Rais asiwe Mwenyekiti wa Chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais asiwe Mwenyekiti wa Chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Che Guevara, Jan 18, 2010.

 1. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]Date::1/18/2010 [/FONT]
  [FONT=&quot]CCM wataka rais asiwe mwenyekiti wao [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT][FONT=&quot][/FONT]​
  [FONT=&quot]Exuper Kachenje na Sadick Mtulya, Mwananchi.[/FONT]
  [FONT=&quot]WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema wakati umefika wa kumpunguzia rais majukumu ya kichama ili awajibike zaidi katika kazi za serikali na kukifanya chama kuwa na nguvu ya kuhoji utendaji wake.[/FONT]
  [FONT=&quot]Wakati mjadala dhidi ya utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete ukielekea kupoa, Wana-CCM hao wameibuka upya na kujenga hoja kuwa kumuachia rais madaraka ya serikali na chama ni chanzo cha kukwama kwa utekelezaji wa malengo mbalimbali ya kitaifa na kinaondoa nguvu ya kumbana anaposhindwa kuwajibika ipasavyo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mwishoni mwa mwaka jana, mawaziri wawili wa zamani walionyesha kuwa na wasiwasi na utendaji wa Rais Kikwete wakisema anashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na kwamba chama kimepoteza hadhi yake kutokana na kutekwa na matajiri.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mjadala huo ulipoa baada ya Rais Kikwete kuahidi kukaa na wenzake kuandaa majibu, hata hivyo suala hilo linaonekana kuibuka kwa sura nyingine. [/FONT]
  [FONT=&quot]Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi katika ofisi ndogo za Bunge jiijini Dar es Salaam wakati wa kujadili ripoti hiyo ya Mfumo wa Kupima Utawala Bora wa Umoja wa Afrika (APRM), baadhi ya wabunge na wanaharakati wameshauri kutenganishwa kwa mamlaka ya chama na serikali kwa rais kwa maslahi ya taifa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Wametaka pia vyama vya siasa kuangalia na kurekebisha katiba zao ili kuondoa utata huo ambao walidai unakwamisha uwajibikaji.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Ni kitu kibaya kwa rais kuwa mwenyekiti wa chama," alisema mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe alipozungumza na Mwananchi.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Upo umuhimu wa kutenganisha nafasi hizo. Tatizo tumerithi katiba nusu nusu. Tumerithi nusu kutoka Marekani tunayotumia kuchagua rais na nusu ya Jumuia ya Madola tunayotumia kupata mawaziri na watendaji wengine, lakini sasa tunatakiwa kurekebisha katiba ya nchi na ya chama (CCM)."[/FONT]
  [FONT=&quot]Alifafanua kuwa tatizo la kofia mbili linaonekana katika utekelezaji wa maamuzi na kwamba mengi hukwama kutokana na hali hiyo na akaongeza kusema:"Ni vyema rais asiwe mwenyekiti wa chama ili kutoa nafasi ya uwajibikaji zaidi na chama kuwa na nguvu ya kuhoji utendaji wake."[/FONT]
  [FONT=&quot]"Hii ndiyo hali yetu ya sasa... rais ndiye mwenyekiti wa chama, kwa hali hiyo yeye ndiye anaongoza vikao vya kamati kuu ya chama pia ndiye mwenyekiti wa baraza la mawaziri. Nani atahoji utendaji wa serikali ikiwa rais ni mwenyekiti wa chama, baraza la mawaziri na hata vikao vya Nec."[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa mujibu wa Mpendazoe mfumo huo ni wa kulindana na unasababisha kuchelewa kutolewa kwa taarifa za utekelezaji zinazojadiliwa ndani ya chama na serikali.[/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema tatizo hilo pia lipo kwa mawaziri ambao nao hutumia nafasi zao za uwaziri na kujipatia nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, hivyo kuweka ugumu katika kufuatilia utendaji wao hasa serikalini kwa kuwa huweza kujijengea wigo wa kujilinda ndani ya chama.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli alisema ili kudhibiti mfumo wa kulindana ambao alidai umeota mizizi, mawaziri wanaoteuliwa na rais wathibitishwe na Bunge.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Hii itasaidia kuongeza ufanisi na uwajibikaji utakaokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa," alisema.[/FONT]
  [FONT=&quot]Lembeli, ambaye ni mmoja wa wabunge wanaojipambanua kuwa wapambanaji wa vita ya ufisadi, alikwenda mbali zaidi na kuhoji: "Pamoja na baraza la sasa la mawaziri kuwa na vijana wengi, utendaji na ufanisi wake upo wapi? Haya ndiyo madhara ya kulindana na kubebana."[/FONT]
  [FONT=&quot]Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Dk Benson Bana alisema si lazima rais kuwa mwenyekiti wa chama.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, akasisitiza kwamba:" Hakuna utata wowote kwa rais ambaye anatokana na chama tawala pia kuwa mwenyekiti."[/FONT]
  [FONT=&quot]Dk Bana, ambaye ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya sayansi ya siasa, alifafanua kwamba kitendo cha rais kuwa na kofia mbili kinasaidia kuondoa migongano baina ya chama na serikali hasa katika nchi ambazo ni changa kidemokraia na mifumo ya utawala.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Kutokana na uchanga wa mifumo ya utawala na masuala ya demokrasia katika nchi nyingi za bara la Afrika na hata Tanzania ni muhimu Rais akawa pia ni mwenyekiti wa chama ili aweze kudhibiti migongano ndani ya chama na pia kati ya chama na serikali. Lakini sio lazima rais awe ni mwenyekiti na pia sio mfumo mzuri," alisema Dk Bana.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mtaalamu huyo alisema katika nchi zilizo na mifumo imara ya utawala na demokrasia, rais anaweza asiwe mwenyekiti wa chama. [/FONT]
  [FONT=&quot]Akizungumza hivi karibuni kuhusu viongozi kuwa sehemu ya mihimili ya nchi (Bunge na serikali) na hasa mawaziri, mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango alisema ni muhimu mfumo ukabadilishwa ili mawaziri wasitokane na wabunge.[/FONT]
   
