Rage: Hivi Haya Ni Kweli Jamani?

Rage: Hivi Haya Ni Kweli Jamani?

Mkuu ukifuatilia sana hilo utawapoteza watanzania wote waishio mipakani maana hivyo vizazi vikirudishwa nyuma wengine tutakua wa south africa bure.
 
Someni Haya maneno ya mzee John Kitime yanaweza kuwasaidia pa kuanzia kuhusu hUYU ADEN mnaembagua kutokana tu na rangi yake.......

Zamani wakati nasoma Tabora enzi zile za miaka ya sabini tulikuwa tunakwenda kuangalia mazoezi ya Segere Matata. Wakati ule watoto au wanafunzi hatukuruhusiwa kuingia Dansini hivyo mara nyingi kama kulikuwa na dansi tuliishia nje . tuliusikiliza muziki kwa nje na mara nyingi tulikaa katika baraza ya mama mmoja maarufu sana Tabora mama Adeni. Mama yake (Ismail Aden Rage huyu wa Moro star). Mama huyu alikuwa na Hoteli iliyoitwa Tanzania Hotel iliyokuwa mtaa wa Rufita. kwa wale wanaojua Tabora na hulka zake, katika hoteli ile kulikuwa na Baraza kubwa sana ya kahawa. Tanzania hoteli ilikuwa pua na mdomo kutoka Lumumba uliokuwa ukumbi wa Tabora Jazz-JOHN KITIME.
 
Hivi na mimi naweza kwenda Somalia/India nikakubalika mpaka kugombea uongozi?

Au mtoto nitakayemzaa Somalia/India atakubalika hivyo?

huko india ndio kabisa wewe n takataka zaidi hata ya wala ma-dalits na huko somalia ni wabaguzi ingawa ni waafrika hawa watu walistahili warudishwe kwao ila sisi wabantu kwa ulimbukeni wetu tunaona sifa sana kuji-associate na watu wasiokuwa jamii yetu ingawa ndio wabaya wetu!!tusiruhusu hawa watu wakapata uongozi ktk nchi yetu hata kama wana uraia wa hapa sisi ndio tunaojifanya hatuujui ule msamiati wa ubaguzi lkni walahi hawa wenzetu wanathubutu kutubagua ndani a nchi etu itakuwaje sasa ukiishi kwenye nchi yao??
 
Udini, ukabila, rangi ya mtu na ubaguzi wa kujumla wa binadamu, hautakiwi hapa Tanzania, mtanzania sio lazima awe mbantu wa Tanganyika, anaweza kuwa mweupe, mwarabu, msomali, mwanamke, shoga, mkristu au muislamu.

Hio ndio siri ya sisi wabongo kutokuwa na mavita ya kijinga kijinga mpaka leo, sijui wengine wataelewa haya lini....!
Tatizo tulilonalo baadhi yetu ni ufinyu wa kuelewa kwani kujua ASILI ya mtu sio UBAGUZI.
 
Mkuu ukifuatilia sana hilo utawapoteza watanzania wote waishio mipakani maana hivyo vizazi vikirudishwa nyuma wengine tutakua wa south africa bure.

ndivyo mnavyojidanganya hivyo hizo ni propaganda za wageni wa nchi hii kusema tukichunguzana wote tutakuwa wageni!! ina maana tanzania hii hakuna wenyeji??au huko nchi za jirani zetu kama zambia malawi msumbiji,kena na ethiopia hakuna watu wa mipakani waliochanganyika na wa2 wa nchi nyingine jirani??hizo ni mbinu za wageni feki kutuziba midomo tusiwanooshee vidole,zinduka
 
Huo uhusiano wa mama, baba, bibi, mmasai nk umenichanganya sana!
 
Someni Haya maneno ya mzee John Kitime yanaweza kuwasaidia pa kuanzia kuhusu hUYU ADEN mnaembagua kutokana tu na rangi yake.......

Zamani wakati nasoma Tabora enzi zile za miaka ya sabini tulikuwa tunakwenda kuangalia mazoezi ya Segere Matata. Wakati ule watoto au wanafunzi hatukuruhusiwa kuingia Dansini hivyo mara nyingi kama kulikuwa na dansi tuliishia nje . tuliusikiliza muziki kwa nje na mara nyingi tulikaa katika baraza ya mama mmoja maarufu sana Tabora mama Adeni. Mama yake (Ismail Aden Rage huyu wa Moro star). Mama huyu alikuwa na Hoteli iliyoitwa Tanzania Hotel iliyokuwa mtaa wa Rufita. kwa wale wanaojua Tabora na hulka zake, katika hoteli ile kulikuwa na Baraza kubwa sana ya kahawa. Tanzania hoteli ilikuwa pua na mdomo kutoka Lumumba uliokuwa ukumbi wa Tabora Jazz-JOHN KITIME.

