Raia wa nje wanaongoza jinai Tanzania

Mkata Mtaa

Senior Member
Jun 10, 2016
136
141
Nilifanya utafiti wangu kupitia magazeti ya kampuni mbili tu kwa miezi mitano, nilikuja kugundua raia wa nje wanaongoza kwa kufanya jinai ni hawa chini hizi ni habari zilizoripotiwa tu na vyombo viwili tu

1.Mchina afikishwa kortini kwa kukwepa kulipa kodi mwenye kampuni ya HM Textile Co Ltd iliyopo mtaa wa Agrey kariakoo, Hui Fang Ma, aukumiwa kwenda jera miaka miwili au kulipa faini ya milione nne, alipa faini. Mwananchi 23/03/16.

2. Wachina wafikishwa kortini kwa kukwepa kulipa kodi, Liu Song Yue, Liu Peng Fey na Jiang Zendog wenye duka lilipo Tabata, wahukumiwa kwenda jera miezi sita au kulipa faini ya milioni nne, walipa faini. Mwananchi 12/4/16.

3. Mkuu wa mkoa Morogoro kaka kakamata wachina wawili kwa kuendesha mgodi wa Marumaru kinyume na sheria na kukwepa kulipa kodi ya milioni tisini na mbili mil 92, cha Zhan Fa construction material Group Ltd. Mwananchi 17/4/16.

4. Mchina Bui Hao jera miaka ishirini kwa kukutwa na meno ya simba na kucha. Tanzania Daima, 20/4/16.

5. Wachina wawili wafikishwa mahakamani kwa kukwepa kulipa kodi, wenye kampuni ya Dong Shen International mtaa wa Narung'ombe Kariakoo. Pai Shu Chea na Apple Chen, wahukumiwa kwenda jera miaka mitatu au kulipa faini milioni mbili kila mmoja, walipa faini, Mwananchi 20/4/16.

6. Wafanyakazi wa Kampuni ya China Railway Jiangchan Engineering Ltd (CRJE) wanaojenga Hoteli ya NSSF Mwanza wagoma kwa kulipwa pesa pungufu na kunyanyaswa. Tanzania Daima 15/4/16.

7. Jumuia ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) yalalamika kuhusu wafanyabiashara wa kichina Kariakoo. Mwananchi 14/4/16.

8. Wachina mbaroni kwa kutaka kutorosha noti za mia tano zenye thamani ya milioni therathini, noti sitini elfu (60,000) Su Ning na Feng Guang Quan. Mwananchi 31/3/16.

9. Wachina wanaofanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (Chinese medical team) wanaswa wamejiunganishia maji ya DAWASA Oysterbay mtaa wa Mtwara. Watozwa faini ya milioni kumi na saba, (17) wanatakiwa kulipa faini ndani ya kipindi cha miezi ishirini na nne, (miaka miwili) Tanzania Daima 21/3/16.

10. Wachina wawili Xu Fujie na Huang Gin waliyokamatwa na meno ya Tembo mia mbili ishirini na sita (226) wafungwa jera miaka therathini au kulipa faini bilioni mia moja na nane (208) waenda jera, Mwananchi 9/3/16.

11. vigogo laki tatu (300,000) wa chama cha kikomunisti China (CCP) kinachotawala China wafungwa kwa ufisadi. Mwananchi 9/3/16.

12. STAMICO yaingilia mgogoro wa wachina na wafanyakazi wake kuhusu mikataba na maslahi ya wafanyakazi wa kampuni ya China Civil Engineering construction corporation, wanaofanya kazi hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananchi 1/3/16.

13. kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism development Ltd ambayo ni waagizaji wa pikipiki aina ya Falcon. Wakamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutengeneza namba za pikipiki na magari bila kuwa na kibali cha TRA cha kufanya hiyo kazi kinyume cha cha sheria, mkurugenzi mkuu Donglinh Guo, meneja wake Yong quing Chen na mtunza stoo Peng Zhan. Waleta fujo wakati wa kukamatwa kwao. Tanzania Daima 9/2/16.

14. Wafanyakazi wa kampuni ya Ocean kiss walalamika kwa kupata mshahara mdogo, kunyanyaswa na kukatwa mishahara elfu ishirini wanapochelewa. Tanzania Daima 9/2/16.

15. Wafanyakazi zaidi ya mia mbili (200) wa kampuni ya China railway Jiangchang engineering (CRJE) wanaofanya mradi wa daraja la kigamboni wagoma kwa kupunjwa stahiki zao. Tanzania Daima 16/2/16.

16. Wachina kumi na sita (16) wakamatwa Geita wakiwa wanachimba madini na viza ya utalii, Mwananchi 18/2/16.

17. Wafanyakazi mia mbili (200) wa Chima Hainan International Co. (CHICO) wanaotengeneza barabara ya Kyaka - Bunene. Wagoma walipwe malimbikizo yao ya mishahara na kunyanyaswa. Mwananchi 6/3/16.

18. Kampuni ya Kichina StarTime inayojishughulisha na huduma za vigamuzi yakamatwa na simu elfu mbili mia saba orobaini na nne, (2744) zisizo lipiwa kodi. Mwananchi 3/2/16.

19. China ni kinara wa wahamiaji haramu nchini, wakamatwa mia mbili themanini na tano kwa siku sita tu. (6) Kuanzia February 8-14. mwananchi 25/1/16.

20. Wachina wanaswa wakiiba maji, ni kampuni ya Allied Transportation inayotengeneza mabati iliyoko maeneo ya Buguruni. Tanzania Daima 25/1/16.

