Rage na bastola, hakuna jipya

ShockStopper

Senior Member
Apr 10, 2009
124
56
Masanja Mkandamizaji kwa sasa anatamba na kibao chake kinachosema 'Hakuna jipya chini ya jua', inawezekana aliona mbali, hebu ngoja tujaribu kuangalia.
Kuna methali nyingi tu za kiswahili zina maana sana, wahenga waliziweka zitusaidie, ila tatizo tunazipuuza au tunazisahau mapema ndio maana tunaduwazwa na watu kupanda jukwaani wakiwa silaha. Moja ya methali hizo ni hizi hapa "Mtoto wa nyoka ni nyoka"; Ukipenda boga, penda na ua lake"; n.k.
Kutokana na methali hizo, kwa uchache tunaweza kupata kauli hizi, 'Mtoto wa haramia ni haramia'; 'Ukipenda msomali, penda na uharamia wake'. Kwa hiyo mimi simshangai Rage, ila nawashangaa wale waliomchagua. Sasa nawauliza ninyi mnaomshangaa na kumkasirikia Rage, mlikuwa wapi kuwashangaa na kuwasuta wananchi wa jimbo waliompa msomali ubunge, hivi mmasai akipanda na shuka jukwaani au akipanda na sime utashangaa? si anadumisha mila, mwacheni Rage adumishe mila yake. Hata kule Tarime watu walienda kwenye mkutano na mapanga mkafikiri wanamtisha Mbowe, kumbe kule wanaume hawatembei mikono mitupu. Hivi ukienda kuoa kule Somalia utadaiwa kupeleka mahari gani kama sio AK47? LOL! acheeni hizo!
Hata Biblia inalo la kusema kuhusu hili, inasema hivi katika Matayo 7:18
"Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mema"
Hivi mliao usipozaa machungwa utaulaamikia?

Iwapo kwa kelele hizo mmeshazinduka, basi msimpokonye Rage bastola yake, bali mnyimeni jukwaa 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom