Rafiki yangu wa chuo kikuu

A teller

JF-Expert Member
Feb 6, 2018
490
687
rafiki yangu, umelala? Fumbua macho tafadhali!! Japo kidogo tu John, nikuulize, nataka nikuulize kwanini usingenitafuta labda ningekuwa na kitu cha kukupatia, usingeweza chukua maamuzi haya…ni kweli nilikuwa mbali lakini simu yangu ilifanya kazi mda wote..wewe ndiye ulikuwa rafiki yangu wa pekee nakumbuka ulinitia moyo hasa baada ya kutoendelea kwangu na kidato cha 6 kwani matokeo hayakuwa mazuri kwangu kama ilivokua kwako!

Nadhani nimeshachelewa,moyo wangu unavuja damu, nafsi yangu inauma na mwili wangu unasisimka pindi nikumbukapo rafiki yangu hasa mambo mengi tuliyofanya mimi na wewe rafiki yangu.

Najua upo gizani, na ni giza nene lililotutenganisha tusionane tena, umepotea ghafla katika uso wa hii dunia huku ndoto zako zikizimwa kama mshumaa.

John , Ona sasa, ona ulivoniacha mpweke, muone mama yako anavyolia kwa uchungu, huku fahamu zake zikimtoka na kuzirai mara kwa mara kwani haamini kilichotokea kwani ndiyo kwanza ulibakiza miaka michache umalize shahada yako ya udaktari,pia hata hukupata nafasi ya kumuaga katika hii safari yako, safari uliyoipanga unaondoka lini na wakati gani, John mtazame mdogo wako anavyotokwa na machozi muone John, alikuamini, alikuwa na matumaini na wewe, alikutegemea wewe kama mkombozi wake, kama shujaa wake wa kumpa mfano hai wa kuikomboa familia yenu masikini wewe kama mtoto wa kwanza anayesoma chuo kikuu, yeye baada kufeli darasa la saba.

Waone John wanavyolia, wanavyokulaumu juu ya uamuzi huu wako uliouchukua wa kujitoa uhai mapema kiasi hiki eti kisa tu MAPENZI, muone mama yako alivyoweka tumaini lake kwako, mtazame John alivyosumbuka na kuhangaishana na mgambo wa jiji katika biashara ya pombe, muone alivyopauka, moshi wa kuni huku ukiyafanya macho yake kuwa mekundu ili tu auze pombe upate kusoma, umalize elimu yako ya sekondari…..Ona John, kumbuka wewe ndiye ulikuwa tumaini lake na tegemeo lake akiamini siku moja utabadilisha maisha katika familia yenu.

Mama huyu alikutegemea wewe, kwani aliachwa mjane na baba yako baada ya kufariki akiwa anauguza maradhi yake ya muda mrefu kitandani kwani alikosa pesa ya kufanyiwa matibabu, Ndiye kwanza alikuacha unamiaka 6 tu, huku mdogo wako akiwa tumboni na alivyowaliza watu mara mbili msibani kwani mama yako alijifungua akiwa msibani, najua mda ule ulikuwa hujui lolote lakini ulisimuliwa habari hizi ulipokuwa unakua John, mimi pia nilisimuliwa na babu yangu kwani walikua marafiki sana na baba yako enzi za uhai wake, Mjane huyu alikupenda, alikulinda wewe na mdogo wako Lilian.

Uliapa utasoma kwa bidii zote na kwa nguvu zote ingawaje maisha yalikuwa magumu, ndoto zako ilikuwa uje kuwa daktari. Ni kweli ilikuwa hivo, juhudi zako zilionekana ulifanya vizuri katika masomo yako huku ukiruka viunzi vyote vya uhuni, makundi hatarishi pamoja na mapenzi pia.Ni kweli hukuwahi kushiriki katika matendo hayo maovu, pia na ni kama jinsi ulivowahi kunisomea mafungu kadhaa katika biblia yanayokataza kufanya hivo ukiniambia ni dhambi katika imani yako ya kikristo uliyoiamini tangu tukiwa sekondari. Sasa ulimaliza sekondari na high school pia nyota yako iling’aa pindi ulipochaguliwa chuo, furaha iliyoje kwa familia yenu John?......John nashindwa kuendelea,… nalia tu…

John hivi ni kweli mapenzi yamekuua? John umejitoa uhai kwa kujinyonga, Eti kisa mpenzi wako wa chuo uliyempenda amekuacha? Kama jinsi barua yako inavosema …..miaka miwili tu ilibaki umalize masomo yako ya udaktari, nani aliyekuloga John? kwani nakujua vizuri rafiki yangu ? tulitegemea unarudi na shahadi yako kama zawadi ya matunda ya elimu yako sasa umekuja wewe na jeneza AU John shahada yako utaitumia ahera?.....John nakiri kabisa ulikuwa mtu mwema na ulisoma biblia kwa umakini mkubwa hata kuwasaidia watu juu ya mafumbo ya biblia yaliyoonekana kuwa magumu kwao,.. Lakini John ulisahau…………... Ndiyo naweza sema ulisahau John……... Ulisahau juu ya kuwa na kiasi katika mambo yote…Sheria hii muhimu uliisahau rafiki yangu japo ulisoma sana maandiko………John ulipenda sana…Moyo wako uliutoa wote kwake, tumaini lako ulilitoa lote ukiamini yeye ndiye tulizo la moyo wako, ona sasa alivokufanyia, ona uamuzi uliouchukua bila kujali ungewaumiza wangapi nyuma yako!!!!!…..John ulikuwa imara sana pindi tulipokuwa sekondari, tulipiga soga nyingi sana katika Nyanja zote na mapenzi na mahusiano pia yakiwemo, nakumbuka ulikiri haitokuja tokea maishani mwako kiasi cha kuwa zoba / limbukeni/ kutawaliwa na mwanamke huku ulikiri wazi kuwa wanawake wanapaswa tuishi nao kwa akili bila kusahau ulituhadithia visa kadhaa vya biblia kama kisa cha Samsoni na Delila. John nakumbuka, nakumbuka yote John!!!. Ni wapi ulipoteleza ukashau haya yote rafiki yangu!!!!

Ni kama nipo usingizini naota, natamani iwe ni njozi tu niamkapo mambo yawe shwari nije kwenu nikusimulie njozi hii ya kusisimua inayotia huzuni..Lakini haiwezekani, sidhani kama kuna muujiza utatokea iwe hivo, haya niyaonayo ni ya kweli kabisa, nakuona wewe John umelela usingizi kwenye jeneza lako, ukisubiri hatua za mwisho kufanikisha safari yako katika nyumba ya milele…..John nashindwa kuendelea tena……nashindwa John acha niende mbali nashindwa hata kuuona mwili wako ukishuka mavumbini acha niende mbali kabisa nikae mbali na kwenu……

Ipo siku nitakuja huko gizani ulipo……..
 
ila kujikatisha maisha ni tukio la dk. chache kama hutapata kuyasema yanayokusibu ama kupata mtu wa kukupa ushauri.

kuna watu watabaki sema mbona hili dogo mtu kaamua kukata kamba, pole sana kwako mkuu na familia ya bwana john
 
John kwanini umewatenda hivi ndg na rafiki yako, pole rafiki wa John ulikuwa mbali ndio sababu John alikosa mshauri
 
Back
Top Bottom