Rafiki wa Ex wangu ananitongoza

Rafiki wa Ex wangu ananitongoza

Mara nyingi, Wanaume huwa hawagombani kisa wanawake.
Kuna nafasi kubwa jamaa amepewa mchoro aje aipige. Na ataipiga tu afu atasepa.

Siku moja katika matembezi yako utawakuta wakila bata na kufurahia. Wewe utabaki unaona haya.
 
Yalinikuta hayo, demu aliyezaa na mshikaji wangu tena wakaishi PIKA PAKUA, ananitaka mpaka leo hii, nishamchana sasa siokoti simu zake wala kujibu msg.
Japo mchizi kwa sababu ya harakati zetu, sio kama miaka mi5 nyuma ila bado siwezi famya umafia huu.
 
Lamomy alisema niendelee kushea episodes za maisha yangu, basi leo kuna jambo limenitokea na hapa ndiyo pa kusemea.

Iko hivi, mnajua nimeachana na yule mwanaume bondia, sasa huyo Ex wangu alikua na rafiki yake wa karibu sana ambaye wamekua wote tokea wadogo, familia zao ni marafiki yani ni kama ndugu tu na tulikua tumezoeana sana ananiita shemejiakeee.

Huyo kaka alikua mchechi sana na alikuwa anakuja home kwa Ex wangu, wanaangalia mpira pamoja, wakati mwingine nawapikia na yeye ndo ambaye wakati mwingine nilikua namlalamikia matatizo ya rafiki yake.

Aliomba tukutane nimsimulie nini kimetokea mpaka uhusiano wangu umefikia mwisho. Leo mchana nimekutana naye nikamsimulia, amenisikiliza, akanipa pole halafu akaanza kunitongoza. Amesema amekuwa ananipenda wakati wote ambao niko na rafiki yake ila ni heshima tu ilimfanya ajizuie. Amesema yuko tayari kwa lolote na yeye yuko serious anataka kunioa.

Nimechoka maana nilifikiri wanaume hawatongozi wala kutaka kuoa maEx wa rafiki zao ambao ni sawa na ndugu.

View attachment 3307399

Mimi simuamini na bado siko tayari kwa mahusiano ila kama ni wewe, ungefanyaje?
Mkubalie
 
Back
Top Bottom