Umejitutumua sana dada angu kim kumtetea bwana Rage, lakini ukweli unabaki pale pale huyu mamake rage alikuwa ni msomali sasa yeye anatudanganya kuwa ni mmasai ili atutawale vizuri hapa, na rage alizaliwa miaka hiyo ya 50s sio tabora bali arusha au nje ya Arusha kama vile somalia au kenya na hapo tabora walihamia tu rage akiwa tayari kashazaliwa sasa anatudanganya kazaliwa tabora!!

Ieleweke wasomali kwao ni somalia na hawana mapenzi ya kweli na nchi hii hata kidogo na ndio mana wanajitahidi kuwaingiza na wenzao kwa siri na kuiba mali zetu, somalia ikitulia watatuachia nchi yetu ikiwa haina kitu hta kidogo watarudi kwao.sio watu wazuri hata kidogo. Rage ni msomali aliezaliwa somalia.
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Wote wanaopinga hii hoja ya kuhoji uraia ni WAPAMBE wake, ndiyo maana wanataka nchi ishikwe na wakimbizi kama watz original hawana akili!! wanatoa povu kutetea bila sababu!!! kunaubaguzi gani hapo?

Kaburu ni kaburu haijalishi rangi yake ,ni upuuzi kubagua watu angalieni taifa kkama Marekani Obama hana asili ya hilo taifa lakini wamemchagua kuwa Rais huu ubaguzi wa kipuuzi tunautoa wapi ?
 
Kaburu ni kaburu haijalishi rangi yake ,ni upuuzi kubagua watu angalieni taifa kkama Marekani Obama hana asili ya hilo taifa lakini wamemchagua kuwa Rais huu ubaguzi wa kipuuzi tunautoa wapi ?
USA ni nchi tofauti. Ile ni nchi iliyojengwa na wahamiaji. Niambie UK, Germany, Italy, n.k.

Pia USA unapata nafasi kama aliyopata Obama kwa merit. Na Obama amewashinda wapinzani wake tukishuhudia.

Unataka kuniambia Rage ndie the smartest guy in Tabora? Pamoja na background yake ya kwenda jela n.k.? Au tunathamini mtu kwa pesa yake? Au Usomali wake ndio mtaji tusionekane tunambagua?

Usomali ni kitu kimoja, ebu nitajie kitu gani cha pekee kinachomfanya Rage awe mwakilishi bora au kiongozi bora?

Zamani walikuwepo akina Jamal, Al Noor Kassum, tuliwaona performance yao mbona hatukulalamika?
 
Nimemsikia mweshimiwa huyu kwamba eti yeye baba yake ni msomali na mama ake ni mmasai,na kwamba yeye kazaliwa Tabora mbaya zaidi anadai kuwa wakati mama yake rageh yuko kigoli alifiwa na mama yake yani bibi yake rageh mzaa mama na babu yake Rage akakataa kuoa mpaka mama yake rageh aolewe!! swali hivi hili linawezekana kweli kwa wamasai wenye kuoa wake wengi??

Mbaya zaidi mama ake Rage alilelewa na bibi ake aitwae bint ahmed hivi kuna wamasai waislamu kweli miaka hiyo ya 1950??mi naona historia hii ina walakini pili Rage anazungumza kisomali vizuri na hii haiwezekani mpaka baba na mama wawe wanaijua lugha hiyo au kama mzazi mmoja basi lazima atakuwa ni mama mana ndio anaeshinda na watoto,sasa anasema mama yake ni mmasai hivi kuna msomali miaka hiyo ya 50s aliweza kuoa mmasai kweli??mana mtu wa mwisho msomali kuoa ni msomali mwenzake kama akkosa mzungu au mhindi au mwarabu!!

Je Rage sasa hivi mke wake ni msomali au ni wa jamii gani?? Wajuzi mnaomjua vizuri tujuzeni tafadhali.

Mimi sina asili hata tone ya KIHINDI, lakini nazungumza URDU kushinda wahindi wa TZ, jee Usambaa wangu una utata. KUna Jamaa wa KI NGUU pale ilala, Baba na Mama wote ni wanguu, anazungumza kisomali utadhani katoka Hargeisa leo, JEE UU TZ wake unautata. Ndugu yangu Huna lolote la kusema, basi tuu tunawaonea wasomali sijui kwanini. Hutasikia hapa Jukwani wakisemwa Wabunge wa Kihindi,Kiarabu, chotara wa Kizungu nk. Bali wasomali tuu ambao nao ni wa Africa wenzetu.

