Raia wa China kizimbani kwa nyara za mamilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia wa China kizimbani kwa nyara za mamilioni

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 11, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Raia wa China kizimbani kwa nyara za mamilioni

  Imeandikwa na Flora Mwakasala; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:26 Imesomwa na watu: 125; Jumla ya maoni: 0
  RAIA wa China, Li Guibang (42) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matano likiwemo la kusafirisha nyara za serikali zenye thamani ya Sh milioni 165.5.

  Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali, Zuberi Mkakati alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mwaka juzi Dar es Salaam na Zanzibar.

  Katika shitaka la kwanza, ilidaiwa kati ya Juni 19 na Agosti 21 mwaka juzi, mshitakiwa alikamatwa akiwa na kilo 2,005.6 za pembe za ndovu zenye thamani ya Sh milioni 165.5 bila kuwa na leseni.

  Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa kati ya Mei 9 na Juni 9 mwaka juzi, mshitakiwa alikamatwa akisafirisha nyara hizo kinyume cha sheria kwenda kwenye kampuni ya Hong Kong Investment and Trading iliyopo Vietnam.

  Ilidaiwa pia kuwa mshitakiwa alisafirisha nyara hizo kwenda kwenye kampuni ya Hai Phong Investment bila ya kuwa na kibali.

  Wakili Mkakati alidai kuwa katika shitaka la nne mshitakiwa alisafirisha na kuuza nyara za serikali nje ya nchi bila kuwa na kibali.

  Mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kurudishwa rumande hadi Januari 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Wachina sasa siyo wakomunisti tena........................ila ni mabepari tu kama nchi nyinginezo...............
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Kwa bongo yetu hii wala sitashangaa akiachiwa huru huyu bwana!
   
 4. P

  Percival JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,568
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Muachie huyu mchina hana makosa. Mpeleke mahakamani huyo mhusika serikalini aliezitoa hizo pempe kwa huyu mchina.

  Kwanza huyi mchina alikamatwa mwaka juzi na na hizo pembe na leo 2011 ndio anapelekwa mahakamani. Sababu tutambiwa uchunguzi ulikua unaendelea - lakini wote tunaju kuwa muda wote huo huyu jamaa alikua anatolewa pesa na labda sasa ameishiwa.

  Pia kuna mambo mengi hayaeleweki kwenye statement hizo hapo juu
  "
  Katika shitaka la kwanza, ilidaiwa kati ya Juni 19 na Agosti 21 mwaka juzi, mshitakiwa alikamatwa akiwa na kilo 2,005.6 za pembe za ndovu zenye thamani ya Sh milioni 165.5 bila kuwa na leseni.

  Vipi mtu atakamatwa kati ya juni 19 na agosti 21. Mtu anakamatwa tarehe moja na saa moja na dakika moja sio baina ya tarehe hii na hii.

  "Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa kati ya Mei 9 na Juni 9 mwaka juzi, mshitakiwa alikamatwa akisafirisha nyara hizo kinyume cha sheria kwenda kwenye kampuni ya Hong Kong Investment and Trading iliyopo Vietnam. "

  Pia huyu mshtakiwa alikamatwa akisafirisha hizo nyara baina mei na juni !! Angalia hizo statement mbili hapo juu - huyu mshtumiwa alikamatwa akisafirisha hizo nyara Mei 9 na Juni 9 mwaka juzi hiyo nikabla ya siku aliokamatwa nazo hizo nyara Juni 19 na Agosti 21 !!
   
Loading...