Rai yangu kwa waumini: Kauli za viongozi wetu wa dini tuchanganye na akili zetu

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,474
2,648
Wasalaam, Leo viongozi wetu wa dini wametoa maono hatujui kama yametoka kwa mungu au kwa shetani kikubwa ni ushauri waliotupatia watanzania kwamba tuwapuuze vyama vya upinzani hasa vile 7 vilivyosusia uchaguzi wa Nov 24 na kwamba tukapige kura kwa wingi kuipigia CCM ili hali CCM wenyewe wameshashinda kwa kishindo 95% hawana mpinzani.

Vile vile viongozi wetu wamewashangaa wanaomnanga Rais wetu kwamba ni dicteta ili hali mh Rais wetu ni mwanademokrasia ndio maana tupo huru hadi Leo, wameongelea zaidi Uhuru wa kuabudu hivyo viongozi wetu wametuomba tumuunge mkono Rais wetu.

Hizi ni nasaha inawezeka vitabu vya dini vinaelekeza hivyo ya kwamba mamlaka yote duniani yàtoka kwa mungu, hivyo uwepo wa Rais wetu wa sasa inawezekana ni mpango wa mungu kwa maana Rais Magufuli amefanya makubwa ndani ya muda mfupi kabisa.

Tutafakari tukapige kura hiyo Nov 24.
Mungu ibariki Tanzanià.
 
Jana askofu kawapa neno la uzima mkatubu tu ,mtapambana na kila taasisis kwa ujinga wenu

Mungu amemtuma askofu awasaidie mbele ya kanisa ujinga utapingwa sana

State agent
 
Sisi kama wanasiasa wanaharakati tuliwataka watoke waseme, nao wameitikia wito wametoka na wamesema. Kazi kwetu kusuka au kunyoa!!
 
Hawa viongozi wa dini wanafurahia hii hali ya watu kuwa ktk "vita isiyotumia silaha". Kwamba kuna utulivu wa nje lkn siyo wa kiakili na kisaikolojia miongoni mwa waumini wao.

Utulivu huu una faida sana kwa hawa viongozi wa dini, kwasabb kila jumapili wao hupata sadaka. Hata hawajali umeipata kwa shida kiasi gani hiyo sadaka
 
Hawa viongozi wa dini wanafurahia hii hali ya watu kuwa ktk "vita isiyotumia silaha". Kwamba kuna utulivu wa nje lkn siyo wa kiakili na kisaikolojia miongoni mwa waumini wao.

Utulivu huu una faida sana kwa hawa viongozi wa dini, kwasabb kila jumapili wao hupata sadaka. Hata hawajali umeupataje hiyo sadaka
Ki ukweli sijaelewa
 
Hawa viongozi wa dini wanafurahia hii hali ya watu kuwa ktk "vita isiyotumia silaha". Kwamba kuna utulivu wa nje lkn siyo wa kiakili na kisaikolojia miongoni mwa waumini wao.

Utulivu huu una faida sana kwa hawa viongozi wa dini, kwasabb kila jumapili wao hupata sadaka. Hata hawajali umeipata kwa shida kiasi gani hiyo sadaka
Mkuu taratibu usikufuru
 
Kwa taarifa yako kila kitu kimeshawekwa mfukoni kuanzia mihimili hadi viongozi wa dini!
 
Mimi nilishaacha kuchanganya zao na zangu, bali kwa sasa za kwao nazitupilia mbali na ninabaki na za kwangu tu.
 
Back
Top Bottom