Jamni Kasumba hii ya Ajabu, Tutazidi kufa masikini kwa kuoneana wivu
 
==================================================================================
Wacha Ujinga Kijana, Rage was the best of the LOT who stood with him for election, sasa kwanini kachaguliwa, kila tunaposhindwa na wenzetu tutasema katumia pesa. Very cheap excuse. Rage anakubalika Tabora, wala usitake kubisha. Na pia kuna huyo mjinga mwengine asemaye kila anayemtetea Rage ni mpambe wake, Thats too low for an Inteligent person to say, Tutawatetea wote wenye haki ambao wanonewa hapa JF, this is a congregation of the Inteligent, Fair and Democratic, nashindwa kujua nyie mnafanyanini humo, sipo kwenu.
 
wageni Tz wapo wengi sana na hata wengine wamekuwa kama wenyeji na hii ndiyo ilikuwa makosa ya Mwalimu
 
Wee kweli MENTALI! sasa huu utafiti wako utatusaidia nini? kama ni u-simba na u-yanga wako peleka huko kwingine hapa si mahalin pake, sikia meeen!!
Nimemsikia mweshimiwa huyu kwamba eti yeye baba yake ni msomali na mama ake ni mmasai,na kwamba yeye kazaliwa Tabora mbaya zaidi anadai kuwa wakati mama yake rageh yuko kigoli alifiwa na mama yake yani bibi yake rageh mzaa mama na babu yake Rage akakataa kuoa mpaka mama yake rageh aolewe!! swali hivi hili linawezekana kweli kwa wamasai wenye kuoa wake wengi??

Mbaya zaidi mama ake Rage alilelewa na bibi ake aitwae bint ahmed hivi kuna wamasai waislamu kweli miaka hiyo ya 1950??mi naona historia hii ina walakini pili Rage anazungumza kisomali vizuri na hii haiwezekani mpaka baba na mama wawe wanaijua lugha hiyo au kama mzazi mmoja basi lazima atakuwa ni mama mana ndio anaeshinda na watoto,sasa anasema mama yake ni mmasai hivi kuna msomali miaka hiyo ya 50s aliweza kuoa mmasai kweli??mana mtu wa mwisho msomali kuoa ni msomali mwenzake kama akkosa mzungu au mhindi au mwarabu!!

Je Rage sasa hivi mke wake ni msomali au ni wa jamii gani?? Wajuzi mnaomjua vizuri tujuzeni tafadhali.
 
Mimi sina asili hata tone ya KIHINDI, lakini nazungumza URDU kushinda wahindi wa TZ, jee Usambaa wangu una utata. KUna Jamaa wa KI NGUU pale ilala, Baba na Mama wote ni wanguu, anazungumza kisomali utadhani katoka Hargeisa leo, JEE UU TZ wake unautata. Ndugu yangu Huna lolote la kusema, basi tuu tunawaonea wasomali sijui kwanini. Hutasikia hapa Jukwani wakisemwa Wabunge wa Kihindi,Kiarabu, chotara wa Kizungu nk. Bali wasomali tuu ambao nao ni wa Africa wenzetu.
Jamni Kasumba hii ya Ajabu, Tutazidi kufa masikini kwa kuoneana wivu

wasambaa na wanguu na wazigua ni kabila moja hapo mwanzoni kabla hawajatengana ukienda huko somalia kuna wazigua au kwa jina jingine wanaitwa somali bantus hawa mabwana tangu waende somalia enzi hizo hadi leo hii hawajawahi kupewa uhuru wao wanaitwa tu abdi watumwa na wasomali na wanawaconsider ni wa lowest class huko somalia hadi leo hii, japokuwa hawa jamaa wazigua wa somalia wanaongea kisomali fasaha lakini wasomali wamekataa kuwaasimilate kuwa sehemu ya jamii yao,huu ni ubaguzi wa hali ya juu wale somali bantus japokuwa ni weusi na wengine walichanganika kidogo na wasomali bado wanachukuliwa kuwa ni wageni na watumwa hawaruhusiwi kufanya kazi yeyote ile ya heshima ndani a somalia wala kushika nyadhifa za kisiasa mana wao ni watumwa tu sasa nakushangaa wewe mwenzangu msambaa unaowatetea hawa wasomali ni kule kutaka kujifananisha nao na wewe wakuite msomali au ni ulimbukeni tu wa kutokujua?? huko tanga kikwete aliwarudisha wazigua wa somalia tanga mana waikuwa wananyanyasika sana kama vile siyo watu nao na hata ukienda kuwauliza watakwambia jinsi wasomali walivowatesa mana hadi leo pamoja na kukaa karne nyingi somalia hawakuruhusiwa hata kuoa binti wa kisomali wala wasomali ilikuwa nadra kuoa mbantu na wamerudi vile vile na rangi yao waliyoondoka nayo,lakini wasomali wakija bongo wanruhusiwa kuoa wabongo tena bila kelele zozote labda wasitake wao sasa kati a sisi na wao nani ni mbaguzi hapa??fikiri kabla hujakurupuka wacheni ile kasumba yenu kuwa wasambaa,wazigua na wanguu si wabantu bali ni waisrael kama mngekuwa hivyo wasomali wasingewabagua mana hao wasomali wenyewe wanawaabudu waarabu na wanabaguliwa na waarabu pia.!!!!!
 
