Tena mpaka leo anasema namshukuru sana mr. X kwan bila yeye nisingepata wife material I was looking for
Maneno matamu ya kutongozea hayana ukweli kwenye maisha halisi.
Kuolewa ni jambo la kheri, lakini tujadili aina ya huyo mchumba kwanza.
Mzaha mzaha na ulegevu katika kutafuta mwenza wa maisha,wengi huwagharimu sana,tena sana wanapoanza kuyaishi maisha halisi.
Utakapoolewa na huyo rafiki wa mchepuko wako, nikuulize. Je watakuwa wamevunja urafiki wao kwanza? Ama je kama hawajavunja urafiki wao, baada ya kuolewa nae kwa macho makavu kabisa, huyo mchepuko wako,utabadili gia angani na kumuita shemeji? Utakapokutana nae mkawa wawili utamuita shemeji ivyoivyo?
Marafiki ni sawa na ndugu. Tusikupotoshe, mwanamke yeyote ni mrembo mbele ya macho ya mwanamme na wewe mwenyewe ni shahidi wa maneno haya. Chagua mchumba mwenye haiba na staha isiyokuwa na mawaa,ili baadae usije kujutia maamuzi yako.
Tena huyo (shemeji)rafikiye mchepuko wako, hana adabu "kahuni".
Tabia yake ya kutoheshimu mahusiano ya watu wengine yatakuja kukurudi na wewe. Yawezekana siku moja akaja "kumla" hata ndugu yako kwa visingizio vya kitotototo! Huu uzi ulioleta,unafanana na yaliyompata rafiki yangu,miaka imepita.
Alipata mchepuko akaubeba ad "gesti" alikoacha marafikizake. Walipofika wakamshawishi huyo mchepuko kuwa wote wanamtaka, si kwa kulazimisha bali kwa maelewano,kwa hiyari yao na kwa hiyari yake wote wakakubaliana "wakamla" kwa zamu.
Hakuna kesi ya ubakaji'apo ila likaja tatizo. Katika "fujo"hiyo rafiki yangu akanogewa akaamua asogeze kabisa, namaanisha kuoa!
Kimbembe kikaja walipoanza maisha halisi.
Wale jamaa zake wakawa wakifika pale kwake wakimkuta huyo "shemeji" yao wanamsalimia shemeji yao kwa kebehi huku wakicheka. Hakuishi kwa amani ajili ya kumbukumbu ya dhambi yao ya "asili". Walizaa watoto adkufikisha wawili,lkn baadae walikuja kuachana kwa sababu ya kutokuwa na amani ktk ndoa yao.
Mifano ni mingi,huo ni mmoja,lakini kiuhalisia hapo ndoa haipo,labda ungesema huyo shemeji mchepuko amekuvutia unataka kupiganae uhuni.