Rais Abdulaye Wade wa Senegal akubali kushindwa!

Rais Abdulaye Wade wa Senegal akubali kushindwa!

Maverick

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2008
Posts
308
Reaction score
11
Rais wa Senegal Abdulaye Wade amekubali matokeo katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa urais. Wade ambaye ana miaka zaidi ya 80 alibadili katiba ili aweze kugombea mara ya tatu.
 
Safi sana hichi kibabu hadi kinakera kilivyokuwa kinang'ang'ana kubaki ikulu.
 
Habari zilizotufikia ni kwamba rais babu king'ang'anizi wa Senegal Abdulaye Wade ameshindwa vibaya na mpinzani wake Mecky Sall kwenye marudio ya uchaguzi uliofanyika leo. Wade alionywa asigombee kipindi cha tatu kinyume cha katiba lakini alikataa. Sasa amefurushwa kwa aibu na zomeazomea.

Kwa mara nyingine chama tawala kimfurushwa madarakani kwa amani kupitia sanduku la kura.

Hata hivyo Wade ameonyesha ukomavu wa kisiasa kukubali kushindwa tofauti na vibabu kama Mwai Kibaki wa Kenya na Robert Mugabe wa Zimbabwe. Alluta Continua Afrika kunazidi kucha.
 
Karibu kijiweni Abdulaye Wade and RIP the rest of your power struggle
 
Bado chama cha magamba.....
Kwani magamba wamekuambia wanampango wa kushindwa? Hata Arumeru wanadai watashinda! Hata wasingeweka mgombea watashinda na utashangaa tayari wana kura asilimia 72! Hawa jamaa achana nao... Hata ufanyeje wao ni washindi tu hata kwa kutumia mashetani kuwapigia kura!
 
hakuna mtu ana mpango wa kushindwa au anajiandaa kushindwa!!! kura ndio zinasema nani kashinda nani kashindwa!! nadhani hii asilimilia umekosea mimi nahisi wana 27%
 
Kwani magamba wamekuambia wanampango wa kushindwa? Hata Arumeru wanadai watashinda! Hata wasingeweka mgombea watashinda na utashangaa tayari wana kura asilimia 72! Hawa jamaa achana nao... Hata ufanyeje wao ni washindi tu hata kwa kutumia mashetani kuwapigia kura!

Hata Mwigulu amejitapa tarehe moja Sioi bungeni bila aibu kabisa JF!!!!! Kuwa shabiki wa CCM Arumeru kunahitaji roho ngumu sana.
 
Senegal ni mfano mzuri Afrika, hata Wade mwenyewe alikuwa mpinzani akamng'oa mwenzie. Akatamani kufunga mlango alioingilia, poor him.

Hiki Chama Dikteta cha hapa kwetu mwisho wake umefika. Wakajipange upya.
 
Hongera Senegal kwa Demokrasia nzuri huo ni mfano mzuri wa kuigwa, kwa hapa kwetu wakuu ngojeeni mpaka Mwaka 2015 msipayuke payuke ovyo tu pasipo na sababu tusubiri Mechi yetu ya fainali Mwaka 2015 mwamuzi wa mwisho ni

hakim na hakim wetu ni sisi wenyewe wananchi tutakao chaguwa Kiongozi anayeweza kutufaa kutuongoza nawapa hongera tena Wa Senegal.
 
......Hata hivyo Wade ameonyesha ukomavu wa kisiasa kukubali kushindwa tofauti na vibabu kama Mwai Kibaki wa Kenya na Robert Mugabe wa Zimbabwe. Alluta Continua Afrika kunazidi kucha.

Kwa hilo Babu kanifurahisha ingawaje kulikuwa hakuna haja ya yeye kugombania mara ya tatu. Na kikubwa zaidi kampigia simu na kumpongeza Macky Sall.
 
Back
Top Bottom