Rais ajaye akerwe na udini kwa vitendo

Dini/iman haikuwahi na haiwezi kuwa identity ya mtu hata kidogo. Kitendo cha kusimamia misingi ya imani /dini katika taifa ni sehemu ya madhaifu ya hao tuliowapa mamlaka.....

Aisee huwa nachukia sana kuona viongozi wetu wanendekeza huu utomvu wa nidhamu katika ofisi ya jumuiya.....

Kuna siku niliona aibu sana askari walikuwa wamekaa pamoja wanakemea ndani ya kituo cha polisi..... Ile kitu sikuipenda hata kidogo....

Pia kuna askari m'moja nadhani kwa sasa amefariki, MUNGU amrehemu..... Alikuwa anapiga kaswida huku kavaa jezi za jeshi la polisi.... Aisee nilisikia fedheha kubwa sana...

Kuwa tunawafunza nini watoto wetu.... Hiki wanachokiona kwetu ndicho watakuja kukirudia na kitawaletea mitafaruku mikubwa sana.....

Ni marufuku kufanya siasa na shughuli za kiserikali zenye mlengo wa kidini, kiimani, kikabila au rangi.... Sio vizuri
 
Umesema vyema lakini hapo kwenye kiti Moto ni kama vile hiyo ndo sababu Prof Assad alitumbuliwa kwasababu hatafuni yule mdudu pendwa!
 
Watu ni wagumu sana kuelewa, yaani inakera sana.
 
Umesema vyema lakini hapo kwenye kiti Moto ni kama vile hiyo ndo sababu Prof Assad alitumbuliwa kwasababu hatafuni yule mdudu pendwa!
Yaani saga la Prof Assad tulilishuhidia mwanzo Hadi mwisho, kuita Bunge dhaifu, Bifu na Ndugai likafuatia, Magufuli akamuondoa na kumpiga vijembe, hapa Dini iliingiaje?
 
Sio kweli.

Nyie Wakristo tokea zamani sana mnatumia mbinu za kiharamu mpaka mnafoji mashahada mnakula rushwa... Nk, ndio maana tz haiendelei.
Basi Zanzibar ingetakiwa iwe imeendelea sana, Kama tatizo la Tz Ni Wakristo
 
Umeongea vizuri comrade, hii mijamaa haitaacha kulalamika mpaka kiama nikikumbuka nilivyo struggle toka mdogo kijijini sina ndugu kigogo au mwenye fedha nikapata kaajira halafu kuna jitu linasema hii nchi ina upendeleo wa kidini nabaki nashangaa kama jitu lina akili timamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
professionalism kivepee? walioajiriwa, wenye profession ndio mafisadi, ndio wala rushwa, na ndio watunga sera mbovu kwa manufaa ya kikundi fulani. Kwahiyo wewe unaona mafisadi, wala rushwa na watunga sera mbovu wawe wa jamii moja pendwa?
So kama wataalamu ni wezi na wala rushwa serikali iajiri kwa kigezo cha dini? Mbona hata misikitini na makanisani kuna makasisi, mashek wala rushwa, wezi na wazizi!!
 
Sasa ilunga chuki gani alie sema zaidi kusema ukweli kuhusu nchi hii inavyoendeshwa chini ya kanisa kama vipi tafuta lukuvi alisema nini kanisani kuhusu zanzibar na muungano ndio utajua kama wakiristo wanaleta chuki au laa
 

Huwezi kuelewa machungu ya waislamu kwa sababu mfumo una kufavour, utawafavour na watoto wako na wajukuu wako.
Kwa rekodi nchini zilivyo, ni rahisi mkiristo kuitwa kwenye interview, kupata ajira na kuteuliwa nafasi za juu kuliko muislamu.

Leo kwenye utumishi wa umma waislamu ni wachache mno, uchache huo unashtua.
Ni lazima hili suala litafutiwe suluhisho la sivyo hili ni bomu linalosubiri kulipuka!
 
