Kaya Nogu Sabho Ndamu
Member
- Sep 4, 2016
- 44
- 28
Nimeona mara mbili sasa inajirudia, Rais anapotembelea ofisi (mfano airport, na pale bandarini) anapouliza maswali na kubaini makosa watu waliowekwa pale huanza kujitetea, nakutaka kumfundisha rais (kumlecture).
Mimi kwa maoni yangu sio jambo zuri kwa wewe mtumishi kuanza kubishana na rais, hii sio adabu kabisa. Lazima ujue unaongea na mkubwa anapokuambia kuna tatizo sehemu fulani we kili tu huwezi kufa, kwani ukikili harafu ukajirekebisha kunatatizo gani?.
Pia watu lazima wajue Rais wetu Magufuli ana PhD sio ya kupewa, kasomea hivyo siyo rahisi kwa mtu mwenye PhD kudanganywa kijinga kijinga, kama walizoea kudanganya wabadilike.
Mtu anayetuongoza ni msomi sio rahisi kumdanganya. Mfano pale bandarini anakueleza kwamba kwanini mtu aki feed information kule wewe huoni unapokuwa ofisini, oo eti, eti eti. Kwanini usiseme tu kwamba nimekosea na nitajirekebisha au tutajirekebisha.
Mimi wakati nasoma MSc nilikuwa nambishia Prof wangu juu ya topic fulani akaniambia don't lecture me, baadae nikajifunza unapomsikiliza Prof unajua mengi ambayo ulikuwa hujui kuliko kuanza kujifanya na wewe much know.
Nilipokuwa nafanya PhD niliendelea kumsikiliza Prof bila kumbishia ila tu nilikuwa natoa maoni kwanini isiwe hivi, na Prof alikuwa anajibu na kuonyesha njia.
Nawaomba watanzania wenzangu wajue Dr. Magufuli sio Dr wa kuchoma sindano, au Dr wa kupewa, ni PhD holder. Huwezi ukamyumbisha kijinga kijinga.
Ujue watu kama hawa waliosoma hawayumbishwi kijinga, huwa hawatetemeshwi na nyau.
Angalia hata Prof Muhongo, huwezi ukamshake kwa maneno yako yasiokuwa na kichwa au miguu. Hata wazungu wanajua kwamba tunaenda kuonana na mtu msomi sio yes man.
Zamani akija mzungu tu wizarani, utasikia waziri, ee tujiandae kwa mapokezi maalumu. Hayo yamepitwa na wakati kwa serikali yenye wasomi kama ya JPM.
Watu walikuwa wanakuja na begi tu eti anataka kuwekeza na walikuwa wanakubaliwa ila angalia sasa hivi hawaji, wameshasoma upepo.
Sasa watanzania tubadilike, Rais akija kwako akibaini kuna makosa, kubali halafu badilika, sio kujitetea. Hii inatuonyesha hufai maana hujui unacho kifanya.
Muungwana anakubali na anabadilika.