Nashindwa kuelewa inakuwaje tuko dhaifu kimfumo na kisheria mpaka Rage na wenzake wakawa viongozi wakubwa.
So far ushahidi wa Bashe na Kinana umeonekana na kasoro nyingi za kimsingi.

So inawezekana Assad wa Syria akaja kuwa Rais hapa ikiwa watamtimua kule!
 
Wewe unajua ukiingiza kubaguana wengine watasema Wairaqw sio Watanzania kwa hiyo Dr Slaa arudi kwao
 
Kila kitu kinawezekana!. Nenda Arusha, mitaa yote mbele ya soko la Arusha ni nyumba za wasomali watupu!, wamezaliwa Arusha, wamekulia Arusha na watafia Arusha! ni Watanzania Wenzetu!.

Nenda umasaini eneo la Ngaramtoni, utashuhudia Wasomali pure, wanaongea Kimasai safi!, wamezaliwa umasaini, wamekulia umasaini na watafia umasaini, ni Watanzania wenzetu!.

Nenda uhindini, kuna watoto wamezaliwa uhindini, wamekulia uhindini lakini hawazungumzi Kiswahili ila ni Wanzania wenzetu!.

Rage ni Msomali Mtanzania mwenzetu!, Kinana ni Msomali Mtanzania mwenzetu na Bashe ni Msomali Mtanzania mwenzetu!. Tusiwasakame bure kutokana na rangi zao!, kuna Warundi, Waganda, Wakenya, Wanyarwanda, Wajaluo, Wazaire, Wamalawi, Wazambia, Wamsumbiji kibao wako kwenye madaraka makubwa serikalini tena wengine mpaka idara nyeti!, wamepose kama Watanzania, hatuwasakami kwa sababu tuu wamefanana na sisi!, kitendo cha kuwasakama Wasomali na Wahindi tuu, huu pia ni ubaguzi mbaya!.
Pasco.

MKUU Pasco!

Heshima kwako!

Hija hapa sio Msomali/ Mhindi kuzaliwa Umasaini, kukulia umasaini na kuzungumza kimasai fasaha, laa!!!! Unaweza kutimiza haya yote na bado kisheria hujakidhi vugezo vya kuwa raia wa Tanzania.

Kwani ni wahindi wangapi wamezaliwa hapa na wanaongea lugha za makabila ya ndani kabisa na bado si raia wa Tanzania!!!! Nikiwa na maana kwamba wana vitambulisho vya urai zaidi ya Utanzania, au hujui hilo? Wahindi wangapi wana uraia wa Kanada na bado ni raia wa Tanzania???? Au tulikuwa na Wanyaruanda wangapi jeshini ambao tulitambua kwamba ni raia wa Tanzania, na baada ya Kagame kuwa raisi Rwanda wote si walikimbia tena kwa kutoroka kurudi Rwanda na kuwa wanajeshi kule!!!!?

Kwa hali hiyo, mtu kuhuji uraia wa mtu kilingana na mashaka anayo yaona isiwe tabu Mkuu!!!!! Muhimu kama ni raia basi tujue vigezo vinavyo mfanya awe raia wa Tanzania. Hoja ya kusema kwamba tukianza kuhojiana huyu anatoka wapi, eti ni ubaguzi hiyo kwa ulimwengu wa sasa tunaita ni "HOJA MFU".

Mahali popote duniani utakapo kwenda, lazima serikali makini zitahiji uraia wako: Iwe ni raia wa nchi hiyo, lazima watahiji uraia wako tu. Kuhoji uraia wa mtu kwetu tunaona ni jambo la kibaguzi kwa sababu tumezoe ili mradi liende tu.
 
Back
Top Bottom