Rais ajaye ayajue haya

BWANANDUGU

Member
Jan 1, 2014
28
0
Heri ya Mwaka Mpya. Naependa kujadili kidogo mambo ambayo rais ajaye anapaswa kuyafahamu kabla hajaja kutuomba ridhaa ya kutuongoza.

Mambo hayo ni haya;

1.Ajue kuwa vijana wamepuuzwa na kudharauliwa ndani ya nchi yao.Wamefanywa kama daraja la wazee kuyafikia mema huku vjana wakibaki kuwa washangiliaji wa jinsi wazee wanavyotanua.

2.Afahamu kuwa huduma za afya ni mbovu,wajawazito wanalala chini tena wawili kwenye kidoro kimoja.

3.Ajue kuwa nchi hii sasa RUSHWA ni sehemu ya maisha,bila kutoa hupati huduma.Mtoaji na mpokeaji ckuhizi ni marafiki wakubwa hivyo ajipange kuufuta urafiki huo.

5.Ajue kuwa uchumi wetu unachezewa na wajinga wachache,kuna noti 2 kwenye mzunguko fedha ndani ya nchi moja.

Ajue kuwa hauna kitu cha sh.60 dukani kwa sababu hakuna sh.10 hivyo kumfanya masikini kunua vitu vya sh.60 kwa sh.100. 6.Ajue kuwa wabunge wetu huwa hawana akili mpaka wakumbushwe.

Hii ndio sababu wakapandisha bei ya mufuta ya taa ili kudhibiti uchakachuaji badala ya kutunga sheria kali za kuwabana wachakachuaji.

MWISHO Rais ajaye aweze kutuambia anaenda Ikulu kufanya nini?,kuongoza au kutawala?
 

mwahaja

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
387
225
Na bei mpy za umeme ni tatizo kubwa,kuna haja ya wananchi kuchukua hatua za dharura haraka iwezekanavyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom