Nimekuwa mfuatiliaji wa mikasa ya watu humu leo na mimi nikaona nilete jambo langu linalonitesa kwa muda mrefu ili nijue nini cha kufanya. Mimi ni binti niko ndani ya ndoa, wakati naolewa mume wangu alikua na rafiki yake wa kike ambaye wenyewe wanadai urafiki wao ni wa kawaida tu kwani wanajuana muda mrefu. sasa tatizo huu urafiki wao umekuwa kero kwangu yani ni ule urafiki uliopitiliza kiasi kwamba kilasiku nikiangalia kwenye cm ya Mr lazima nikute wamewasiliana hata mara 50 text ndo usiseme. Kila sehemu wanaenda wote na huyo binti yani kama kumbikumbi mimi niko chuo wakati mwingine nikiwa chuo nikirudi hom namkuta huyo binti na Mr sebuleni inamaana ana courage ya kuja kwangu mimi nikiwa sipo, mara nyingine weekend tuko nyumbani na Mr, binti anampigia Mr cm njoo nyumbani kwangu ule nimepika, mume naye kilasiku lazima aripoti nyumbani kwa binti, mara binti aje nyumbani kumpitia Mr amsindikize sehemu, wakati mwingine tumelala weekend asubuh saa 1 binti kapiga cm kwa mr unafanya nini amka twende kwa fulani {mshikaji wao} yani full tafrani hana adabu kabisa ila nilichogundua ni kua mr nae ndo anampa ujeuri coz kuna kipindi niligombana sana na huyu binti kuhusu tabia zake huwezi amini alinijibu kuwa mimi siwezi kuwatenganisha kamwe nikitaka nimwambie mume wangu ndio ampige yeye marufuku kua na ukaribu nae ila sio mimi. Jamani cm wanapigiana mpaka saa 6 usiku. wenyew wanadai wao ni marafiki wa kawaida tu na hakuna kinachoendelea. nimejaribu kuuvunja urafiki huo unaoniumiza nimeshindwa mimi wenyewe hawana hata habari. Je kuna urafiki wa aina hii kweli kati ya mwanamke na mwanaume tena mume wa mtu? kwanini kusiwe na mipaka jamani..Huyo mwanamke ni mjeuri hatari ukimwambia anakujibu kwa dharau sana, mume naye ndo kwanza hana habari nisaidieni jamani nifanyaje?
karibu mto linguse nguse tuvie samaki