia, kushughulikia matatizo makubwa ya msingi yanayowakumba watanzania kwa sasa?

  Kwani nini anawatega mawaziri ili waonekane hawawezi wakati ukweli ni kwamba anawatumia kama kinga huku akiwa hana kabisa dharira ya dhati ya kutatua tatizo husika?

  Kwa nini ameshindwa kusimama katika nafasi yake kama rais wa nchi kuonyesha uwezo na uwepo wake?
  Ninaomba ajue tunafuatilia kwa makini jinsi ambavyo amejiweka mbali na matatizo ya watanzania na kuamua kukaa mbali huku akiangalia matatizo ya watanzania kama movie ya vichekesho.

  Naomba JK ujiulize kwa uaminifu kabisa kwa nini upo hapo kama kiongozi wa nchi wakati wa TZ wanakosa majibu ya matatizo yao kama umeme, kufeli kidato cha nne, mauaji Arusha N.k. Ina maana wewe uko busy kuliko Barak Obama wa US ambaye kila wakati siyo tu ana updated information za mambo yanayoendelea ktk nchi yake at his finger tips bali anayashughulikia kwa wakati muafaka.

  Mkuu JK una viporo vingi sana vinavyosubiri majibu yako kama mtu mwenye mamlaka makubwa kuliko watu wote katika nchi hii. Hatuwezi kusubiri hadi utoe hotuba ya mwaka mpya tarehe 31/12/2011 tunahitaji utuambie wewe una solution gani kama rais. Tunataka tuone creativity au maadam wewe tatizo halikuhusu basi tukafilie mbali sisi.

  Tunachotegemea sisi ni kwamba rais angekuwa yeye ndo anakula mfupa uliomshinda Ngeleja, Shukuru Kawambwa, Said Mwema, Pinda na mawaziri wengine.
  Sasa mkuu wewe unafanya tu vitu vilaini na visivyo vya lazima na kuwaachia mawaziri vitu vyote vigumu bila msaada wowote?. Please JK take your position acha kukwepa majukumu kwani unadhalilisha cheo cha urais na unataka tuamini kwamba urais ni just symbolic na wala huna meno.

  Ninavyoona JK unataka kuwa kama mfalme na siyo mtendaji mkuu wa serikali mwenye kufanya maamuzi makubwa na magumu kwa mustakabali wa nchi yetu na haswa watanzania wote.

  Kwa ufupi tunashindwa kukuelewa. Kama ulijua urais mgumu kwa nini hukumwachia mtu mwingine basi agombee urais kuliko kutumia Ikulu kama kijiwe cha kupumzikia na kwenda kufanya matembezi ngorongoro, mikutanoni n.k.

  Kwa ufupi mkuu JK ni jambo la wazi kabisa unawategea mawaziri na umewasukumia kazi zako zile ngumu na za kuumiza kichwa na za kwao rais ukachukuwa wewe.
  Na ndiyo maana ninasema mkuu unaogopa majukumu yanayoumiza kichwa na badala yake unafanya vile vitu vyepesi then unajidai unaongoza nchi.

  Hii nchi kwa sasa inajiongoza yenyewe kwa sababu umekimbia kiti na kama ni gari basi brake zimefeli tena likiwa linashuku mlima na hapa hatujui tutaangukia wapi.
  Polisi na Mabomu ya machozi ndio mtindo mpya uliobaki wa kuongoza nchi.

  Please rudi kwenye kiti uongoze nchi au declare umeshindwa tujue moja ila kwa namna nchi inavyokwenda ni kama haina rais kwa sasa
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [SIZE=+2]TO TYRANTS OF THE WORLD

  [/SIZE]By Tunisian Poet Abul Qasem El-Chebbi (1909 - 1934)

  Hey you, the ruthless tyrants...
  You lovers of darkness...
  You the enemies of life...
  You've made fun of innocent people's wounds; and your palm is covered with their blood
  You deforming the value of existence and sowed seeds of sadness in their land

  Wait, don't let the spring, the clearness of the sky and the shine of the morning light fool you...
  Because the darkness, the thunder rumble and the blowing of the wind are coming toward you from the horizon
  Beware because underneath the ash there is fire

  Who grows thorns will reap wounds
  The river of blood you shed will sweep you away and you will be burned by the fiery storm.