Sio kweli, kwamba elimu za waislam ni ndogo, ishu hata kudahiliwa huko unakokusemea kuna upendeleo
 
So kama wataalamu ni wezi na wala rushwa serikali iajiri kwa kigezo cha dini? Mbona hata misikitini na makanisani kuna makasisi, mashek wala rushwa, wezi na wazizi!!
Kumbe unaitetea rushwa?
Basi itakuwa na wewe ni miongoni mwa wala rushwa
 
Basi Zanzibar ingetakiwa iwe imeendelea sana, Kama tatizo la Tz Ni Wakristo
Itaendeleaje na nyie wakristo wa bara ndio mlioitawala Zanzibar?

Mkitaka Tanzania iendelee acheni kula Rushwa, ubaguzi, ufisadi na acheni maovu yote... ndio TZ itaendelea

Mkiendelea kujifanya wajuaji kuliko Mungu aliyowaumba, TZ itaendelea kubaki nyuma na umasikini utaendelea mpaka siku ya kiyama
 
Mzee mbona mikoa yenye Waislam wengi ndio Ni masikini kuliko yote? mikoa Kama Lindi, Pwani, Mtwara ?
 
Kweli wewe ni bomu la taifa,sasa kwa taarifa yako nchi hii haijafika huko unakosema mimi pamoja na marafiki zangu wa Islamu tuliajiriwa miaka ya nyuma kidogo na ninaamini tulichaguliwa kwa rehema za Mungu,sifa zilizohitajika na uhitaji wa serikali kwani kwasasa nina wadogo zangu ambao hawajaajiriwa lakini silaumu mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

sasa ulidhani tukisema waislamu wanabaguliwa kwenye ajira tunamaanisha wapo 0% kwenye utumishi wa umma na serikalini? - Tunamaanisha wako Kidogo mno mpaka inaleta maswali mengi yasiyo na majibu.

Why Muslims are so few in public service?
 
sasa ulidhani tukisema waislamu wanabaguliwa kwenye ajira tunamaanisha wapo 0% kwenye utumishi wa umma na serikalini? - Tunamaanisha wako Kidogo mno mpaka inaleta maswali mengi yasiyo na majibu.

Why Muslims are so few in public service?
Kwa takwimu zipi ulizonazo,wapi muislamu mwenye sifa ya kuajiriwa aliachwa kwasababu ya dini yake au upo hapa kwaajiri ya kulaumu tu,tukianza na wewe mwenyewe CV yako ipoje mpaka unaachwa na Wakristo wanapendelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa takwimu zipi ulizonazo,wapi muislamu mwenye sifa ya kuajiriwa aliachwa kwasababu ya dini yake au upo hapa kwaajiri ya kulaumu tu,tukianza na wewe mwenyewe CV yako ipoje mpaka unaachwa na Wakristo wanapendelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Anza na teuzi tu za awamu hii kisha ulete majibu kwa nini teuzi zinanuka udini?
Kwa nini waislamu wanaoteuliwa ni wachache wakati wenye elimu hadi PhD na vigezo vingine mamlaka za uteuzi haziwaoni zinaona Wakiristu kwa wingi kupita kiasi kuliko waislamu?
 
Shida sio nani anateuliwa wapi Bali shida ziko 2. Ya kwanza Ni maamuzi yanayofanywa na walioteuliwa/kuajiriwa yanayowaathiri jamii iliyoachwa kwenye teuzi, pili Ni uwekezaji unaofanywa na walioteuliwa/ajiriwa kwa kutumia mishahara, posho na urahisi wa kukooa mikopo ujiwa muajiriwa
 
Huu ndio wimbo wenu miaka yote,ndio maana hutasikia mkristo analalamika pindi marais waislamu wanapoongoza, kwasababu hatuamini kama wanaoteuliwa wanateuliwa kwa udini bali kwa uwezo wao zamu ikifika yeyote anaweza pata nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…