Rais anapotembelea ofisi mbalimbali

Rais anapotembelea ofisi mbalimbali

Urais ni taasisi hivyo elewa kwamba Rais anajua kila kitu.
Hivi wewe umesoma ulichandika au unapost post bila kujua unapost nini. Hakuna aliyezaliwa na mwanamke anayejua "kila kitu". Kweli ndalichako ana kazi!
 
Ww umetumwa kuchokoza mada, tuongee mbovu watu wakamatwe ushindweeee!
 
Kwahio ukiwa na PhD ndio unajua ofisi zote nchini zinafanya vipi kazi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimeona mara mbili sasa inajirudia, Rais anapotembelea ofisi (mfano airport, na pale bandarini) anapouliza maswali na kubaini makosa watu waliowekwa pale huanza kujitetea, nakutaka kumfundisha rais (kumlecture).

Mimi kwa maoni yangu sio jambo zuri kwa wewe mtumishi kuanza kubishana na rais, hii sio adabu kabisa. Lazima ujue unaongea na mkubwa anapokuambia kuna tatizo sehemu fulani we kili tu huwezi kufa, kwani ukikili harafu ukajirekebisha kunatatizo gani?.

Pia watu lazima wajue Rais wetu Magufuli ana PhD sio ya kupewa, kasomea hivyo siyo rahisi kwa mtu mwenye PhD kudanganywa kijinga kijinga, kama walizoea kudanganya wabadilike.

Mtu anayetuongoza ni msomi sio rahisi kumdanganya. Mfano pale bandarini anakueleza kwamba kwanini mtu aki feed information kule wewe huoni unapokuwa ofisini, oo eti, eti eti. Kwanini usiseme tu kwamba nimekosea na nitajirekebisha au tutajirekebisha.

Mimi wakati nasoma MSc nilikuwa nambishia Prof wangu juu ya topic fulani akaniambia don't lecture me, baadae nikajifunza unapomsikiliza Prof unajua mengi ambayo ulikuwa hujui kuliko kuanza kujifanya na wewe much know.

Nilipokuwa nafanya PhD niliendelea kumsikiliza Prof bila kumbishia ila tu nilikuwa natoa maoni kwanini isiwe hivi, na Prof alikuwa anajibu na kuonyesha njia.

Nawaomba watanzania wenzangu wajue Dr. Magufuli sio Dr wa kuchoma sindano, au Dr wa kupewa, ni PhD holder. Huwezi ukamyumbisha kijinga kijinga.

Ujue watu kama hawa waliosoma hawayumbishwi kijinga, huwa hawatetemeshwi na nyau.

Angalia hata Prof Muhongo, huwezi ukamshake kwa maneno yako yasiokuwa na kichwa au miguu. Hata wazungu wanajua kwamba tunaenda kuonana na mtu msomi sio yes man.

Zamani akija mzungu tu wizarani, utasikia waziri, ee tujiandae kwa mapokezi maalumu. Hayo yamepitwa na wakati kwa serikali yenye wasomi kama ya JPM.

Watu walikuwa wanakuja na begi tu eti anataka kuwekeza na walikuwa wanakubaliwa ila angalia sasa hivi hawaji, wameshasoma upepo.

Sasa watanzania tubadilike, Rais akija kwako akibaini kuna makosa, kubali halafu badilika, sio kujitetea. Hii inatuonyesha hufai maana hujui unacho kifanya.

Muungwana anakubali na anabadilika.
Hoja yako ni nini hapa maana andiko lako linajichanganya sana!
 
Inajiludia = inajirudia

Kili = kiri

Ndugu msomi wa PhD kama hujui kuandika mimi nawashawishi vipi wanafunzi wangu wa darasa la nne waandike vizuri?
Hayo makosa ni common sana,na pengine sio kuwa mtu akikosea anakuwa hajasoma.imategemea na amebobea wapi,na zaidi kuna mother tongue effect....

Kwa mfano wahaya badala ya kusema Ali,wanasema Hali.

Watu wa kusini badala ya kusema mtu utaskia ntu...lakini ksin hukohuko nyanda za juu badala ya karibu au kaburi ataandika ama kusema ,kalibu au kabuli.

Watu wa iringa badala ya mpaka,wanaandkka au kusema mbaka,

Ntakuja wanandika ndakuja...hii haitegemei Elimu ya mtu...utakuea shahidi kwa hili kama ww ni mfatliaji mzuri....issue ni umebobea wapi?
 
