Rafiki wa Lowassa ashikwa vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rafiki wa Lowassa ashikwa vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Aug 12, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Habari zilizonifikia punde zimesema kuwa rafiki mkubwa wa MH. waziri mkuu mstahafu EL, Mheshimiwa Pelo amepatikana na kashfa ya kuleta mganga wa kienyeji toka mkoa wa Manyara na amekamatwa usiku wa manane kata ya Makuyuni ambapo mh. Pelo aliyekuwa diwani kapigwa chini katika kura za maoni.

  Je alikuwa anakusudia kumdhuru nani? Polisi walipomhoji mchawi mwenyewe alisema kaletwa na Pelo kuendesha kampeni zake ili apate ushindi katika marudio ya kura. Katika sakata hilo, pia mhudumu wa mahakama kakamatwa na kadi za CCM za Mh Pelo kugawia watu ili wapige kura.

  Source, RPC-Arusha. Mlioko monduli tupeni habari timilifu.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sasa hapo wapi iliposema ni rafiki yake Lowassa..ushabiki mwingine wa kipuuzi sana
   
 3. M

  Msharika JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu ndugu ni rafiki wake mkubwa sana , na inajulikana siyo siri, alikuwa mwenyekiti wa alimashauri monduli
   
 4. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 994
  Trophy Points: 280
  Kwenye matukio kama haya ndiyo utajua waganga ni matapeli.

  Mosi, kama kweli ana nguvu kama anavyodai angeweza kujua polisi wanakuja.
  Pili, kama ana uwezo wa kufanya hayo Pelo aliyokuwa anataka afanye;kufanya wapiga kura wamchague Pelo katika kura za marudio kwanini asitumie nguvu hiyo kuwapumbaza mapolisi wamwachie.
   
 5. k

  kipuyo JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2010
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 1,143
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa ameshatofautiana na mh EL muda mrefu sana na ndio maana amepigwa chini
   
 6. T

  Taso JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Yeye mwanga ndio aliowapa hao polisi nguvu ya kumkamata. Hata Yesu aliambiwa jifungue hiyo minyororo ka we kweli mwana wa Kikwete wa Mbinguni, halafu akapigwa bonge moja la mjeledi pwaaaaa! Wanafunzi wakasema, Yesu eeh, mbona tunapewa kisago na wewe uko hapa hapa tena we ndio unaongoza kwa kipondo, huna namba ya babako uagize defender za usalama wa Taifa la mbinguni zije kutu rescue?

  Yesu akasema "baba yangu wa mbinguni ndio kawapa nguvu ya kunipa kisago, ili neno la manabii litimie."
   
 7. B

  BigMan JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Na Mwandishi Wetu Arusha

  Mganga wa kienyeji , Mussa Slaa (55) mkazi wa Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo baada ya kutuhumiwa kwa vitendo vya uchawi na wananchi.

  Mganga huyo anatuhumiwa kuchota udongo kwenye vituo vya kupigia kura kwa lengo la kumsaidia mgombea udiwani wa kata ya Makuyuni,Daudi Pelo ashinde katika kura za maoni.

  Wananchi wa kata hiyo ya Makuyuni, wamewaeleza waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo alikwenda katika kituo cha kupigia kura cha Naiti kisha akaenda kituo cha Makuyuni na Mbuyuni, akiwa na mpambe wa Pelo Meshuki Laizer wakitumia pikipiki.

  Walidai kuwa wakati wakiwa huko wananchi waliwashitukia na wakaanza kuwafukuza ndipo mpambe wa mgombea huyo aliacha pikipiki na kukimbia na Mganga huyo alitiwa mbaroni na wananchi na kuanza kumpiga mpaka akawaeleza ukweli, kuwa ametumwa na meshuki Laizer, ili ampe dawa za ushindi mgombea wake katika kura za maoni.

  Aidha wananchi hao walidai baada ya kupata maelezo hayo wakaamua kumpa kibano cha nguvu na mara polisi wakatokea na kumchukua hadi kituoni.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha,Basilio Matei alidai kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 11 mwaka huu majira ya saa 11. 00 alfajiri, huko Makuyuni.

  Alisema Mtuhumiwa huyo akiwa na mkoba wake, alifika eneo la Makuyuni na kuanza kufanya ushirikina na ndipo wananchi wakamkamata na kuanza kumpiga.

  Alisema kutokana na kichapo hicho sangoma huyo ilimpasa kueleza ukweo kuwa ametumwa na Meshuki Laizer ili atengeneze dawa za mgombea kiti cha udiwani David Pelo wa kata hiyo ili ashinde kiti hicho cha udiwani

  Alisema kuwa baada ya kuwaeleza hivyo wananchi walimlazimisha kula dawa walizomkuta nazo na polisi walipopata taarifa na kutinga eneo hilo la tukio, wakamkuta na hirizi tano, mikia miwili ya nyati na dawa za kienyeji mbalimbali.

  Wananchi hao walieleza walimchukuwa mtuhumiwa huyo mpaka kituoni lakini hawakumfungulia shtaka la uchawi kwa madai hawana ushahidi na badala yake wamemfungulia shtaka la kukutwa na nyara za serikali

  Hata hivyo mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa hadi hapo atakapofikishwa mahakamani.

  David Pello aliyekuwa diwani wa kata ya Makuyuni kwa miaka zaidi ya ishirini na pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli na ameangushwa Abdillahi Ally Warsama.

  Mwisho
   
Loading...