 2. T

  TheUchungu Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili lilishasemwa hapo mwanzo....kweli lisemwalo lipo....kweli EL anatisha...
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  I strongly agree with the idea.
   
 4. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri lakini wamelitoa kiunafiki zaidi tatizo linaeleweka ni utendaji hafifu wa rais aliyepo madarakani si kofia mbili hawataki kusema ukweli kofia mbili hazikuanza leo Mwl, Mwinyi na Mkapa pia walivaa, kama wanafikiri kutenganisha kofia ndio suluhu ya matatizo they are wrong ndio italeta matatizo zaidi kiutendaji M/kiti wa chama tawala ataonekana ndiye mwenye sauti na rais atataka ku-prove kuwa yeye ndiye the top misuguano haitaisha.

  Mimi nachofikiri ni wao kuelezea wazi wazi uwezo wa kiutendaji wa rais ikiwezekana kupiga kura ya kutokuwa na imani na uwezo wa rais tusilipake mafuta tatizo tuliseme wala si uhaini kujadili uwezo wa rais kwa manufaa ya taifa sababu rais ni wetu sote.
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  It make sense!
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wazo zuri je litatekelezeka hapa kwetu asa ccm
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ya kofia mbili hata baba wa taifa alishayaongelea enzi za uhai wake, kutenganisha shughuli za kichama na Serikali inakuwa vigumu sana.

  Kwa mfano Rais yupo Ziara ya kiserikali mikoani, utakuta Mwenyekiti wa CCM mkoa naye yupo katika list ya wenyeji wake na magwanda yake ya kijani eti anakuja kumpokea mwenyekiti wake.

  Hata Pinda alishakiri kwamba ni vigumu kwake kutenganisha shughuli zake za kiserikali zisiingiliane za zile za kichama. Haya ni mambo ya kimfumo ndiyo maana tunasema turekebishe hivi vitu mapema kuepusha usumbufu.

  Kumbukeni kwamba hawa wakubwa wanapokua katika ziara za kiserikali wanatumia pesa zetu si pesa za CCM, pia wanatukera sisi ambao si wanachama wa CCM kutubana na ziara hizi za viongozi wetu wa taifa.
   