Hoja yako ni nini hapa maana andiko lako linajichanganya sana!
Hoja ni kwamba Raisi anapokutembelea ofisini kwako, akabaini kuna tatizo hata kama upeo wako hauoni ni tatizo kubali tu, usibishane nae kwenye camera. Hiyo ndio adabu. Nitajitahidi kutoa elimu humu JF naona wengi hawana elimu ya maadili, wamezoea baba anasema na mtoto anasema (tabia mbaya kabisa)
 
Lakin kuwa na PHD sio tafsri ya kuwa unajua kila kitu....na

Hivi kwa mfano ukiwa na PHD utajua watu hulala vipi ndani ya majumba yao?

Mim ndio nilichokiona pale bandarini..wale wameweka partitions za vyumba na wanautaratibu ambao unawasaidia wao palepale ili kuendesha shughuri zao(sio lazima rais kujua kama tu mbo yanenda vzr).

Rais alitakiw awasikilize then atoe maoni yake juu ya kile alichokuwa anakisema kama vile kuweka madrisha ili waweze kuona kama alivyotaka.

Hii ingechukuliwa kama maboresho tu ya ofisi lakin sio kuwathreaten kisa ana PHD kama ww unavyosema..kama anajua kila kitu si afanye kila kitu basi yeye mwenyewe

Na PHD Yenyewe unaspecialize sio kuwa ndio unabobe kila angle hapana bnaaaa....
 
Hoja ni kwamba Raisi anapokutembelea ofisini kwako, akabaini kuna tatizo hata kama upeo wako hauoni ni tatizo kubali tu, usibishane nae kwenye camera. Hiyo ndio adabu. Nitajitahidi kutoa elimu humu JF naona wengi hawana elimu ya maadili, wamezoea baba anasema na mtoto anasema (tabia mbaya kabisa)
Kwa sababu yeye ni malaika?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hayo makosa ni common sana,na pengine sio kuwa mtu akikosea anakuwa hajasoma.imategemea na amebobea wapi,na zaidi kuna mother tongue effect....

Kwa mfano wahaya badala ya kusema Ali,wanasema Hali.

Watu wa kusini badala ya kusema mtu utaskia ntu...lakini ksin hukohuko nyanda za juu badala ya karibu au kaburi ataandika ama kusema ,kalibu au kabuli.

Watu wa iringa badala ya mpaka,wanaandkka au kusema mbaka,

Ntakuja wanandika ndakuja...hii haitegemei Elimu ya mtu...utakuea shahidi kwa hili kama ww ni mfatliaji mzuri....issue ni umebobea wapi?
umefanya vizuri kumuelimisha, hawa ndio wakipewa mtihani anahangaikia nukta badala ya kuendelea ma kujibu maswali mengine.
 
Haiwezekani kwamba raisi atajua kila kitu that's why kila mtu ana ujuzi wake,unapasa kumsikiliza mtu Maelezo anayokupa but mtu bado anajieleza we unaondoka lazma mtu ajisikie vibaya.mengine yako juu ya uwezo wetu inapasa asikilize ili afanye Marekebisho panapo upungufu.mtu hasikilizwi but kutumbuliwa ndo uamzi unaochukuliwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aisee kwa hiyo injinia Mwenye PhD anajua tiba zaidi ya Mganga Mwenye stashahada? Hivi kwa nini mnawaogopa sana watu kwa sababu ya elimu zao!!
 
Kuwa na Phd au professor sio kwamba anajua kila kitu...Mtu kama professor Lipumba unategemea watu wasimbishie eti sababu ni professor?? Akitembelea sehemu asiyoijua ni vizurai apate shule aelewe ila kama anaempa shule atakua anajitetea hiyo nayo sio nzuri. Naunga mkono hoja kwamba Rais aendelee kutembelea maofisi ili kujionea kinachoendelea kwa macho yake.
Halafu hii dhana ya kumuona Rais kama mtukufu flani hivi haijakaa sawa. Rais ni mtanzania mwenzetu tuliyempa dhamana ya kuongoza nchi na kuzisimamia rasilimali zote na anatakiwa kupita baadhi ya sehemu kuona kama rasilimali tulizompa dhamana ya kuzisimamia zinatumiwa vizuri. Tuache uoga
 
Sijasema mtu mwenye PhD anajua kila kitu, ila elewa kwamba mtu mwenye PhD ana horizon ya kuona mbali kuliko mtu mwenye MSc na BSc. Nazani umeelewa.
 
Maandishi yako hayaoneshi kabisa kama Na wewe ni msomi wa kiwango ulichosema, unarudia rudia maneno hayo hayo. Ujumbe wako mzuri hata mm naukubali kwa kiasi fulani but too much repeations
 
Back
Top Bottom