  (The Original Version)
  [​IMG]
  SOURCE: UNITED NATIONS. TO TYRANTS OF THE WORLD.

  UJUMBE HUMU:

  Ni ajabu na kweli kwamba kumbe yale yote yaliotokea Tunisia kupindua serikali dhalimu ya aliyekua Rais Ben Ali na kisha nguvu za virutubisho vya 'Matunda na Mboga Mboga' Shujaa Machinga Mohamed Bouazizi kuvuka mipaka yote YALISHATABIRIWA MNAMO MWAKA WA 1934 KUTOKEA.

  Mtunga mashairi mzaliwa wa nchini Tunisian, Ndg Abul Qasem El-Chebbi (1909 - 1934), aliyaona kwa macho yake udhalimu na ufisadi ukitendeka nchini mwake hata akaamua kuyaweka katika kumbukumbu za kimaandishi kama tulivyoyaona hapo juu.

  Baada ya takriban miaka 76 yale maoni yake yakaondoka kwenye karatasi; yakaenda mitaani na kugeuka moto mkubwa usiozimika uliotimulia mbali madikteta 2 hadi sasa na kuendelea kushika kasi!!! Mmachinga Mohamed Bouazizi ndiye silaha ya maangamizi iliokamilisha utabiri mzima!!!


  [​IMG]sidi‑bouzid‑12.jpg

  200 × 200 - Mohammed Bouazizi's (and Tunisia's) agony.


  [​IMG]

  6a00d8341c60bf53ef0133f5f3acc6970b‑500wi

  ... Tunisian Mohamed Bouazizi, whose immolation, December 17, launched the ...
  xomba.com

  Similar ‑ More sizes


  [​IMG]

  self‑immolation.jpg

  240 × 196 - In the case of Mohammed Bouazizi, the youth from Sidi Bouzid in Tunisia, ...
  jonathanfryer.wordpress.com  [​IMG]

  12626.jpg

  450 × 338 - Mohamed Bouazizi's fruit cart pushes over Ben Ali's throne
  israelagainstterror.blogspot.com


  [​IMG]

  b2f9473a7b98b167c7130b26111d028b.gif

  ... the Tunisian revolution began in with the suicide of Mohammed Bouazizi ...
  rozhlas.cz​
  Laiti watawa huwa huchukua japo dakika 30 tu kujisomea kila siku, badala ya kuendelea mfululizo kusikiliza maoni ya wanafiki, naamini wangeweza kuona shairi hili na kuzingatia zaidi onyo kali kwenye mistari ya 7 na ya 10 ili zahama yasiwakute kama ambavyo tunaendelea bado kushudia hivi leo.

  Enyi watawala: kuleni kidogo kwa afya njema na wala msizidishe kipimo chenu. Kila mmoja wetu katika jamii ANAYO UMUHIMU WAKE na wala asidharauliwe kitu.
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nilimfahamu mkwere tangu zamani kwamba yeye ni mtu wa starehe na hapendi kuumiza kichwa. Matatizo ya umeme, foleni za magari mijini, ukosefu wa madawa hospitalini, n.k hayamsumbui hata kidogo.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..matatizo ya mgao nadhani yalianza wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

  .
   
 5. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Anaendesha nchi kama daladala au familia yake!
   
 6. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Obama ametenga budget kubwa kwenye energy,Mzee Zuma huku ametenga heftly, mzee Museveni pia...sasa tangu kihansi iwekwe na mzee Mkapa mpaka leo hakuna mradi wa maana, kipaumbele ni kipi?
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yanayotokea ndani ya wiki moja
  - Waziri Mkuu Pinda anapindisha sheria kwa kulidanganya bunge na wananchi huko Dodoma bungeni
  - Spika Anna Makinda Samamba anatetea wongo wa pinda Bungeni kwa kumtetea Pinda aheshimiwe kama mkubwa hata akidanganya
  - Mheshimiwa Godbless Lema ananyimwa haki bungeni ya kuanika ukweli ambao Pinda amelidanganya bunge na wananchi
  - Msafara wa Mke wa Rais Kikwete unapata ajali na dereva wa Ikulu (usalama wa taifa) anafariki ajalini
  - Leo ghala la silaha za vita la jeshi la Wananchi mabomu yanalipuka na kuathiri makazi ya raia kitu ambacho kilishatokea ndani ya miaka miwili huko Mbagala.
  Tuendelee kuomba Mungu atunusuru
   
