FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,867
- 5,064
Ananisimulia Bukembe Mtobo, rafiki wa Muha.
Baada ya mambo kuniendea kombo mjini Arusha au Chuga kama waitavyo wengine. niliamua kukimbilia jijini Dar ili kuunusuru mtaji mdogo uliosalia.
Mwaka mmoja baadae nikiwa jiji Dar mambo bado hayakwenda kama nilivyotarajia. Nilifilisika kabisa.
Ndipo sasa nikalazimika kutumia karata yangu ya mwisho ya ujasiriamali wa kutengeneza vyungu vya kupandia maua.
Nilianza kutafuta eneo huku maisha sasa yakiwa ya kubangaiza hata chakula ni shida.
Niliambaambaa pembezoni mwa barabara maarufu ya Morogoro na kuibukia kwenye moja ya banda kuukuu nikakutana na Dogo mmoja aliyejaaliwa weusi wa kutosha.
Alinisalimia kwani nilikuwa nimemzidi umri kwa mbali tu.
Nikamueleza adhma yangu na moja kwa moja alionesha ananielewa ninachoongea.
Baada ya muda nilijikusanyakusanya na kuanza shughuli zangu.
Eneo lile lilikuwa limesambaa samani tofautitofauti, nyingi ya hizo zilionekana zimeshachoka kwa kunyeshewa mvua na kupigwa na jua muda mrefu.
Baada ya muda Mimi na Bw Muha tulishazoeana ndipo naye akanieleza wakati mgumu anaopitia kwa Bosi wake (mmiliki wa zile samani), Muha analalamika kuwa Bosi amemuweka pale ni karibia mwaka wa pili sasa, suala la malipo limekuwa kizungumkuti. Maisha yamekuwa magumu, anashinda njaa muda mwingi.
Siku Muhusika alipopita pale (maana alikuwa na shughuli sehemu nyingine) nilimsomea mashitaka yake naye alinieleza mambo yalivyo magumu akinionesha zile samani pale zikivyopoteza hata mvuto sasa kutokana na kukaa muda mrefu bila kununuliwa. Nikaishia tu kusema duh.
Mara moja moja Muha alikuwa anatoka na jembe lake akiniambia kuwa ameitwa mahali akapige kazi.
Walau kwa nyakati kama zile Muha anakuwa Mtu mwenye matumaini.
Sasa hata kuni zinakuja na ugali unasongwa.
Siku zikaenda baadae Muha alinifahamisha ya kuwa mmoja wa Mabosi wake (wa kulimiwa) amerejea mkoani, hivyo ile sehemu aliyokuwa anaitwa kulima sasa ataitumia yeye.
Siku zikaenda na kweli sasa Muha alikuwa Bize na tulionana kwa nadra sana.
Miezi ikaenda Muha akanifuata na kuniomba nimfikishie ujumbe Bosi wa zile samani kuwa sasa yeye ameshapata chumba na anaondoka pale.
Mjumbe hauwawi, Jamaa alipigiwa simu alipofika nikampa taarifa na alionekana kusononeka sana ila ndio hivyo afanyeje.
Siku, Miezi, Mwaka sasa Muha yupo Bize, sasa hata ana simu janja na amenunua mashine mpya kabisa Kariakoo ya kumwagilia na mara moja moja jumapili anapita ameulamba akiniambia anaelekea kwenye ibada, ingawa leo atasema anaenda kkkt kesho kwa Mwamposa potelea pote alimradi anaenda iibadani.
Siku moja mchana jua kali nikiwa nimejilaza chini ya kivuli nikaona zile Gari ndogo maarufu kama Kirikuu iikiwa imepakiwa magunia mengi tu, nikawa naitazama inapoelekea kwa upande wa pili wa barabara, Gari ile ilisimama na kuanza kuteremsha magunia yale, kumbe alikuwa Bosi Muha kaleta mbolea ili kazi iendelee Wakazi wa Mbezi waendelee kula mchicha...
Nikatabasamu na nikajiambia mwenyewe kwamba kutoka kushinda njaa siku mbili mpaka tatu leo Muha Kawa bosi analipa Kirikuu ikamchukulie mzigo, nikamalizia kwa kusema kweli mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.
Nikakumbuka kwenye maongezi yetu Muha aliwahi kuniambia kule Kugoma ameacha wanafamilia wake,
nikawaza nikasema siku napata fursa ya kuwasiliana nao nitawaambia ya kuwa ndugu yao sasa ni Bosi huku Dar, anamiliki kipande cha ardhi kando ya barabara kubwa tu.
Ndipo nikasikia kama alarm kubwa inanishtua na kuniuliza,
"ardhi kando ya barabara kubwa?.. Dar.?.. ndio kusema Muha kamzidi hata kina Vunja bei, Diamond".
Kama ni muvi basi hapa ndio ilikuwa kama mgeuko "turning point" kwangu sasa nimekuwa mwenye simanzi kila niliwaza vipi siku Mnyang'anyi yule(Tanroad) atakaporudi kama walivyorudi Wana Israel na ku claim kipande chake cha ardhi kutoka kwa Mpalestina (Muhai?).
Nini hatima ya rafiki yangu Muha ambaye sasa ameshajipata na muda si mrefu anavuta na jiko?.
Kila nikikutana na Muha huyu mwenye matumaini tele ambaye wala hana hata habari kama kuna Tanroad.
Namsaidiaje Muha?