Rage kugombea nafasi ya Dalali Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rage kugombea nafasi ya Dalali Simba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-bongo, Dec 23, 2009.

 1. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wana Jf nimeona nilete mjadala huu hapa Jamvini.
  Leo asubuhi nikiwa na kunywa chai Hapa Tabaora ktk Hoteli ya MEYA,kuliibuka mjadala juu ya Dhamira ya bwana Ismail Aden Rage juu ya yeye kugombea Uenyekiti wa Club ya Simba,mjadala huu ulikuwa mkubwa na watu kujadili je Rage anadhamira ya kweli kutaka nafasi hiyo?

  Wadau wa soka hapa wamekuwa kidoago na wasiwasi hasa baada ya wengi kuhusisha swala hili na Historia ya Rage ktk Soka na Siasa,Wanyamwezi hawa walikuwa wanajaribu kujenga hoja kuwa Rage anataka kutumia nafasi hiyo kujijenga kisiasa zaidi kwani wanadai kuwa 2000 alikuwa na Nguvu sana ktk Jimbo la Tabora,ana Rage alitumia Mali za FAT wakati huo kujijenga kisiasa,hapa inakumbukwa wanadai alitumia Fedha na Vifaa kujijengea uhalali wake ktk Siasa nadani jimbo la Tabora Mjini.

  Wana dai kuwa huyu jamaa atatumia klabu ya simba kujinufaisha zaidi binafsi kwani wanadai kuwa TAREFA chama cha mpira atabora kina kashafa kuwa FEDHA walizopewa kwa ajili ya TAIFA CUP Rage alitia Ndani sasa wengi wanadai hapa kuwa Rage atapoteza mafanikio ya Club ya simba walopata kwa kipindi hiki akichukua nafasi basi atatumia kwa maslahi binafsi kwani sasa hata chama cha Mpira hapa Tabora wanadai kina Mgogoro ambao ni ubadhirifu,wengine walidai kuwa Uchumi wa Rage umeyumba sana kwahiyo atatumia Club ya Simba kujiwezashe zaidi kuliko kuiwezesha Club.

  Walokuwa wanamuunga mkono wana dai Rage ni mwana Michezo na Anaipenda Simba hawezi kuihujumu.

  Lakini maswali makubwa ni Je RIKODI YA RAGE AKIWA KIONGOZI WA CLUB INAONYESHA MAFANIKIO?JE RAGE CRIMINAL RECORD YAKE HAIWEZI KUIATHIRI CLUB YA SIMBA INTERMS OF REPUTATION/LOCALLY NA INTERNATIONALLY?JE RAGE ANAMPANGO WA KUJINUFAISHA ECONOMICALLY NA POLITICALLY KUPITIA CLUB YA SIMBA?

  Nimeona nilete mjadala huu hapa tuujadili.
   
 2. J

  JOHN KITABI Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Nov 10, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  M-bongo,
  Naamini Meya ameimarisha huduma ya chakula zaidi kwa sasa hasa akizingatia kuwa anakaribia kuingia kwenye muongo mwingine na hata biashara zake zinahitaji kuwa za kisasa zaidi.
  Bwana Rage sina ukaribu nae sana. Nilishawahi kufanya kazi nae hapo Tabora akiwa kama Mwenyekiti wangu katika jumuiya ya wazazi CCM mkoa. na hata mwaka jana pia alirudishwa kwenye nafasi hiyo kwa mara nyingine. Ukimuangalia vizuri Rage nimekuwa nikimuona kama siasa ni kivuli tu. Namuona Rage kama anapenda kuongoza mpira kuliko siasa. Nafikiri hivyo. Sijamuona Rage kwa hivi karibuni akiwaza kugombea hata ubunge. Lakini yote mema. Mie namtakia kila la heri. Muache agombee simba, nafikiri kwa damu yenye mapinduzi ya mabadiliko nadhani atakuwa na changamoto kwa ajili ya kuiongoza simba. Kwa sasa viongozi wengi wanakabiliwa na changamoto kubwa moja kuwa watu wengi wanaoongozwa wana mawazo mengi ya mapinduzi ya mabadiliko.
  Kila la heri Rage
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  M-bongo chai ulinywea Meya ya sokoni au huku juu maktaba?? Kwa mtazamo wangu Rage kuongoza klabu kama Simba sioni kama atakuwa na jipya atakalopeleka pale. Nadhani wapenzi wa soka wanakumbuka vizuri alipokuwa katibu wa FAT jinsi ambavyo chombo hicho kilivyokuwa duni kiutendaji. Si ubaya na Rage na mimi ni mshabiki sana wa Simba lakini kiukweli kabisa klabu zetu Tanzania zinahitaji watu wenye mitazamo mipya ili kwanza klabu zenye ushindani kimataifa, klabu kuachana na mifumo ya kutegemea ufadhiri wa watu fulani na kwa kweli klabu zinahitaji sana kuwa financially stable!

  Rage amekuwa kiongozi wa mpira katika ngazi mbali mbali laiti angekuja kwangu kutaka ushauri wa kugombea au kutogombea ningempa jibu la pili. Kwa nini kwa muda aliokaa nje ya medani ya soka sioni kama atakuwa na jambo jipya. Lakini kwa kuwa anafahamu tabia za mashabiki wa Simba sitashangaa akigombea na hata akishinda. Mashabiki wa Simba na Yanga hawachagui kiongozi kwa kuangalia kitu gani kipya cha maendeleo ataleta klabuni ili mradi tu historia ikimlinda na akiwahakikishia kuwa siku ya mechi ya Simba na Yanga ataleta ushindi.

  Nadhani huu ni wakati sahihi watanzani wapenda soka tubadirike hasa unapofika muda muhimu kama wa uchaguzi. tuchague kiongozi ambaye kweli atafanya kitu zaidi ya kuifunga Simba au Yanga. Nadhani ndoto alizokuwa nazo aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga Abbas Tarimba kutaka kuifanya Yanga kampuni huenda ingetuonyesha mwanga wa nini tunatakiwa kufanya lakini kwa tabia za watu wetu kupenda kudumaa walimkwamisha na mwisho wanakubali kwenda kumpigia magoti Manji..eti mfadhili ujinga mkubwa kabisa.

  So kama mungu ataniweka hai hadi siku ya uchaguzi wa Simba nitashiriki nikiwa mwanachama hai kabisa na kama Rage atagombea mimi binafsi sitampa kura yangu.

  Hizi kelele za kumlaumu Maximo kila siku sijui kama hatujui uozo uko unaanzia wapi? Huwezi kuwa na timu imara na nzuri ya taifa kama chimbuko la wachezaji wa timu ya taifa yaani klabu zimeoza na hazina mipango endelevu ya kimpira..

  Tanzani tunahitaji mapinduzi ya kisoka ndio tupate mafanikio kinyume cha hapo naona tunamnyima bure Maximo ulaji maana hata akija Fabio Cappelo, Scolari au Marcelo Lippi hadithi itakuwa ile ile.....
   
Loading...