 8. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  KWa CCM hii hilo ni kama ndoto ya mchana. Nani anaweza kumvika paka kengele kati yao? Hilo litatekelezeka iwapo Katiba ya Nchi kwanza itapitiwa upya. Ikiwa CCM na Serikali yake wanaogopa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi ambalo ni suala dogo tu hilo la kumpoka Rais Uenyekiti wa Chama wataweza? Yangu Macho and am waiting for that.
   
 9. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #9
  Jan 18, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,452
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi sana na Dr. Bana,kama hajikombi kwa watawala,basi anauwezo mdogo sana huyu jamaa.
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni mfumo wetu. Siasa zetu zina tegemea sana na nafasi ya mtu kwenye chama chake. Raisi asipo kuwa mwenyekiti wa chama chake haswa CCM I guarantee you hiyo ita sababisha mvutana wa kugombania influence. Kutokana na hali ya sasa don't know how well it would work. Ni good theory but kwa reality yetu I don't know how well it would work.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Tatizo sio Rais kuwa Mwenyekiti, mbona Mwalimu alikuwa na vyote na hakukuwa na tatizo na uongozi wake, ambao ulikuwa very clear anasimamia nini as opposed na hawa wa sasa ambao mpaka leo we have no clue wanasimamia nini hasa,

  - Tatizo ni uwezo mdogo wa uongozi kutoka kwa viongozi wetu ambao wanatumia hela nyingi sana kutafuta uongozi, hela nyingi kuliko hata mishahara watakayoipata wakiwa kwenye power, sasa unajiuliza wanatafuta nini kama sio rushwa?

  - Hawa viongozi wa CCM ni vyema tukawa makini nao sana na kila wanalolisema, hili la Mwenyekiti na Rais wala sio ishu wanaogopa nini kusema the really ishus! Kama hawazijui basi watuulize wananchi, lakini sio kutupandisha mikenge!


  Es!
   
 12. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Jamaa anadharirisha sana taaluma.
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ninakubaliana na mawazo yako Mwanafalsafa1. Ukweli ni kwamba mawazo ndiyo baadae hujenga au kubomoa kile ambacho kinafikiriwa. Mimi binafsi sioni tatizo kwa Rais kuwa Mwenyekiti wa Chama au la. Kimsingi ni kwamba je haya ambayo tunayatamka yamefanyiwa utafiti wa kiasi gani ili tuweze kuyaona kwa kina na kuyajadili? 'Experience is the best teacher', uzoefu na uchanga wa demokrasia katika nchi zetu hasa za kiafrika unaonyesha kuwa bado hatujakuwa na utamaduni wenye mafanikio wa kuendesha nchi katika mfumo ambao unatoa fursa kwa viongozi wa juu kimamlaka yaani Rais na Kiongozi Mkuu wa Chama Tawala kuwa tofauti. Inawezekana kabisa tofauti yetu sisi Tanzania na Somalia ya leo ni kuwa na uongozi wa juu usiokuwa wa migongano. Ni hulka ya wanademokrasia wachanga kujikita katika kugombania madaraka ya nchi bila ya kujali athari zinazoweza kuwakuta wananchi wa kawaida. Utekelezaji wa demokrasia hautakuwa na maana yeyote endapo usalama na amani kwa raia utakuwa katika mashaka. Kwa mfano, Rwanda baada ya RPF kuingia madarakani ilikuwa inatumia mfumo wa Kiongozi wa Nchi (Rais) si Kiongozi wa Chama Tawala. Kwa kuzingatia demokrasi yetu changa ya kiafrika, Rwanda iliyumba-yumba hadi pale walipopata Rais ambaye pia ni kiongozi wa Chama Tawala. migongano kati ya Rais na Kiongozi wa chama tawala yalizorotesha ukuaji wa amani na usalama wa raia. Leo hii Rwanda inasonga mbele kwa kasi kwa sababu moja ya TAASISI muhimu katika katika maendeleo ya kichumi na kisiasa yaani RAIS inaweza kufanya kazi zake bila ya migongano ambayo si ya lazima sana.
  Ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu kama kuna chama kinaona kuwa Rais wa ni vema akawa ndiye Kiongozi Mkuu wa Chama, basi waachiwe, kwani wanahoja yenye nguvu na maslahi kwa wapiga kura wao.
   
 14. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Bramo, from my hearing of Dr. Bana from time to time, that's my thinking also.
   
Loading...