Rafiki yangu amevunja uchumba wangu

Rafiki yangu amevunja uchumba wangu

!
 

Attachments

  • habari mbaya.jpg
    habari mbaya.jpg
    12.7 KB · Views: 34
Hbr wana MMU ?

Bila kupoteza muda niende kwenye mada. Naandiki nikiwa na uchungu mkubwa sana moyoni mwangu.

Ilikuwa tarh 2/1/2019 siku moja tu baada ya mwaka mpya nilirudi nyumba nikitokea Nairobi nilipokwenda kwa shughuli zangu binafsi, nilipofika home nikaoga na kuamua kutoka kwenda nyumbani kwa mpenzi wangu. Huyu mpenzi wangu tulikuwa tumeshaenda mbali sana kiasi cha kuwa nimeshalipa na mahali kwao.

Sikutaka kumpa taarifa kama nimerudi ili nimfanyie surprise kama mjuavyo tena surprise ni kitu cha kawaida kwa wapenzi.

Nilibeba vijizawadi ambavyo nilimnunulia nilipokuwa Nairobi, nikashika njia huyo mpaka home kwake, ilikuwa inaelekea saa tatu usiku Mara huyo nikafika. Nilipokelewa na house girl.

Nilipoingia sebuleni tu house girl akaninong'oneza kuwa mtu yupo chumbani na mpenzi wangu.
Sikuamini Maneno yake nikaelekea chumbani kwa speed kujaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa nafunguo, nikaamua kugonga ilichukua muda kidogo mpaka mlango unafunguliwa.

Alipofungua mlango tu mm nikamsukuma nakuzama ndani, wakati huo yeye alikuwa na kanga moja tu, mara nikakutanisha uso na rafiki yangu kipenzi akiwa kajilaza kwenye Kitanda cha mpenzi wangu huku akiwa kajifunga taulo ambalo huwa nalitumia mm nikilala kwa mpenzi wangu.

Sikuamini macho yangu, nilisimama kwa dakika kadhaa nikiwa sijui cha kufanya baadae nikaamua kuondoka bila ya kusema neno.

Baada ya kuondoka mpenzi wangu alinipigia simu kwa kweli sikupokea alipiga mpaka akachoka. Siku moja baada ya tukio aliamua kunifuata home hakuja peke yake alikuja na wazazi wake kwa kweli niliwafukuza sikuwa tayari kuongea lolote.

Baada ya wiki kupita niliitwa na mshenga akaniuliza kilichotokea nilimueleza kila kitu alichonijibu kama hayo ni kweli huyu hakufai tena .

Alinishauri nikutana naye mbele ya wazazi wake nimpe msimamo wangu, sikusita nilikutana nao nikawaeleza kuwa sitaweza kuendelea tena na binti yao. Mambo yakawa mengi wakaanza kunisihi nisamehe kwa kweli nilishindwa nikainuka na kusepa zangu.

Tangu siku ile wananisumbua sana kila siku kunitumia watu ili niendelee na binti yao kiukweli siwezi kuwa mnafiki moyo wangu hauwezi hili kbsa. huwa sina unafiki kabisa.

Mimi ni mwamnifu sana sijawahi kuwa na mahusiano nje yake iweje Leo yeye anifanyie hivi?

Rafiki yangu kweli umeamua kunifanyia unyama huu woote? Hukumbuki fadhira zangu? Bila Mimi ungekuwa hivyo? Ungekuwa hapo ulipo?

Nimeandika haya kwa lengo la kuwashirikisha ili nitue mzigo wa uchungu nilionao moyoni mwangu.

Sina mpango naye tena hata aje nani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hili nalo neno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii stori ina uwongo na ukweli,pia ni habari ya upande mmoja,mimi nilishakataa kabisa kuamini habari za upande mmoja..hadi aje shemeji nae hapa atoe ushuhuda ili tujue sababu ya haya unayoyatolea shutuma...usikute wewe ndio ulikuwa tatizo na ndio umeachwa unajifariji hapa...
 
Hii stori ina uwongo na ukweli,pia ni habari ya upande mmoja,mimi nilishakataa kabisa kuamini habari za upande mmoja..hadi aje shemeji nae hapa atoe ushuhuda ili tujue sababu ya haya unayoyatolea shutuma...usikute wewe ndio ulikuwa tatizo na ndio umeachwa unajifariji hapa...

Hata kama kuna kipi kitaongelewa na upande wa pili, kama ni kweli alimfumania baaasi
 
Usamehe mchumba kwa fumanizi?? Toka lini


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hata kama kuna kipi kitaongelewa na upande wa pili, kama ni kweli alimfumania baaasi
Ni kweli mkuu,lakini unaamini vipi kwamba huyu jamaa anasema ukweli?
nahisi uzi umejaa uhaya flani..kuna sehemu anatudanganya,wakwe wanampigia kumuomba msamaha??
 
Haya mambo ya kufumania siyataki kuyasikia tena kudadeki, kuna rafiki yangu alinipigia simu niende nikamsaidie. Nilikwenda na rafiki yangu mwengine tukawa tupo 3 kufika eneo la fumanizi jamaa akafungua mlango. Kuingia ndani ile njemba sio ya nchi hii kudadeki inapiga karate kama Bruce lee madafanta, hata sijui tulitoroka vipi mule ndani


Ndukiiiii [emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️
Nimecheka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom