Ivi kwa nn huyu jamaa anaukomalia sana U-Rais? Hana shughuli nyingine zenye utukufu anazoweza kufanya akatambulika duniani kote? Reginald Mengi yuko pale, kwa nn hamfuati na kuiga mifano yake. Na hawa ndugu zetu wa magazeti kila kukicha ni habari ya Lowasa, Lowasa, Lowasa. Na huyu Daktari(cjui wa nn) kaja na yake eti katumwa na watu wa mikoa sita ya kanda ya ziwa kumwaomba Lowasa agombee U-Rais, wamekutana wapi na lini. Lkn pia nina wasiwasi na akili za hao watu, mtu yuko katika kifungo cha siasa na hatma yake haijajulikana wao wanamtaka agombee U-Rais sawa sawa kweli. Mwanao yuko gerezani kafungwa wewe unamtafutia mchumba zinafanana? Jamani tuacheni tutulize akili zetu tumchague Rais bila shinikizo kutoka upande wo wote. Kama alivyosema Mh Rais kule Songea, mgombea U-Rais tunayemtaka bado hajajitokeza, Lowasa ameshajitokeza kiaina na ameshafanya sherehe kadhaa hasa pale aliposema "safari ya matumaini imeshaanza", je, huku si kujitokeza? Kwa hiyo hayumo katika wale tunaowataka. Ana uwezo mkubwa kipesa, ashauriwe anunue moja ya migodi iliyopo nchini ili wazawa wafaidike na rasilimali zao kwa asilimia moja CCM oyee!
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums