Mkuu kwani kuhoji uraia wa mtu ndiyo kumbagua?Ukiona wageni wanaingia nchini kinyume na taratibu za nchi na ukaamua kuhoji huo ni ubaguzi?Udini, ukabila, rangi ya mtu na ubaguzi wa kujumla wa binadamu, hautakiwi hapa Tanzania, mtanzania sio lazima awe mbantu wa Tanganyika, anaweza kuwa mweupe, mwarabu, msomali, mwanamke, shoga, mkristu au muislamu.
Hio ndio siri ya sisi wabongo kutokuwa na mavita ya kijinga kijinga mpaka leo, sijui wengine wataelewa haya lini....!
mke wake ni msomali pure namfahamu vzr sana alipokuwa anaishi pale samora avenue opposite na tanesco. Sijui kama wamehama.
Udini, ukabila, rangi ya mtu na ubaguzi wa kujumla wa binadamu, hautakiwi hapa Tanzania, mtanzania sio lazima awe mbantu wa Tanganyika, anaweza kuwa mweupe, mwarabu, msomali, mwanamke, shoga, mkristu au muislamu.
Hio ndio siri ya sisi wabongo kutokuwa na mavita ya kijinga kijinga mpaka leo, sijui wengine wataelewa haya lini....!
Nimemsikia mweshimiwa huyu kwamba eti yeye baba yake ni msomali na mama ake ni mmasai,na kwamba yeye kazaliwa Tabora mbaya zaidi anadai kuwa wakati mama yake rageh yuko kigoli alifiwa na mama yake yani bibi yake rageh mzaa mama na babu yake rage akakataa kuoa mpaka mama yake rageh aolewe!! swali hivi hili linawezekana kweli kwa wamasai wenye kuoa wake wengi??mbaya zaidi mama ake rage alilelewa na bibi ake aitwae bint ahmed hivi kuna wamasai waislamu kweli miaka hiyo ya 1950??mi naona historia hii ina walakini pili rage anazungumza kisomali vizuri na hii haiwezekani mpaka baba na mama wawe wanaijua lugha hiyo au kama mzazi mmoja basi lazima atakuwa ni mama mana ndio anaeshinda na watoto,sasa anasema mama yake ni mmasai hivi kuna msomali miaka hiyo ya 50s aliweza kuoa mmasai kweli??mana mtu wa mwisho msomali kuoa ni msomali mwenzake kama akkosa mzungu au mhindi au mwarabu!!Je Rage sasa hivi mke wake ni msomali au ni wa jamii gani??
Wajuzi mnaomjua vizuri tujuzeni tafadhali.
Udini, ukabila, rangi ya mtu na ubaguzi wa kujumla wa binadamu, hautakiwi hapa Tanzania, mtanzania sio lazima awe mbantu wa Tanganyika, anaweza kuwa mweupe, mwarabu, msomali, mwanamke, shoga, mkristu au muislamu.
Hio ndio siri ya sisi wabongo kutokuwa na mavita ya kijinga kijinga mpaka leo, sijui wengine wataelewa haya lini....!
Kila kitu kinawezekana!. Nenda Arusha, mitaa yote mbele ya soko la Arusha ni nyumba za wasomali watupu!, wamezaliwa Arusha, wamekulia Arusha na watafia Arusha! ni Watanzania Wenzetu!.
Nenda umasaini eneo la Ngaramtoni, utashuhudia Wasomali pure, wanaongea Kimasai safi!, wamezaliwa umasaini, wamekulia umasaini na watafia umasaini, ni Watanzania wenzetu!.
Nenda uhindini, kuna watoto wamezaliwa uhindini, wamekulia uhindini lakini hawazungumzi Kiswahili ila ni Wanzania wenzetu!.
Rage ni Msomali Mtanzania mwenzetu!, Kinana ni Msomali Mtanzania mwenzetu na Bashe ni Msomali Mtanzania mwenzetu!. Tusiwasakame bure kutokana na rangi zao!, kuna Warundi, Waganda, Wakenya, Wanyarwanda, Wajaluo, Wazaire, Wamalawi, Wazambia, Wamsumbiji kibao wako kwenye madaraka makubwa serikalini tena wengine mpaka idara nyeti!, wamepose kama Watanzania, hatuwasakami kwa sababu tuu wamefanana na sisi!, kitendo cha kuwasakama Wasomali na Wahindi tuu, huu pia ni ubaguzi mbaya!.
Pasco.