21. Polisi wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wanamlinda raia wa china mwenye kiwanda cha Mega copper anayefyatua risasi hovyo kutisha wananchi. Mwananchi 20/1/16.

22. Wafanyakazi wa mia tatu na sitini (360) wa kichina wa kiwanda cha Dangote Mtwara wakamatwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini. Mwananchi 10/1/16.

23. Naibu waziri wa mazingira afuta kibali cha kiwanda cha Dhahabu Mbeya cha Sunshine Mining cha wachina kwa kushindwa kutimiza vigezo na kuchafua mazingira kwa kiasi kikubwa. Mwananchi 10/1/16.

24. Mchina mbaroni kwa kukutwa na meno ya Ngiri uwanja wa ndege Dar es salaam, Mwananchi 5/5/16.

25. Naibu waziri afungu kiwanda cha S & Y Co. Kutokana na mazingira' kutokuwa salama na kuwa na wafanyakazi wengi wasiokuwa na vibali zaidi ya kumi (10) cha kutengeneza mbao nyepesi, Mwananchi 7/5/16.

26. Kiwanda cha sunshine Industry cha Dodoma kinachozalisha mafuta ya Alizeti kina wafanyakazi wengi ambao hawana vibali vya kufanya kazi nchini. 7/5/16.
 
ni porini pekee ndo wanyama wanaishi bila ya utaratibu simba anaweza kuja kwenye kundi la nyumbu na kumchukua mmoja na kumtafuna na wengine wala hawajiulizi hv kesho simba huyu akisikia njaa atakuja kumchukua nani ??? ni Africa tu ambae watu wake wana worry about today future wanamwachia mungu

ni Africa tu ndo mtu anaweza kuja na kufanya chochote na wala asichukuliwe hatua yeyote ni Africa tu ndo natural resources zote ni mali za wawekezaji na mzawa ni mtumwa sioni tofauti na nyani na sokwe kwa muonekano wao wa kidogo kufanana na binadamu tulitegemea ndo wangekuwa kings of jangle lakini crown ilo linashikiliwa na simba na wanyama wengine pamoja na kufanana na kinadamu kwa mbaali tulitegemea wangekuwa na maisha bora kuliko viumbe wengine wote porini lakini wameshindwa hata kujenga nyumba ya nyasi kujikinga na mvua wamezidiwa akili na ndege wenye chumba na sebule juu ya mti

ni watu weusi pekee ndo linalowapata weusi wenzao hujifanya wana hisia sana na kupost na kutukana lakini hawachukui hatua ku make sure this is not happen again kwa mwenzao tena je kuna tofauti gani na wale nyumbu porini wanao tafunwa na simba porini wameshindwa kutumia wingi wao ku make sure jambo ilo alitokei kwa mwenzao mwingne Leo simba wangekuwa wanakula majani kama wao wangechukua hatua
 
Kitu kinachosababisha waendelee kufanya makosa sababu ni kupigwa faini kidogo na rushwa iliyokuwa kubwa Nchini,
Nchi nyingine mgeni ukifanya kosa ni faini kubwa au kifungo baada ya hapo ni kurudishwa kwenu na utakiwi kurudi tena.
Ili kukomesha hii tabia lazima tutunge sheria kali kwa wageni kama nchi nyingine zinavyofanya.

Ata kuanzia ngazi ya familia tu mtu ambaye anaweza kuvumiliwa na mtoto wa nyumbani tu kama ana tabia mbaya sio mgeni wa kukaribishwa, tabia mbaya kafanyie kwenu si kwa watu, Nashangaa ata Balozi wao sijui haoni watu wake wanavyojihusisha na uharifu sana ua anaona lakini anafumbia macho na uwa anakutana raia wake mara kwa mara na wanajumuia zao hapa Tanzania.
 
Sio wawekezaji bali waporaji na wahuni wana tabia chafu ila kwa watu wenye uelewa mdogo wanawaona kama wawekezaji
 
Wanajua waliuziwa tanzania na watu wake kwa thamani ya mtu mmoja, hivyo serikali haiwezi kuwatetea raia wake. Si kama hivi hapa chini.

Mchina anaua kijana wa Kitanzania kwa sababu tu wame voice up kwa nyongeza ya malipo!


imageuploadedbyjamiiforums1469254304-125360-jpg.370230imageuploadedbyjamiiforums1469254317-258743-jpg.370231imageuploadedbyjamiiforums1469254327-688071-jpg.370232Kijana amuawa.

Serikali inalinda wachina, eti wawekezaji!

Ninadhani kuna kila sababu sasa ya Wananchi kuchukua jukumu la kujiilinda dhidi ya hawa wewekezaji wa ccm!. Wanatumaliza. Hawa wachina wanaona namna serikali haiko na Wananchi na ndiyo sababu wanafanya watakayo. Ni wapi duniani itokee hivi halafu kimdudu cha kichina kibaki kinaonekana mitaani?
 
Ngoja tuone hii serikali itawachukulia hatua gani maana serikali iliyopita hawa watu walishaota pembe, hii post ilichukuliwa kwenye gazeti mbili tu kati magazeti yote nchini haijumulishwi na vyombo vingine kama radio na Tv, na ndio iliripotiwa kuna habari nyingi haziripotiwa, unaweza kuona mwenyewe kwa jinsi wanavyofanya makosa mengi, serikali inatakiwa iamke na kuangalia kwa jicho la pili.
 
Back
Top Bottom