 8. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kuna kitu nimefikiria kwa muda mrefu na ninaamini hakuna raha na urahisi kama kuwa kiongozi wa nchi za Afrika....viongozi wengi wanafikiria kujilimbikizia mali...hivi huoni siku hizi ubunge imekuwa deal kama hun pesa hupati ubunge?

  Jaribu angalia marais wetu kabla na baada ya kupa ta urais...wanvyong'ara


  [​IMG]Kabla[​IMG]
   
 9. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ebu tuwekeeni picha ya mkwere naye tumwone kabla na baada ya kuwa rais kutokana na uchakachuaji. Ikiwekwa na ya mamsapu wake (salma) itaboresha hoja yako kwani naona shingo ake inaendelela kupata makunyanzi kutokana na supu za magogoni.
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Haya yote ni matokeo ya mafanikio ya utekelezaji wa sera za chama tawala. Upungufu wa umeme ni matokeo ya kuongezeka kwa viwanda vinavyohitaji umeme zaidi na wananchi wenye uwezo wa kutumia umeme. Foleni ni matokeo ya neema kwa wananchi, kutokana na ongezeko la kipato, ambao wamenunua magari mengi zaidi na hivyo kusababisha foleni.
   
 11. Double X

  Double X Senior Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nakumbuka sana maneno ya prof Lipumba wakati jk anagombea 2005, alisema huyu mtu namfahamu sana tokea akiwa chuo kikuu nikimfundisha, ni mtu wa MZAHA-MZAHA sana na akaongeza ni mtu anaependa starehe tuu, na ndio alivyo, jk is not serious in any matter which needs seriousness, i dont know what thing is he capable with, watu wanaangaika namna ya kutatua tatizo la umeme yeye yupo ngoongoro kwa shuguli ya kipuuzi kabisa ambayo hata DC angeifanya, he is a mere moron, stupid idiot!!!!
   
 12. P

  Preacher JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa jamani raisi wetu si BONGO-LALA???? thinking capacity = NIL - alidhania kuwa rais ni kupigiwa makofi, kupishwa kwenye foleni, kupanda ndege kwenda majuu, kutanua na familia yake - kucheka cheka ovyo.................

  mwanzoni alijifanya anaenda kutembelea wagonjwa muhimbili ................ilikuwa danganya toto .........sasa wanapolala chini, hawana dawa, wanakufa kwa kukosa matibabu kisa hawana hela za rushwa.................. mbona haonekani tena??????????? JK TAFADHALI SANA JIUZULU
  wenzako kina BEN ALI, HUSSEN MUBARAK - hawakutegemea watakimbia siku moja .................... JK DONT BE SO SURE - TAKE ACTION AND RESIGN - NCHI IMEKUSHINDA - ACHA MWINGINE AONGOZE ..........ni BETTER UTOKE HIVI SASA KWA HESHIMA KULIKO KUTOKA KWA AIBU BAADAYE ................ ALAMA ZA NYAKATI ZINAONYESHA.
   
 13. m

  mtimbwafs Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenye macho haambiwi Tazama!!!.
   
 14. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana, rais asiyependa kutatua mambo magumu au kufanya maamuzi mazito! huyu mzee hawezi kazi bora aondoke wengine waongoze wenye uwezo wao
   
 15. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Serikali yetu imejaa watendaji wavivu,wanaopenda starehe na kusifiwa,wasiopenda kuwajibika,wala rushwa,wanaopeteza muda mwingi kusia chama tawala wakiongozwa na raisi mvivu!!!
  but one day watanzania watakataa upuuzi na ujinga wa viongozi and that time is very close!!
  THE END OF CCM AND AFTER
   
Loading...